MAGEREZA: Si kweli kwamba mfungwa akihukumiwa miaka 30 basi itahesabika usiku na mchana

Askari wa Magereza ni rafiki sana wa wafungwa. Askari Magereza ni tofauti kabisa na Polisi. Askari magereza ni kati ya makundi yanayotambua kwamba maisha hayana mwenyewe na alipo mfungwa basi kesho anaweza akawepo yeye. Tofauti kabisa na Polisi, Polisi wajuacho ni wao ni wao, na wanajua kwamba hakuna meingine zaidi yao.
Anayesababisha magereza/jela iwe na picha iliyojengeka kwa jamii ni wafungwa wenyewe na viherehere manyapala.
Otherwise heshima kwenu askari magereza, naikubali sana kazi yenu ni nzuri kwa kweli.
Ila kabla sijaondoka nina kaswaki ka kizushi. Hivi ni kwa nini ni nadra sana kukosa askari wenu kadhaa wakifuga bata kwenye makambi na kota zenu? Kuna mahusiano gani kati ya bata na Magereza?
 
View attachment 622442

Studio za Radio Times Fm wapo SACP Charles Novat, ASP Deodatus Kazinja kutoka Jeshi la Magereza nchini wakieleza kuhusu hali Magereza na wafungwa.

Ufuatao ni mtiririko wa mahojiano yao na Waendeshaji wa kipindi cha Maisha Mseto

Magereza hayapo ili kumuongezea mfungwa adhabu, tupo kuhakikisha mfungwa anatimiza adhabu aliyohukumiwa na mahakama. Ni jukumu letu kuhakikisha mfungwa anatoka na afya njema kama ambavyo aliingia nayo.

Wafungwa wote ni sawa, hakuna mfungwaa VIP. Huduma zote hupata sawa ispokuwa kwa wenye matatizo ya afya. Wafungwa wanapata taarifa, kuna TV na magazeti. Ni haki yao.

Nyampara ni kiongozi wa wafungwa ili kuongoza wafungwa wengine. Ni kiungo kati ya askari na mfungwa. Nyampara ni kama internal mechanism ya kuwafanya wafungwa wabadilike,

Nyampara hana mshahara isipokuwa anakuwa favoured kwenye vitu vidogo vidogo tu, ni sawa kama ilivyo kwa kiranja kwenye mashule.

Tunawatenga wafungwa kutegemea vitu mbalimbali ikiwemo umri wa mfungwa, jinsia na idadi ya vifungo.

Watu wanachanganya shule za maadilisho na magereza. Wanaopelekwa kule sio wafungwa. Mtoto haruhusiwi kupelekwa gerezani ispokuwa pale utata inapojitokeza.

Wafungwa/mahabusu wa kike wanapata huduma kama sheria inavyosema,Wapo watu binafsi wanaleta misaada kuwahudumia,hatukatai. Magereza hatuko kwa ajili ya kudhalilisha utu wa mfungwa.

Ufanisi wa mkuu wa gereza huonekana pale ambapo gereza linakabiliwa na changamoto. 1995 Wafungwa waliwahi kupiga kura, tulifanya utaratibu na wafungwa walipiga kura.

Changamoto ni kupata vituo vya jirani na gereza, pia wafungwa hujiandikisha kwenye vituo tofauti na magereza waliyopo. Sheria haikatazi mfungwa kupiga kura, ni utaratibu tu ambapo Tume ya Uchaguzi ikiandaa basi sisi tutafuata maelekezo.

Ikitokea mfungwa amefiwa na ndugu yake wa karibu, hakuna uwezekano wa kuhudhuria, utekelezaji wake ni mgumu kutokana na usalama

Sisi tuna vyuo vya ufundi, mfungwa anafundishwa ufundi stadi na kuzalisha vitu mbalimbali ikiwemo samani. Kutoa mitaji kwa wafungwa ni jambo jema lakini utekelezaji wake hautokuwa rahisi.

Kiutaratibu mfungwa akishiriki kwenye uzalishaji kuna kiwango flani kinatengwa kwa ajili yake ili kuwa motisha kwake.

