Magenge hatari ya uhalifu duniani

vivaforever

Senior Member
May 30, 2016
113
162
Hakuna kifaa kinachoweza kupima unyama wa Binadamu isipokuwa tuu kwa kuwalinganisha matendo yao wenyewe kwa wenyewe.

NOTE: Nitayaelezea machache tuu kuhusu haya makundi ya Uhalifu ingawa kuna mengi ya kuelezea. Unaweza kuongeza info nyinginezo unazozijua juu ya hawa watu ili tupate kujifunza zaidi.
Welcome.

1. Mara Salvatrucha (MS-13)
Hakuna mpaka maalumu wa kufanya jambo kwa hawa jamaa ambao makao yao ni pale Los Angeles, California. Wanachama walioanzisha hili genge walikuwa ni wakimbizi kutoka nchini Salvador.

Hili genge lina wastani wa wanachama 70,000 Dunia nzima huku 8,000 hadi 10,000 wakiwa America pekee. Lina wahalifu ikiwemo wauaji wakatili ambao wapo tayari kuua si watoto wala wanawake. Wanahusishwa sana na mauaji ya kukodishwa (contract killings) na wanahusika na biashara ya Bangi America ya kaskazini na ya kati yote.

Washirika wake:
 •Los Zetas. •Sinaloa Cartel. •Jalisco New Generation Cartel. •Gulf Cartel. •Mexican Mafia. •Sureños.

Mahasimu wake:
 •18th Street Gang,  •Latin Kings, •Bloods. •Norteños.

Shughuli zao za uhalifu;
Usafirishaji haramu (Madawa ya kulevya, siraha haramu, watu), mauaji, utakatishaji pesa, utesaji, utekaji, uporaji, uhamiaji haramu, ukahaba n.k

Hebu tujikumbushe matukio machache ya uhalifu ya kukumbukwa yaliyofanywaga na hawa jamaa;

● Tarehe 13/7/2003, Brenda Paz, binti wa miaka 17 ambaye hapo hawali alikuwa mwanachama wa hili kundi la MS-13 aligeuka mvujisha siri., siku kadhaa alikutwa akiwa amefariki kwa kuchomwa kisu huku mwili wake ukiwa umetupwa pembezoni mwa mto Shenandoah huko Virginia. Aliuwawa baada ya kutoa taarifa kwa F.B.I juu ya shughuli za kihalifu za hili kundi. Rafiki zake wawili hapo baadae wakaja kutiwa hatiani kwa mauaji hayo.

● Tarehe 23/12/2004, hii ndio siku ambayo moja ya matukio mabaya zaidi kufanywa na hili kundi yalifanyika. Tukio hili lilitokea hiko Chamelecón, Nchini Honduras, ambapo basi likiwa limesheheni abiria lilisimamishwa na kumininiwa risasi mfululizo huku wakiuwawa abiria 28 na kujeruhiwa 14 wengi wao wakiwa ni Watoto na Wanawake. Chanzo cha yote haya ni Serikali ya Honduras kutangaza kuwa wamerejesha adhabu ya kifo.

2. Cosa Nostra (MAFIOSO)
Cosa Nostra ni msemo wa ki-Italiano unaomaanisha "Kitu chetu" au ("our thing" in English). Genge hili limejikita kwenye kisiwa cha Sicili huko Italia, mizizi yake imeanzia siku za mwanzoni huko New York City pande za mashariki ya chini mwa jiji hilo. Wanachama wake wanajiita "watu wa heshima" ingawa jamii iliyowazunguka haiwatafsiri hivyo. Inadaiwa kuwa wana wanachama kama 25,000 hivi huku wakiwa na washirika karibia 250,000 Dunia nzima.

Hawa jamaa shughuli zao kuu ni kulinda zile biashara halali ambazo mizizi yake ni haramu (Mf: Kufungua Hotel kwa mtaji wa pesa ya Madawa ya kulevya), kuanzisha migogoro, kusimamia makubaliano haramu pamoja na pesa haramu. Ili kulielewa Vibe la hawa jamaa, tazama series ya “The Godfather”.

