Magufuli na mradi wa laptop kwa kila mwalimu,hivi tatizo ni ukosefu wa laptops?

Status
Not open for further replies.

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,384
Katika gazeti la Raia Mwema toleo no.418 ipo habari ya Mgombea Urais wa CCM kuwa eti atawapatia walimu wote laptops ili kuinua kiwango cha elimu,na labda kwa fikra zake,kuondoa umaskini nchini...

Nikiwa mwalimu,ahadi hii inanikera,hivi anafikiri sisi ni wapuuzi kiasi hicho cha kufikiri kuwa tutaipigia CCM kura kwa ahadi ya laptops?Na OK,ni lini katika madai ya msingi ya walimu kwa serikali kwamba kukosa laptops kumewahi kuwa tatizo?Na hivi katika ilani ya uchaguzi ya CCM kugawa laptop ndicho kipaumbele?

Na basi tukubaliane kuwa tunataka laptops,zitasaidia vp kuinua kiwango cha ufundishaji?Iko wapi miundombinu ya ku-support hiyo project?Mradi wa JK wa Tanzania & Beyond uko wapi?

Kwa ufupi,mradi wa laptop umekwama Kenya na ulikwishakwama Nigeria...Mh.Magufuli kama hakujiandaa kugombea urais au kama mafuriko ya UKAWA yanamchanganya basi atangulie tu jehanamu,moto umewaka...waalimu hatuna mpango na CCM na kama haelewi basi aendelee kubwabwaja na mradi wake wa laptop

=================

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kutoa kompyuta mpakato (laptop) kwa kila mwalimu hapa nchini na shilingi milioni 50 kwa kila kijiji, kwa ajili ya kukuza uchumi endapo kitashinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM iliyopitishwa na Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika mwezi uliopita, ahadi hizo zitatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya mgombea wa chama hicho (2015-2020), John Magufuli. Kwa maana hiyo, mgombea huyo atapaswa kuwaambia Watanzania maneno hayo wakati wa kampeni.

Magufuli atakabidhiwa ilani hiyo wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) uliopangwa kufanyika mjini Dodoma kati ya Agosti 12 na 13 mwaka huu, mjini Dodoma.

Hatua hiyo ya CCM kutoa laptop kwa walimu ni tofauti na ilivyozoeleka katika nchi nyingine kama Kenya na Rwanda ambako serikali zake zinatoa kompyuta hizo kwa wanafunzi.

Raia Mwema limeambiwa na vyanzo vyake kuwa mpango wa kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji hapa nchini una lengo la kupunguza tatizo la ajira na kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati Maalumu iliyotengeneza ilani ya chama hicho kwa ajili ya kipindi cha mwaka 2015-2020, January Makamba, alilithibitishia gazeti hili Jumatatu wiki hii, kuwa ilani ya CCM iko tayari na imezungumzia mambo mengi ya msingi yakiwamo hayo aliyoulizwa na gazeti hili.

"Ilani iko tayari na mgombea atakabidhiwa kwenye mkutano ujao wa NEC. Siwezi kusema mengi kuhusu hiyo ilani lakini naweza kukuhakikishia kwamba ni ya kisasa, kibunifu na inayokidhi mahitaji ya sasa ya taifa letu," alisema.

Akieleza kuhusu kompyuta mpakato hizo, January alisema zitakuwa na uwezo wa kutumia nishati ya jua (solar) ili kuwafanya walimu waliokuwepo kwenye maeneo yenye shida ya umeme kuweza kuzitumia pasipo shaka.

"Ilani hii imezingatia mazingira ya nchi yetu kuwa kuna maeneo ambako umeme ni tatizo. Hivyo kompyuta hizo zitakuwa na uwezo wa kutumia nishati hiyo ili walimu waweze kuzitumia mara zote.

"Pia, kompyuta hizo zitakuwa zimewekwa kabisa vitabu na mambo mengine ya kusaidia walimu kufundisha hivyo hawatakuwa wanapewa mashine pekee bali na vifaa vingine vya kazi," alisema Makamba.