Kuna wafungwa wana uwezo mbalimbali, inakuwa ngumu kutumia kutokana na ukosefu wa vitendea kazi, mazingira na uhalisia. Gerezani ni sehemu ya mpito, tunategemea mfungwa arudi uraiani akiwa na mawazo ya kutokurudia makosa yake.

Kwa mazingira yetu mfungwa hawezi kukutana na mwenzi wake faragha, lazima iwepo miundombinu mahususi. Nchini kwetu haipo! Lakini tukiruhusu wakutane kimapenzi kati ya mfungwa wa kikee na mkmewe, vip akipata mimba? nani atalea?

Gerezani hakuna mazingira yanayoruhusu mapenzi ya jinsia moja, kama ikitokea wale ni binadamu, siwezi sema halitokei. Tumejitahidi kuweka mazingira ambayo hayatofanya hili jambo litokee, kama wakifanya ni haramu na makubaliano ya watu wawili.

Tuna utaratibu wa kuendeleza vipaji, ikitokea ana kipaji na gereza lina uwezo wa kukiendeleza basi tutamuingiza kwenye program. Kama kuna prodyuza anataka kurekodi nyimbo na wafungwa basi alete maombi na utaratibu utafuatwa.

Mfungwa akihukumiwa toka siku ya kwanza anapata 1/3 ya kifungo chake, lakini anapaswa aishi kwa nidhamu na kutii sheria. Si kweli kwamba mfungwa akihukumiwa miaka 30 basi itahesabika usiku na mchana.

Tunatoa wito kwa jamii kuwapa nafasi wafungwa wanaomaliza kifungo kuonyesha kwamba wamerekebishika kitabia, wasiwanyanyapae.

- Kwa ushirikiano wa Kipindi cha Maisha Mseto, Times FM
Akina Mramba na mwenzake mbona walikuwa.wafungwa VIP! au anadhani wote tumesahau.
 
Kuna jamaa moja liliwatangazia askari magereza kwamba wawahenyeshe wafungwa mpaka wajue kwamba hawakwenda gerezani kustarehe!! Nimelisahau hilo jamaa sijui lilikuwa linaitwaje aisee!! Kuna majitu yana roho mbaya kama shetani!! Usoni watu, rohoni shetani!!
 
Askari wa Magereza ni rafiki sana wa wafungwa. Askari Magereza ni tofauti kabisa na Polisi. Askari magereza ni kati ya makundi yanayotambua kwamba maisha hayana mwenyewe na alipo mfungwa basi kesho anaweza akawepo yeye. Tofauti kabisa na Polisi, Polisi wajuacho ni wao ni wao, na wanajua kwamba hakuna meingine zaidi yao.
Anayesababisha magereza/jela iwe na picha iliyojengeka kwa jamii ni wafungwa wenyewe na viherehere manyapala.
Otherwise heshima kwenu askari magereza, naikubali sana kazi yenu ni nzuri kwa kweli.
Ila kabla sijaondoka nina kaswaki ka kizushi. Hivi ni kwa nini ni nadra sana kukosa askari wenu kadhaa wakifuga bata kwenye makambi na kota zenu? Kuna mahusiano gani kati ya bata na Magereza?
Kuna mabaki mengi ya chakula yanayobaki.

Sasa wana take advantage ya kufuga bata, otherwise wangefuga nguruwe ila nadhani suala la imani linakua kikwazo.
 
Waweke miundombinu ya kukutana wenza wao, ila wawashauri kutumia kondomu kuzuia mimba....
Hiyo sio kazi yao, hiyo ni kazi ya serikali ikishirikiana na mahakama, na wakitaka kuweka hilo basi lazima lipitie bungeni na utekelezaji wake utahitaji bajeti kupitishwa na bunge.