Washirika wao;
Camorra, 'Ndrangheta, Sacra Corona Unita, American Mafia, Società foggiana.

Mahasimu wao;
Stidda.

Amri kumi za Mafioso.
Mwezi wa 11 mwaka 2007, polisi kutoka jimbo la Sicilly walitaarifu juu ya kupatikana kwa orodha ya amri kumi katika maficho ya Bosi wa hawa mafia (Salvatore Lo Piccolo,). Amri hizo zinasema.

01. Hakuna anayeweza kujiwakilisha moja kwa moja kwa marafiki zetu wengine, lazima awepo mtu wa tatu atakeweza kufanya hivyo. (No one can present himself directly to another of our friends. There must be a third person to do it.).

02. Usiwatamani wake wa rafiki zako. (Never look at the wives of friends'

03. Kamwe usipatikane ukiwa na Askali. (Never be seen with cops).

04. Usiende kwenye kumbi za Starehe na vilabu vya Pombe. (Don't go to pubs and clubs).

05. Mda wote ni jukumu lako kupatikana pale Cosa Nostra inapokuhitaji - hata kama mkeo anakaribia kujifungua. (Always being available for Cosa Nostra is a duty - even if your wife is about to give birth.

06. Vikao lazima viheshimiwe. (Appointments must absolutely be respected).

07. Wake lazima waheshimiwe (Wives must be treated with respect).

08. Pale unapoombwa taarifa, jibu lazima liwe la ukweli. (When asked for any information, the answer must be the truth).

09. Money cannot be appropriated if it belongs to others or to other families.

10. Watu ambao hawawezi jiunga na hili kundi ni wale ambao wana ndugu polisi, wenye sifa mbaya na hawana nidhamu. (People who can't be part of Cosa Nostra: anyone who has a close relative in the police, anyone with a two-timing relative in the family, anyone who behaves badly and doesn't hold to moral values.

3. Sinaloa Cartel

Genge maarufu zaidi la wauza unga (sio Sembe wala Ngano... ni Coccaine) huko Mexico ambalo ni hatari kama lilivyo. Ni maarufu sana kwa kufanya mauaji mbele ya Camera baada ya hapo wanatupia mtandaoni watu wajionee. Kiongozi wao mkuu ni Joaquin Guzman Loera (maharufu kama EL-CHAPO) alishawahi wekwa kwenye jarida la Forbes katika orodha ya watu wenye nguvu zaidi Duniani. Alikuwa na nguvu kiasi kwamba aliwahi toroka gereza lenye ulinzi mkali Duniani mara mbili.

Ingawa hivi sasa yupo gerezani lakini bado genge lake linafanya kazi kama kawaida huku likiendeleza unyang'anyi wa kutumia siraha, utekaji, usafirishaji haramu wa watu, mauaji na uhalifu mwingineo wa kifedha.

Kundi lilianzishwa mwaka 1987; miaka 34 iliyopita.

Waaasisi wake ni Joaquín Guzmán Loera, Héctor Palma Salazar, Ismael Zambada García, Juan José Esparragoza Moreno

Lilianzishwa huko Culiacán, Sinaloa, México.

Mipaka yake sasa;
Mexico:
Sinaloa, Baja California, Baja California Sur,Durango, Sonora,Chihuahua, Coahuila,Edomex, Mexico City, Jalisco, Guadalajara, Nayarit, Tepic, Toluca,Zacatecas, Colima,Aguascalientes, Querétaro.
Ibero-Amerika:
Colombia, Peru,Ecuador, Belize,Guatemala, Honduras,Guyana, Venezuela,Brazil, Argentina.

Maeneo mengineyo;
Europe, Asia, magharibi ya Africa, Australia, New Zealand.

Ndani ya Marekani:
California, Arizona,Utah, Texas, Colorado,Ohio, Minnesota,Michigan, Illinois, New York City,Washington.

