Magari ya Serikali kuonekana kwenye kumbi za starehe nyakati za Usiku

I am just trying to be realistic!

Hawa viongizi nao wanamaisha kama sisi, wanahitaji kustarehe kama sisi pindi pesa zinapotutembelea. Hivi wewe tukikupa gari utaacha kumpitisha mtoto wako shuleni kabla ya kwenda kazini kisa sio matumizi ya ofisi?

I am principle based and not rule based! Ukiwa mtu wa uhalisia, maisha yako yatakuwa ya heri na unafuu zaidi. Kuna sheria na taratibu nyingi, nyingine hazifuatwi na zimekuwa dormant kwani sio haki na kila mtu analijua.

ulichoandika ni Africa labda na baadhi ya mabara machche duniani
Kitu kikiwa cha Umma basi taratibu na sheria walizojiwekea kwa watumishi wake zitahakikishwa zinafuatwa kivyovyote vile,,,
Ndio maana waadilifu wanaendelea na sisi wenye mawazo ya kufikiria matumbo yetu tuko pale pale
 
ulichoandika ni Africa labda na baadhi ya mabara machche duniani
Kitu kikiwa cha Umma basi taratibu na sheria walizojiwekea kwa watumishi wake zitahakikishwa zinafuatwa kivyovyote vile,,,
Ndio maana waadilifu wanaendelea na sisi wenye mawazo ya kufikiria matumbo yetu tuko pale pale

Toa mfano usitumie dhana ya ujumla. Mambo mengine tunayofikiri kwa mataifa mengine sio kihivyo, hata mimi niliwahi kufikiri Africa ndiko kuna kila lililobaya na kwa wazungu kila kitu perfect nikaja kumeza fikra zangu.

Gari la ofisi wakati mwingine ni motisha kwa utumishi wako mzuri. Gari inabidi likutumikie na sio wewe kuwa mtumishi wa gari. Ndio maana baadhi ya makampuni binafsi ili kuondoa malalamiko kama haya wanaamua kazi zisiwe na magari bali maofisa wanaostahili wanunuliwe magari kabisa, kazi iwe kwao.

Dhana hapa ni reasonability. Hata gari likiwa lako kwenda nalo sehemu ambayo haikubaliki kijamii sio sawa.

Tutabishana lakini ukweli ndio huo. Nina uhakika hata wewe ukiwa kwenye nafasi hiyo sio kwa kila jambo la kibinafsi utaacha gari la ofisi, haiwezekani.

Mimi niko sekta binafsi ninayaona. Tusiwanyooshee vidole tu watu wa serikali kuna mambo hayawezekani. Nimetoa mfano, utaacha kumpitisha mwanao shule wakati unaenda kazini kisa sio matumizi ya ofisi?
 
Sijajua kwanini unakuwa na jazba, sijakataa kwamba labda ile gari ilipaki "bar''. Ili kama tunakubali kuwa GREAT THINKERS basi tukubali kwenda na hoja inayojitosheleza. Kupiga picha plate numbers za gari hakujitoshelezi kuonesha kuwa hilo gari lilikuwa sehemu isiyohusika beyond any reasonable doubt. Kama "ungepiga picha" labda ikionesha vilevile maeneo kama hiyo "bar" wala nisingehoji. But kutuletea habari zisizo na mashiko ni kuliharibu jamvi na kulifanya kuwa kijiwe cha wahuni. Na hili hatuwezi kukubaliana nalo kama wanasiasa wa CCM kupiga makofi tu hata kama hawajaelewa mada!!!!

One more thing, sikatai kuwa mali za waTz zinatumika isivyofaa, ila lazima twende kwa hoja dude. JF should never in anyway be a den of illiterates who keep nodding their heads as a sign of agreeing with whatever is said even if they don't understand the point and they doubt it. Come on!!!!!!!!!!
Kuna watu mna akili za hovyo sana
 
Habari za siku wakuu,

Katika pita pita zangu kwa muda wa miaka karibu 10 sasa kwenye maeneo mbalimbali nchini, nimekuwa nikijiuliza maswali ambayo wakati mwingine nakosa majibu kutokana na unyeti wa masuala hayo, lakini moja ya masuala hayo ni pamoja na muda wa kuegesha magari.

Ni mara nyingi sasa nashuhudia magari ya Serikali yanazagaa mtaani mara baada ya muda wa kazi za kawaida, Sitaki kuamini kwamba serikali haijaweka utaratibu wa kuyadhibiti magari yake kwa muda yanayotakiwa kufanyakazi na muda yanayotakiwa kuegeshwa.

