Magufuli ampa mkandarasi miezi sita

Mallaba

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
2,554
47
WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli, amempa miezi sita mkandarasi kukamilisha ujenzi wa barabara ya Nyamwage-Somanga, yenye urefu wa kilomita 60.
Dk Magufuli alisema mkandarasi huyo hana sababu ya kutoa visingizio, kwani urefu uliobaki ni mfupi hivyo ahakikishe anakamilisha haraka barabara hiyo haraka.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, kwenye hafla ya kusaini mikataba ya ujenzi kati ya Wakala wa barabara nchini (Tanroads), wakandarasi na wasimamizi wa ujenzi, Dk Magufuli aliwataka wakandarasi nchini kuache kuripua ujenzi wa barabara.
Kuhusu ujenzi wa barabara ya Kilwa, Dk Magufuli alisema eneo lililobaki ni dogo, hivyo mkandarasi hana sababu ya kuchelewesha barabara hiyo.
“Ninataka barabara hii mtu aweze kusafiri kutoka Lindi, Mtwara mpaka Bukoba bila tatizo lolote akiwa juu ya lami, mkandarasi hana kisingizio chochote cha kuchelewesha barabara hiyo, kwani ni kilomita 60 tu zilizobaki,” alisema Dk Magufuli na kuongeza:
“Kilomita 60 ni umbali mfupi mno unaweza ukatumia bajaji, baiskeli, teksi, baada ya miezi sita barabara hiyo iwe imekamilika.”
Dk Magufuli aliwataka wakandarasiwasichukulie Tanzania kama shamba la bibi na kuonya kuwa, sheria zitatumika na wasipofanya kazi inavyostahili na kwa viwango vinavyokubalika, waondoke na wafutiwe mkataba.
“Siku za nyuma gharama za ujenzi wa barabara zilikuwa chini, ila wakandarasi wamefanya ujanja na kupanga bei za juu na watendaji badala ya kutafuta anayefanya kazi kwa ufanisi kwa kiwango kidogo cha bei, mnakimbilia bei kubwa,” alisema.
Katika hatua nyingine, Dk Magufuli aliwataadharisha watu waliojenga maeneo ya akiba ya barabara kuwa sio sahihi, kwani ni hatari kwao wakibomolewa, hawatalipwa chochote.
 
hapa nimeachwa kidogo na hii habari , napenda kuuliza wana JF , hivi ni possible kutokea Lindi/Mtwara hadi Bukoba?
maana najua hiyo mikoa iko kusini na mwingine ni kaskazini
au ni nini amabcho sikukuelea vizuri?
 
Umeelewa vizuri. Ni kwamba waziri anataka mtu asafiri bila shida, akiwa juu ya lami, safari hiyo yote kutoka kona ya kusini kabisa ya nchi hadi kuona ya kaskazini kabisa, Lindi mpaka Bukoba. Njiani asikumbane na vipande vya tope na makorongo (mahandaki).
 
ooh hapo nimekuelewa mkuu
Umeelewa vizuri. Ni kwamba waziri anataka mtu asafiri bila shida, akiwa juu ya lami, safari hiyo yote kutoka kona ua kusini kabisa ya nchi hadi kuona ya kaskazini kabisa, Lindi mpaka Bukoba. Njiani asikumbane na vipande vya tope na makorongo (mahandaki).
 
Back
Top Bottom