Washirika wake;
Los Ántrax, Grupo Flechas, Los Cabrera, Los Rusos, Los Chapitos, Artistas Asesinos, Los Mexicles, Los Salazares, La Barredora, Los Rastrojos, Cachiros, Clan del Golfo, National Liberation Army, Herrera Organization, Fernando Pinea-Jimenez Organization,
Sonora Cartel, Colima Cartel, Gente Nueva, Cártel del Noreste, Cárteles Unidos, La Familia Michoacana, Federal government of Mexico, Independent Soldiers, Cartel of the Suns, Norte del Valle Cartel, Knights Templar Cartel, Milenio Cartel, Los Dámasos, Independent Cartel of Nuevo León, Mexican Mafia Moroccan mafia, Irish mob, Hells Angels, Russian mafia, 'Ndrangheta, Los Oaxacos, La Mano con Ojos.

Mahasimu;

Jalisco New Generation Cartel,
Los Zetas, Gulf Cartel (tangu 2021), Caborca Cartel,
La Barredora 24/7, La Línea, Independent Cartel of Acapulco, Juárez Cartel, Los Negros, Los Mazatlecos, Tijuana Cartel, Logan Heights Gang, Barrio Azteca,
Beltrán-Leyva Cartel.

Taarifa kutoka idara ya kudhibiti madawa ya kulevya Marekani National Drug Intelligence Center.., ndani ya Marekani pekee, Sinaloa Cartel inahusika na kuingiza na kuuza cocaine, heroin, methamphetamine, bangi na MDMA.

4. Bloods & Crips
Magenge mawili yenye wanachama wenye asili ya Africa - America, ukilitaja kundi moja lazima jingine ulitaje na ni adimu kuona linatajwa moja bila ya jingine. Kuna mengi sana ya kuongelea juu ya haya makundi hasimu ambayo yanadhibiti maeneo ya Los Angeles huko jimbo la California.

Ni iko hivi, kundi la Bloods liliundwa kupambana na maovu ya kundi la Crisps kunako mwaka 1972. Bloods husimama kama "Brotherly Love Overrides Oppression and Destruction" (yaani "Upendo wa Ujamaa Unaushinda Uonevu na Uharibifu" sijui kama nipo sawa hapo..!!?) wakati Crips ikiwa inamaanisha "Community Revolution In Progress." (yaani "Mapinduzi ya Jumuiya Yaendelee").

Haya magenge yana vikundi vidogo ndani yake (sets) huku kila kimoja kikiwa na kiongozi na sheria zake na kinafanya kazi kwa kujitegemea. Wanachama wa genge la Bloods huvaa nguo zenye rangi nyekundu na hivi karibuni wamekuwa wakorofi wakizidisha jitihada za kuwashinda Crips.

5. Los Zetas
Los Zetas ("The Zs") ni genge la uhalifu huko Mexico ambalo linachukuliwa kama moja kati ya magenge hatari zaidi ya uhalifu na biashara ya dawa za kulevya huko Mexico. Wanajulikana sana kwa kujihusisha na mauaji ya halaiki kama vile kuchinja watu, mateso ya kifo n.k

Huchukuliwa kama mpinzani mkuu wa Cosa Nostra. Wana miliki sehemu kubwa ya biashara ya dawa za kulevya ndani ya sio tuu Mexico bali pia na maeneo mengi makuu ya Marekani. Wanahusika na mauaji ya halaiki pamoja na uharibifu mkubwa ili tuu wafanye biashara yao istawi. Ni moja kati ya genge ambalo kwa kipindi flani lilikuwa linafanya mauaji ya kikatili zaidi kiasi hata magenge hasimu yalikuwa yanawaogopa.

Moja kati ya matukio yao ya kukumbukwa ni lile la 2011 huko San Fernando (Mexico) ambapo walifanya mauaji ya watu wapatao 193. Uchunguzi ulibaini kuwa Wanawake walibakwa kabla ya kuuliwa huku mateka Wanaume wakipambanishwa wenyewe kwa wenyewe Bloodspot kama njia ya ku-survive (Last Man Standing).

Washirika wake:
Tijuana Cartel, Juárez Cartel, 'Ndrangheta, Los Mazatlecos, Barrio Azteca, MS-13, Texas Syndicate, Gangster Disciples, Triad, The Office of Envigado, La Linea, Hezbollah, Sicilian Mafia, Camorra, Cartel of the Suns.

Mahasimu wake;
Sinaloa Cartel, Knights Templar Cartel, Jalisco New Generation Cartel, Gulf Cartel, Los Zetas Group Bravo (Grupo Bravo), Old School Zetas (Zetas Vieja Escuela).

Ilifikiaga hatua flani ndio walikuwa kundi lenye kutanuka kwa haraka sana huko Mexico wakichukua mipaka mbalimbali kushinda mahasimu wao (Sinaloa Cartel). Lakini hivi karibuni hili kundi limevunjima huku kukiwa na vikundi vidogo mbalimbali, pia ushawishi wake umepungua. Tarehe 30/03/2016, vikundi vidogo vilivyokuwepo ndani ya hili kundi Grupo Bravo (Bravo Group) pamoja na Zetas Vieja Escuela (Old School Zetas) walijitoa na kuunda ushirika na kundi la Gulf Cartel dhidi ya kundi la Cartel Del Noreste (Cartel of the Northeast).

Matukio ya kukumbukwa:
Idara mahiri za usalama za ATF, DEA, ICE na FBI, walifanya Operesheni ijulikanayo kama 'Operation Black Jack' ambapo nyumba za siri tatu za hili kundi hukoMexico zilitambuliwa na kuvamiwa na Idara za Usalama za Mexico ( Mexican Federal security forces ) na kuokoa zaidi ya mateka 40, na kukamata idadi kubwa sana ya Siraha ambayo haijawahi kushuhidiwa hapo mwanzo... katika msako huo walikamata siraha zifuatazo:
● Bunduki kubwa aina ya Rifles 540 (ambapo 288 zikiwa ni Assault rifles na baadhi kama 50 hivi zikiwa ni Caliber rifles).
● Mabomu ya kurusha ya mkono 280 (au tuseme mabomu ya viazi)
● 2 M72 LAW anti-tank weapons,
● Mikanda ya risasi pamoja na mangazini ipatayo 500,000.
● Makoti ya kubebea mabomu 67.
● Makombora ya kutungulia ndege 3.
● Baruti aina ya Dynamite 14.

6. 18th Street Gang ( Genge la uhalifu la mtaa wa 18)
18th Street, wanajulikana pia kama Calle 18, Barrio 18, Mara 18 au kiufupi La 18 huko Amerika ya kati, ni kundi lenye wanachama wa asili mchanganyiko (wengi wao ni wa-Amerika ya kati na wa-Mexico). Hawa jamaa walianza kama genge la uhalifu la mtaani huko Los Angeles na sasa wana wanachama wapatao 30,000 hadi 50,000 kuanzia Mexico, Marekani hadi Amerika ya kati. Pia hawa jamaa wana ufungamano na kundi la Mafia la Mexico (Mexican Mafia).

"Vita iliyopo kati ya hawa watu (18th Street Gang VS Mara Salvatrucha 13) imeligeuza eneo la Amerika ya kati na maeneo ya pembetatu ya kaskazini kuwa ni maeneo mauaji mengi ya kuvamiana Duniani."
- Idara ya Haki (Marekani).

Shughuli zao:
Usafirishaji dawa za kulevya, Mashambulizi ya kudhuru, Mashambulizi ya Moto (Arson), Uporaji, Utekaji, Usafirishaji haramu wa Watu, Wizi, Mauaji, Kufoji vitu, Utakatishaji pesa n.k

Magenge waliyofungamana nayo;
Mafia wa Mexico, Triads, magenge ya uhalifu ya Sureños, Logan Heights.