January alisema kompyuta hizo zitagawiwa kwa walimu wote waliopo nchini na kuwa CCM imeona ni vema walimu kwanza wakawezeshwa kiteknolojia kabla ya kuelekea kwa wanafunzi kwenye awamu nyingine.

"Tunafahamu ziko nchi ambazo wameamua kuanza na wanafunzi. Sisi tumeona tuanze na walimu kwanza ili iwe rahisi kwao kuwafundisha wanafunzi wakati CCM itakapoanza mpango maalumu kwa watoto," alisema Makamba.

Mbali na January, wajumbe wengine wa kamati hiyo ya wataalamu iliyoongozwa na Waziri wa Kilimo na Chakula, Steven Wasira, walikuwa ni Anamringi Macha (Katibu), Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Ummy Mwalimu na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali-Zanzibar, Ali Juma Shamhuna.

Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Anthony Mavunde, Mbunge wa Manyoni Mashariki, Kapteni (mstaafu) John Chiligati na Mbunge wa Morogoro Mjini, Aziz Aboud.

Kuhusu suala la shilingi milioni 50 kwa kila kijiji, Makamba alisema fedha hizo zitatolewa katika kipindi cha miaka hiyo mitano na zitakuwa za mzunguko ili kusaidia watu wengi zaidi kufaidika.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Tanzania ina takribani vijiji 19,200 na kama serikali itatoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji, maana yake ni kuwa itahitaji kuwa na kiasi cha shilingi bilioni 900 katika muda huo.

January alisema mtindo na utaratibu utakaotumika kwa ajili ya kutoa fedha hizo za uwezeshaji vijijini utaelezwa na kufafanuliwa vizuri wakati kampeni zitakapoanza rasmi.

Lowassa na Magufuli
Makamba ambaye pia alijitokeza kuwania urais kupitia CCM katika kinyang'anyiro cha ndani ya chama, alisema chama tawala hakina hofu na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ambaye atashindana na Magufuli kuwania urais; yeye akitumia tiketi ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akizungumza kwa kujiamini, Makamba alisema kinachoonekana katika matukio ya karibuni ya Lowassa ni sawa na uigizaji na hivyo wao CCM hawana sababu ya kuhofia chochote.

"Sisi katika chama tunaamini kuwa kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere angekuwa hai leo na kungekuwa na wagombea hawa wawili; Lowassa na Magufuli, bila shaka angemchagua John Pombe Magufuli. Hili halina shaka.

"Mgombea wetu Magufuli anauzika. Ilani yetu mpya imejaa mambo makubwa mapya yatakayotoa matumaini kwa mamilioni ya Watanzania ambao wana imani kubwa na Chama Cha Mapinduzi pamoja na mgombea wake.

"Tutafanya kampeni ya nyumba kwa nyumba. Si tu ya maandamano na mikutano ya hadhara. Mtandao wa kufanya hivyo tunao na hatubahatishi. Sijui wenzetu wana ilani gani lakini yetu iko tayari na wakati utakapofika tutawaeleza wananchi kila kitu na nukta hadi nukta," alisema.

Maandalizi ya Ilani
Ukiondoa CCM, vyama vingine viwili; ACT Wazalendo na Alliance for Democratic Change (ADC) ndivyo pekee ambavyo hadi vimekamilisha mchakato wa uandaaji wa ilani za uchaguzi.

Hadi sasa, haijafahamika kama mgombea urais wa Ukawa, Lowassa, atatumia ilani ya uchaguzi ya Chadema alichojiunga nacho au umoja huo utatengeneza ilani inayojumuisha mawazo na matamanio ya vyama vyote vinne vinavyounda umoja huo.

Vyama hivyo ni Chadema, NCCR Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF) na National League for Democracy (NLD).


Chanzo: raiamwema

Update;

Hii habari imekanushwa. Mh. Magufuli hajaahidi Laptop Nchi nzima.
 