Ni suala la serikali kuamua tu.
 
maafsa wa jeshi la magereza wengi wamejizira unakuta mkuu wa magereza anazurul mjini akijichokonoa kijiti kwenye meno huku katumia uniform mbovu zilizopauka tofauti na hawa wenzetu wapigana vita naskia kutoka kwake mpaka apate kibari
 
Zile uniforms zao zina rangi mbaya na zinapauka tofauti na uniforms za wengine kama polisi,sasa tunawaona wamepauka sana kumbe nguo zao wanapata vitambaa visivyo na ubora kivile hasa vinavyonunuliwa na serikali yetu
 
Kuna jamaa moja liliwatangazia askari magereza kwamba wawahenyeshe wafungwa mpaka wajue kwamba hawakwenda gerezani kustarehe!! Nimelisahau hilo jamaa sijui lilikuwa linaitwaje aisee!! Kuna majitu yana roho mbaya kama shetani!! Usoni watu, rohoni shetani!!
Mtangazaji angekumbuka angeuliza kama lile agizo linatekelezwa.
 
These officers wanaongea just kupendezesha listeners, jela za Tanzania ni more than hell. Kuna unyama na uchafu wa kila aina, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, mateso ya hali ya juu.
 
These officers wanaongea just kupendezesha listeners, jela za Tanzania ni more than hell. Kuna unyama na uchafu wa kila aina, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, mateso ya hali ya juu.
Maisha ya jela yanapaswa kua tofauti na uraiani, na maisha ya jela yanatokana na hali halisi ya uchumi wa nchi ndio maana jela ya USA ni tofauti na jela ya Tanzania kwakua hata uchumi hatulingani

Maana yake endapo maisha ya jela (Tz) yatakua mazuri kama maisha ya jela (USA) ni kwamba hayo maisha yatakua mazuri kuliko maisha ya uraiani (TZ) jambo litakalopelekea watu kutamani kuishi jela kuliko uraiani. Mwisho wa siku serikali italazimika kuingia gharama kubwa kuwahudumia wafungwa kuliko raia wasio na makosa.

Kingine nchi zetu bado ziko tabaka la chini kiuchumi, ni kawaida sana kwa nchi kama yetu leaders kua corrupt na watu hufungwa kwakua kesi zinatengenezwa watu wapate pesa, na wanaofungwa ni maskini ambao hata faini hawawezi kujilipia. Hii inapelekea msongamano mkubwa magerezani.

Pia wananchi wana hali ngumu kuanzia elimu,uelewa mpaka maisha, wanajikuta wanaingia kesi za kijinga kama kuiba kuku na vitu vya kijinga, matokeo yake wanaishia jela.

Ntarudi baadae mkuu
 
Askari wa Magereza ni rafiki sana wa wafungwa. Askari Magereza ni tofauti kabisa na Polisi. Askari magereza ni kati ya makundi yanayotambua kwamba maisha hayana mwenyewe na alipo mfungwa basi kesho anaweza akawepo yeye. Tofauti kabisa na Polisi, Polisi wajuacho ni wao ni wao, na wanajua kwamba hakuna meingine zaidi yao.
Anayesababisha magereza/jela iwe na picha iliyojengeka kwa jamii ni wafungwa wenyewe na viherehere manyapala.
Otherwise heshima kwenu askari magereza, naikubali sana kazi yenu ni nzuri kwa kweli.
Ila kabla sijaondoka nina kaswaki ka kizushi. Hivi ni kwa nini ni nadra sana kukosa askari wenu kadhaa wakifuga bata kwenye makambi na kota zenu? Kuna mahusiano gani kati ya bata na Magereza?
Umewahi kufungwa au unapopoma tu?
 
Hbr zenu wana jamvi!.

Nianze hivi.. jana mara baada ya kutangazwa hukumu ya yule Miss Elizabeth ya miaka 2 ambayo ni sawa na siku 720 net (usiku na mchana, Kiangazi na masika net)..

Kuna hoja moja imeibuka ya kuwa ktk utaratibu wa Kimagereza huwa wanahesabu usiku na mchana tofauti... yani usiku ni siku nyingine na mchana ni siku nyingine... ina mana siku 720 zitakuwa sawa na 360?

Kwakuwa hili jamvi ambalo ni jungu kuu ambalo linawatu wa rika zote, watu wa aina zote,, nikaona nije niwaulize wafungwa wa JF ambao walishamaliza vifungo je pana ukweli wowote kwenye hili???

Lakini pia askari magereza waliopo humu watuambie pia!.....

Kuuliza si ujinga....
 
Back
Top Bottom