Magenge hasimu;
Avenues, MS-13, Playboys, Santa Monica, Temple Street, Vineland Boys, Florencia, Bloods & Crips.

Imerekodiwa kuwa kwa wastani wa kila siku lazima mtu ashambuliwe au aibiwe na hawa jamaa. Wana rekodi ya kuua karibia mara tatu zaidi ya kundi lolote lile pinzani la kihalifu.

Mfano;
Mwaka 1998, Catarino Gonzalez alifungwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga risasi nyuma ya kichwa na kumuua hapohapo Officer Filbert Cuesta wakati akiwa amekaa doria ndani ya gari ya Polisi.

Mwaka 2019, mwanachama wa 18th Street alipigwa risasi na kufa hapohapo na mwanachama wa kundi hasimu la Mara Salvatrucha ( MS-13 ) huko Queens subway station.

Huko jiji la Guatemala nako, madereva wengi wa Mabasi wameuliwa na wanachama wa hili kundi baada ya kuingia ndani ya mipaka inayodhibitiwa na hili kundi.

7. Mungiki
Ni kundi ambalo limejikita pale Kenya hasa maeneo ya majiji makubwa mbalimbali wakiwa wanaendesha shughuli za ulinzi wa kulipwa na biashara ndogondogo.

Baada ya kuwa kundi la jadi linalojiendesha lililopigwa marufuku, Mungiki wakaamua kubadirika na kuwa kundi hatari la uhalifu pale Kenya. Wameitesa Kenya kutokana na visa vyao vya Utekaji, kukata watu mapanga, kuchoma watu na mikuki, mishale, kushambulia kwa kutumia moto pamoja na Sumu.

Kutokana na kuwa na mienendo ya kishirikina, serikali ya Kenya imeshindwa kuweka rekodi za mienendo ya hili kundi, hapo mwanzoni wanachama wake walikuwa wanafanya matambiko ya kuoga Damu. Miaka michache nyuma shughuli zao za kihalifu zilihusisha mauaji ya kuchinja watu na kuwakeketa wanawake kinguvu.

Wanapinga aina yoyote ile ya Umagharibi (Westernisation) na vitu vyote vile wanavyoamini kuwa vinachochea Ukoloni, ikiwepo imani ya Ukristo. Falsafa ya hili kundi ni ya kimapinduzi na imejikita kwenye misingi ya jadi ya Kikuyu na hawakubaliani kabisa na wazo la kuifanya Kenya kuwa ya kisasa (Kenyan modernisation) wakiamini kuwa ni uharibifu wa utamaduni.

Wamejipatia umaharufu kutokana na kuwapa upinzani Serikali huku wakijiunga wa makundi yeyote yanayopingana na Serikali.

8. United Bamboo
United Bamboo (au waite "Zhu Lien Bang") ni genge la uhalifu huko Taiwan ambalo lina mfungamano na makundi machache makubwa, na hatari ya kihalifu ulimwenguni. Huu uhusiano umewafanya bado wawe na sehemu katika soko haramu Duniani ambapo wanafanya biashara zao haramu. Wanahusika na mauaji ya muandishi wa habari akiwa ndani ya gereji yake.

Kundi hili pia linajulikana kama Bamboo Union liliundwa miaka ya 1950 huku waasisi wake wakiwa ni Wachina wazawa waliojulikana kama Waishengren hawa walikuwa ni watoto ambao walikuwa wanataka kujilinda dhidi ya vitisho vya watoto wa jamii ya Hoklo. Wanachama wa kwanza kabisa wa hili kundi waliishi katika eneo la barabara ya msitu wa mianzi (Bamboo Forest Road) katika jiji la Jung Ho... kaunti ya Taipei, sasa panajulikana kama Manispaa ya Yonghe ya jiji la Taipei jipya.

Mwaka 1980, watoto wa kike na Mama yao wa moja kati ya wanachama wa Upinzani (Lin Yi-hsiung) walikutaa wakiwa wameuwawa kinyama nyumbani kwao huku wahusika wakiwa ndio haohao United Bamboo.