Last edited by a moderator:
Umeme uko wapi wa kuchajia hizo Laptops?Dar umeme ni shida jiji kubwa sembuse vijijini?
Walimu hizo laptop mtachajia kwenye udongo wakati wa mchana.Jamani hii nchi ni shida sana,kwa bei ya GPSA laptop ni tsh2,800,000/=sasa walimu wako wangapi?kwa nini hizo hela msipeleke kwenye miundombinu muhimu?
CCM kweli hawana vipau mbele kukimbizana na kasi ya ukuaji uchumi.
 
Umeme uko wapi wa kuchajia hizo Laptops?Dar umeme ni shida jiji kubwa sembuse vijijini?
Walimu hizo laptop mtachajia kwenye udongo wakati wa mchana.Jamani hii nchi ni shida sana,kwa bei ya GPSA laptop ni tsh2,800,000/=sasa walimu wako wangapi?kwa nini hizo hela msipeleke kwenye miundombinu muhimu?
CCM kweli hawana vipau mbele kukimbizana na kasi ya ukuaji uchumi.

Roho mbaya inakusumbua.
 
Hizi ni ahadi za kipuuzi sana, je hao walimu amewajengea nyumba za kutunzia laptop, na je anauhakika na umeme wa uwasha hizo laptops? Kama wameshindwa kununua madawati na kulipa mishara wataweza laptops au ndo nafasi ya rushwa anajaribu kujitengenezea? Mi na mke wangu ni walimu lakini hatuna kipaumbele cha laptops tulinunua miaka 5 iliyopita na zimetunzwa kwani kijijini tunapofundisha hakuna umeme
 
Serikali ya ccm imezoea kuwachezea walimu kila wakati wa uchaguzi kwa shilingi 10,000 kwa siku , nao walikuwa siku zote hawajitambui wakidhani ndio wameula. Kama walimu wenyewe wanajibu kwa Magufuli namna hiyo sasa najua nao walimu wameamka na wanataka kujikomboa. Shikamoo walimu!
 
Kama ni hivyo huyu jamaa ameanza ubinafsi wake nilikuwa nausikia, nafikir anafanyahivyo kwa vile wake zake ni walimu, si mnaona alipereka mataa ya kuongozea nagari chato na huku akijua majiji kama mwanza, arusha, mbeya na tanga hakuna mataa, aliko weka mataa hayo GARI moja upita kila baada ya dk 40.Simnakumbuka alipindisha barabara ya lami badala ya kupita wilani akamua ipite kijijin kwake wakati huo, lengo hapo ni kufurahisha watu tu pasopokujua hizo furaha na gharama kwa taifa na wala azisaidii kitu kwa uliowapa
 
tangu nimeajiliwa huku kijijini nimemisi fesibuku baada ya kale kasimati foni kangu kukauza kwa kucheleshewa ka mshahara kangu... sasa siwezi kununua tena.. makufuri leta hizo laputopu nianze kufesibuka..hata darasani sitaingia kufundisha...mb zikiisha naangalia movie weee... nakumbuka chuo nilipenda series za kikorea... ccm hoiiiii...samahani hoyeeee
 
Yaani akisema atamaliza tatizo la madawati ningemuona wa maana! hizo laptops ni ndoto za mchana tu anaota!
 
Huyu ....mgombea wa ccm hajui matatizo ya wananchi ,ndo maana anataka kuwapa walom vitu ambavyo kwao hivina maana....Inabid Edo amfundishe amebeba agenda ya walim..nakumbuka wakati anachangia saccoss ya walim pale moshi vijijin alikuwa anagusa agenda zao ..walom mpen kura zen edo ...amebeba agenda zenu.....huyu akiwaletea hela kulen....aliuza nyumba ,,leo hii hamna nyumba za kuishi....polen..sana walimu....
 
ungemuuliza je msipomchagua atawapa laptop,? kama hapana basi ni kwamba anataka kuwahonga aende ikulu
laptopvkwa sasa haiwez kumpeleka ikulu magufuli lbd bao la mkono
 
Mwaka huu magamba yatakufa...Thread zote yanayoanzisha yanamuongelea Rais Edward Ngoyai Lowassa.....na sisi hatuna habari....tunapata upepo wa bahari....mwaka huu si wa propaganda kwetu maana ukweli tulishauongea wananchi wakauelewa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom