Magomeni garden ya serikali kujengwa bar

Babu Ubwete

Senior Member
Jan 26, 2008
169
29
Nimeona kuna ujenzi wa Bar Katika eneo la Botanic Garden ya Magomeni, Wahusika Halmashauri ya wilaya na Maliasili mnalionaje swala hili lina manufaa kwa wakazi wa Jiji la dsm. Faida Kubwa ya baa ni bora kuliko kuwa na Bustani ya kupumzikia na kuleta hewa nzuri kwa wakazi?
 
Ile Botanic garden ya Africana kuelekea Whitesand mh. Londa aliiuza kwa Wahindi na hii ya magomeni mnataka kuiza kwa mchaga? TZ bila Ufisadi inawezekana.
 
Haya ndio maisha Bora kwa kila Mtanzania

Chukua Chako Mapema (CCM)

Na mimi naenda dukani nikanunue vifaa vya ujenzi naeda kujenga bar katika Garden ya IKULU magogoni.

Natafuta mafundi wa ujenzi,

Niliahidi.jpg

Skeleton.jpg

TANZANIA HADI MWAKA 2015 TUTARUDI KATIKA UKOLONI.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Nkuu wa Wilaya ya Kinondoni mpya ndio ameanza kwa kuuza Magomeni Garden????

amekuja na Speed kali kweli!!!!

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Hilo eneo ni garden na wiki iliyopita mama Tibaijuka waziri wa makazi alifika eneo hilo na akamuagiza mkuu wa wilaya aliye pita kupeleka watu wa ramani kupima hilo eneo na kusitisha ujenzi mpaka jibu litoke hata mimi siaafiki ujenzi wa bar magomeni kuna bar nyingi sana
 
Waziri wa ardhi nyumba makazi prof. Anna Tibaijuka alitembelea eneo hilo baada ya wakazi wa kata ya magomeni kumuandikia barua mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni kumtaka aivunje baa hiyo inayojengwa na kuwafikisha mahakamani wavamizi hao, alitoa maagizo kwa maafisa Ardhi wa manispaa kuipitia ramani ya mipango miji ili kubaini eneo husika linasomeka kupaswa kuwa na nini.
barua hiyo inayoonyesha nakala wamepewa madiwani, wabunge wanaoingia kwenye vikao vya manispaa ya kinondoni na mstahiki meya pia.
kuna habari kuwa kamati ya siasa ya ccm kata ya magomeni imepiga dili hilo na kumpa mjenzi huyo wa baa ambaye wengine wanadai ni mtoto wa Bernad Membe huku wengine wakidai ni nyumba ndogo ya Idd Azan kwa madai kuwa eneo hilo ni la tanu walipewa na Kawawa!!!!!
Hata hivyo kwa mujibu wa ramani waliyokuwa nayo wakazi hao wa kata ya magomeni, eneo hilo linaonyesha kuwa ni barabara inayounganisha kutoka mtaa wa uwarani na chemchem kutokezea kawawa road! nitajaribu kuipata hiyo barua na sehemu ya ramani hiyo mpate kuidadavua!!!!!!!!!!
CCM ITAENDELEA KUWA ADUI WA WANANCHI NA HAWAWEZI KUTUSHAWISHI KUWA INAYATENDA WAYATAKAYO WENYENCHI.
 
Nimeona kuna ujenzi wa Bar Katika eneo la Botanic Garden ya Magomeni, Wahusika Halmashauri ya wilaya na Maliasili mnalionaje swala hili lina manufaa kwa wakazi wa Jiji la dsm. Faida Kubwa ya baa ni bora kuliko kuwa na Bustani ya kupumzikia na kuleta hewa nzuri kwa wakazi?

Wakazi wa kata ya magomeni waliomba hilo eneo kwa mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni wajenge sekondari ya kata yao wakanyimwa kwa maelezo kuwa hilo ni eneo la wazi, inashangaza ofisi hiyo hiyo ya mkurugenzi inafumbia macho uvamizi ijengwe baa.
 
Hilo eneo ni garden na wiki iliyopita mama Tibaijuka waziri wa makazi alifika eneo hilo na akamuagiza mkuu wa wilaya aliye pita kupeleka watu wa ramani kupima hilo eneo na kusitisha ujenzi mpaka jibu litoke hata mimi siaafiki ujenzi wa bar magomeni kuna bar nyingi sana
Da asavali bar ijengwe kwani hiyo bustani imekuwa ''Masinde Muliro garden ya bongo''
 
Inakupatia picha halisi ya AKILI ZA VINOGZI WETU!!!! Kujenga shule WAMEKATAA; BAR WAMEKUBALI KWA KUWA NI INCOME GENERATING NA WATAKUWA NA CHANZO CHA MAPATO ili WAPATE PAKUIBA.....
 
jengeni jengeni, si tunbar, bali wajenge bar n guest house kabisa.

Ndo wakati wao huu............

Wasipovuna sasa hawatavuna tena
 
Back
Top Bottom