9. 14k Triad (十四K)
Ni kundi lililojikita huko Hong Kong lakini lanafanya shughuli zake Dunia nzima. Ni kundi la utatu la pili kwa ukubwa nyuma ya kundi la Sun Yee On ambao ndio mahasimu wao wakuu. Kundi hili lina wanachama wapatao 20,000 ambao wamegawanyika kwenye vikundi vidogo mbalimbali.

Shughuli zake kuu nj linajihusisha na usafirishaji wa Dawa haramu za kulevya (Heroin & Opium) kutoka China au Kusini - Mashariki ya Asia. Mbali ma dawa za kulevya kuwa biashara yao kuu, pia wanajihusisha na Usafirishaji haramu wa watu (human trafficking), kamari haramu, kutengeneza pesa harafu, kusafirisha siraha, ukahaba, utekaji, uporaji, mauaji na mikopo haramu yenye riba kubwa. Hili kundi lina wanachama karibia 20,000 Dunia nzima.

10. Aryan Brotherhood
The Aryan Brotherhood, pia wanajulikana kama AB, ni kundi lenye falsafa za Ki-NAZI ambalo shughuli zake huwa zimejikita sana magerezani huko Marekani, inaaminika kuwa lina wanachama 15,000 hadi 20,000 ndani na nje ya Magereza. Ni moja kati ya makundi ya zamani sana pia ya kibaguzi, kulingana na taarifa za F.B.I inaaminika kuwa hawa jamaa wanaunda sehemu ndugo tuu ya idadi ya wafungwa wa magerezani huko Marekani lakini wanahusika kwa kesi nyingi za mauaji yanayotokea magerezani.

Ni genge ambalo lina watu waliojaa hasira tupu na wanajulikana sana kwa mtindo wao wa kuwasababishia wahanga vifo vyenye maumivu sana. Kati ya 1/4 ya vifo vyote kwenye magereza huko Marekani hawa jamaa wanahusika. Hili kundi liliundwa mwaka 1964 katika gereza la San Quentin karibu na San Francisco. Tangu mwaka 1964 wamejipatia jina la kipekee kama kundi lenye vurugu sana.

Shughuli zao ni Mauaji, Mashambulizi, Uuzaji na usafirishaji madawa ya kulevya, Uporaji, Kamari, Usafirishaji salaha haramu, Umalaya wa magerezani, Biashara haramu ya watu n.k.

Wanachama wao wote ni Weupe (kama nilivyosema hapo juu kuwa ni kundi la kibaguzi) na either wawe wamefungwa gerezani au wana historia ya kufungwa gerezani. Kujiunga na hili kundi ni ngumu sana, mwanachama mpya huwa chini ya uangalizi maalumu kwa muda wa si chini ya mwaka mmoja na lazima atoe kiapo cha Damu (Mfano: Kumuua mwanachama wa kundi hasimu, kumuua Askari, mtu mweusi au yeyote asiye na asili ya weupe).

K A R I B U N I

Jisikie huru kuongeza taarifa zilizokosekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi bomba sana
 
Mwenye majibu naomba anisaidie..

Kwanini Amerika ina makundi mengi yanayoendesha shughuli za kihalifu?
Wahamiaji wengi toka ulaya karne ya 17 ,18,19 na 20 walikuwa waharifu walikimbia mkono wa sheria na kwenda America, kufika uko wakaendeleza uharifu wao kwa kuwauwa wahindi wekundu mamilioni kwa mamilioni, wahindi wekundu wakakimbilia kwenye Misitu ya Amazonian, wagiriki walienda sana Brazil, spania walienda sana South America, Colombia, Guatemala, Peru, borivia, etc. Walivyofika uko wakaendeleza uharifu wao mpaka leo, kwa hiyo kizazi kinarithi toka kizazi kingine.
 
Nahisi nimekupata vema mkuu
 
Back
Top Bottom