Magazeti yana nini na Mh. Dr. Emanuel Nchimbi?

Hii sio hoja tena alishathibitisha kuwa ana Phd na ilisaishiwa external supervisor UDSM. Wewe umetoka usingizini

Mkuu Fisadi Mtoto,
Hoja ya Msemakweli haikuwa kwamba 'thesis' yake haijasainiwa na external supervisor. Kasome vizuri kitabu cha Msemakweli ndo tuendelee kujadiliana.

 
alinikela tu pale alivyosema lazima gesi ya mtwara hije dar kwa dharau kweliii...


Ni "Alinikera" badala ya "Alinikela".

Kama umeshindwa kutofautisha matumizi ya "l" na "r". Ni vigumu kuilewa hotuba ya Nchimbi.
 
Hoja yangu ni kwamba jana Nchimbi alijitahidi sana na alijitahidi kuacha ushabiki na kuepuka lugha (matusi) ya chama chao.
Jamani hata PhD yake alimuonesha Prof. Mpangala kuwa alikuwa external supervisor wake. Sidhani kama Prof. Mpangala anaweza kujidhalilisha kiasi cha kushiriki kupika PhD.
 
Binafsi nilimuona amejielimisha sana kwa siku za hivi karibuni na jana alidhihirisha hivyo.....ila aliniacha na maswali yasiyo na majibu kwa mfano wake wa mtoto wa mfalme aliyekuwa akipigwa na wenzie jeshini....

1. Je, alijitabiria kuwa yeye atakuwa nani hapo siku za usoni baada ya "kupigwa" hoja za msingi ile jana? au

2. Je, ameshaona utawala kama vile unaenda upinzani ndiyo maana wanawapiga sana wapinzani (rejea kauli ya Mh. Pinda) ili hapo baadaye upinzani ukiingia madarakani wabaki na kumbukumbu kuwa waliwahi kuwa kuwapiga vipigo vitakatifu?
 
Inatakiwa ujiulize Mwangosi aliuliwa na nani na je yeye kama Waziri mwenye dhamana alichukua hatua gani? kwa hiyo vyombo vya habari bado vina kumbukumbu ya tukio hilo.

Kaka aliyesimamia mauaji si amepanda cheo? Aliyempandisha cheo msimamizi wa mauaji ya mwangosi ndoo wa kulaumiwa
 
Hoja yangu ni kwamba jana Nchimbi alijitahidi sana na alijitahidi kuacha ushabiki na kuepuka lugha (matusi) ya chama chao.
Jamani hata PhD yake alimuonesha Prof. Mpangala kuwa alikuwa external supervisor wake. Sidhani kama Prof. Mpangala anaweza kujidhalilisha kiasi cha kushiriki kupika PhD.

Rejea post yangu namba 21
 
Nchimbi alijitahidi sana kujibu hoja kwa majibu ya jumla, hakuwa muwazi sana. Kwa mfano kitendo cha kukiri udhaifu na kusema tutajitahidi kama serikali ni kauli za jumla, haijafafanua hatua gani anatakiwa kuchukua yeye kama waziri wa polisi.

Pia Nchimbi aliharibu pale aliposema gesi lazima iende dar, ikiwezekana hata kwa mtutu wa bunduki (hii ndiyo tafsiri sahihi). Ndugu zangu hapa ieleweke kuwa watu wa mtwara hawajazuia gesi kwenda dar, bali wanataka washirikishwe, pia serikali iwaeleze wanafaidikaje na gesi

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Alijitahidi lakn hakuna haja sana ya kumwandika huyu jamaa mzee wa marathon na udaktari kabla ya thesis

Hayo uliyotaka yaandikwe wewe yameandikwa? Nafikiri kuna mahali hujamwelewa mtoa mada rudia kusoma vizuri kuhusu watu wanaobambikiwa kesi
 
Mdahalo sijauona lakini nasikia Slaa alinywea na ujuwaji ulizimwa ki staili ya pekee na Nchimbi.

Kudos Nchimbi.

Mwenye link ya mdahalo kama imerushwa youtube atuwekee.
 
Ni kweli alijitahidi,lakini ripoti la tume iliyoshughulikia kifo cha mwenzao mwangosi hajaifanyia kazi maana kesi yenyewe inaonekana ya magumashi muuaji anafichwa vyombo vya habari visichukuwe picha yake tofauti na watuhumiwa wengine.pia kuna suala la kibanda kutekwa ambalo mpaka leo wizara yake haijafanya lolote la maana kuonyesha uwajibikaji,mwisho kunakauli alitoa bungeni juu ya ripoti ya tume ya mwangosi je mambo haya na mengine mengi ambayo sijaya andika hapa yanaweza kuwafurahisha waandishi wahabari?je wewe ungekuwa mwandishi haya mambo yangekufanya uwe karibu na mh nchimbi ?mi nataka kujua.
 
Hiyo ilikuwa tu anaonyesha 'a change in strategy' Serikalini. Pitia pia kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu Polisi kutotumia nguvu kupita kiasi. Lakini wanaaminika?
 
Tunataka utendaji wenye ufanisi hai unaoonekana, sio kuremba maneno kama mpiga debe wa bodaboda.
 
Kama kuna siku aliongea vema basi ilikuwa ni jana big up Nchimbi

penye ukweli daima tuseme hata kama tu wapinzani wa serikali,kwenye mjadala kweli jamaa alionyesha kama amekomaa kisiasa,nlipenda sana alivyokuwa anajibu hoja na hakika alijiandaa vizuri,big up sana mh.waziri
 
Nchimbi kazi kweli kweli!nasikia amewahi ishi kwenye kambi za polisi zamani.kama hili ni kweli basi polisi ni ndugu zake na hawezi kuwaadhibu.kwenye mjadala alikua ametulia na alijua anafanya nini.safi sana
 
ni "alinikera" badala ya "alinikela".

Kama umeshindwa kutofautisha matumizi ya "l" na "r". Ni vigumu kuilewa hotuba ya nchimbi.

point yake umeipata, usichambue herufi, sometimes we get meaning through a whole sentence and not one word!
 
WanaJF, kwa waliokuwepo ukumbi wa Nkrumah na kwa waliofuatilia mjadala wa jana kupitia ITV, watakubaliana nami kuwa kama kuna siku Nchimbi alionesha ukomavu wa kisiasa basi ni jana. Kwanza walimuwashia moto kama yeye, waliiwashia moto serikali kwa hali ya juu. Lakini alivyoinuka na kuanza kuongea, hakujibu matusi sana sana aliongea kama utani tu kwamba Dr. Slaa ni padri wake na yeye anamheshimu hivyo. Alijitahidi sana kujibu hoja zilizo kwenye uwezo wake na kuacha zile zilizo juu yake kama ya kumpandisha cheo Kamhanda. Hilo ni la JK mwenyewe. Na baadaye akakili ukweli kuwa kuna mazingira watu wanabambikiwa kesi na kutoa mfano. Cha ajabu magazeti ya leo yote hakuna hata moja lilimcover. Kunani kati ya Nchimbi na vyombo vya habari?

Mimi nilitegemea walau gazeti moja liandike waziri akiri serikali kusingizia watu kesi ili uibuke mjadala utakaopelekea kufanyika kwa uchunguzi wa kina juu ya masikini wengi waliojaa magerezani kisa wamebambikiziwa kesi au hawana nguvu ya kisheria lakini wapi bwana. Waandishi hawako huko.

Ikumbukwe pia kuwa baada ya kumaliza kuongea alipigiwa makofi na watu wengi tu.

Binafsi ninampongeza Nchimbi kwanza kwa kuthubutu kwenda mlimani ambako boss wake anakuogopa kama nyoka, na pili kwa kutoa hotuba fupi ya kiutu uzima na kuonesha kuwa yeye ni mtawala.
Natamani ule mjadala wa jana wauone Nape na Nchemba ambao wanadhani kutukana ndiyo siasa. CCM tumeni watu kama Nchimbi kwenye mijadala sio watukanaji.


Ramadhan Kalim
Ni Ramadhan Kareem na si kalim.
Nilimuangalia akijibu hoja lakini binafsi sikuridhika na majibu yake kwani mambo mazito yote aliyakwepa ni kuishia kutoa mifano na vijembe (King George kupigwa na waliompiga kueleza kuwa kuna wakati atakuwa Mfalme na wao watakuwa wanajisifu kuwa waliwahi kumpiga-akaendelea ya kuwa kuna watu watakwenda nyumbani wakiwa na furaha kuwa angalau wamempiga Mfalme mtarajiwa)
Kama sheria inaagiza vifo tataviundie mahakam ya corona shida iko wapi?Anakiri askari kubamabikia watu kesi amechukua hatua gani?
Binafsi sikuridhika na majibu yake.
 
Back
Top Bottom