Kipindi cha miaka mingi kidogo iliyopita nakumbuka Serikali ilikuwa imepiga marufuku baada ya muda wa kazi magari yake kutoonekana mitaani.

Hivi sasa mpaka nyakati za usiku hata kwenye kumbi za starehe yanaonekana, sasa sijui madhumuni ya magari haya kuegeshwe kwenye maeneo haya ninini? na hatari iliyopo kwa magari kama haya kuwepo kwenye maeneo haya ni ipi? je gharama za mafuta zinazotumika ambazo naweza kuziita sio za lazima nani anazibeba?

Naomba tulijadili hili kwa pamoja na pengine kama kuna ushauri wa kuipa serikali yetu ni vyema tukafanya hivyo kwasababu najua wengi wetu hapa mnafanyakazi katika maeneo haya/mliwahi kufanyakazi katika maeneo haya ili tujue kuwa anayetakiwa kuwajibika katika suala hili ni Dereva au ni nani?
 
Sio hilo tu. Ukienda ofisi zote za serikali unakuta mabosi wako ndani na viyoyozi na madereva wako kwenye magari nje nao wanakula viyoyozi magari yamesimama yako silence.. Hii inasababishwa maderva kujua siri za mabosi wao na mabosi wanaogopa kuwakemea.
 
Sio hilo tu. Ukienda ofisi zote za serikali unakuta mabosi wako ndani na viyoyozi na madereva wako kwenye magari nje nao wanakula viyoyozi magari yamesimama yako silence.. Hii inasababishwa maderva kujua siri za mabosi wao na mabosi wanaogopa kuwakemea.

Mkuu magari yako chini ya TO so siri za bosi na hayo unayosema yatafutie uhusiano sahihi, .

Kwenye kumbi za starehe sio sawa ila wapo "watu" wanafanya kazi beyond hizo saa zilizopangwa, sio tabia nzuri kama mtu hana sababu ila kuna watu wanalazimika mpaka jumapili kuwapo sehemu za kazi au safarini
 
Ww a/c za magari azili mafuta alafu elewa kuwa mabosi wa sasa wanataka sifa bosi anatoka ofisini saa moja ucku anapelekwa sala sala dereva anakaa mbagara sasa ww unaweza kuona gari ya serikali isionekane saa tatu ucku
 
Rais Kikwete aliongeza kuwa wakati alipoingia madarakani makusanyo ya mapato ya ndani yalikuwa sh.bilioni 170 kwa mwezi sasa yamefikia bilioni 900 hivyo hali hiyo imetokana na jitihada za maboresho mbalimbali.

Serikali ilipokuwa inakusanya sh. bilioni 170 kwa mwezi miaka kumi iliyopita maisha ya Watanzania yalikuwa bora zaidi kuliko makusanyo ya sasa ya sh. bilioni 900 ambazo hazina usimamizi, ndiyo maana magari ya serikali yamekuwa ni magari ya familia kila wiki lina jaziwa mafuta lita 200 gari ofisini halionekani liko nyumbani kwa bosi, liko sokoni, liko mashuleni kuchukua wanafunzi, liko shamba kuchukua mkaa, jioni liko baa bosi akiburudika na lager
 
Ww a/c za magari azili mafuta alafu elewa kuwa mabosi wa sasa wanataka sifa bosi anatoka ofisini saa moja ucku anapelekwa sala sala dereva anakaa mbagara sasa ww unaweza kuona gari ya serikali isionekane saa tatu ucku

Matumizi makubwa ya serikalini ni kuhudumia magari yake. Kumbuka miaka mingi ya nyuma serikali iliwapa watumishi wake unafuu wa kodi ya manunuzi wa magari binafsi, kipindi kile serikali ilinuia kuwa watumishi wote watumie magari yao kwenda ofisini na kurudi nyumbani. Magari yote ya serikali yawe kwenye maegesho ya magari ya wizara/idara, mara tu muda wa kazi unapofika, madereva walitakiwa wafike ofini asubuhi wachukue magari kwa kazi za kiofisi tu. Lakini imekuwa tofauti kipindi hiki ambacho serikali haipo.
 
Wakati mwingine njoo na ushahidi wa namba za gari, mtumiaji wa gari hoteli au bar husika na uulize management ya eneo husika kuwa mwenye gari hili anayo kazi ya kiofisi ya kufanya au ni mgeni toka eneo moja kaja kikazi na hilo gari litalala hapo au ni dereva anazurura tu coz gari ni kwa kazi maalum na hakuna sheria inayozuia mtumiaji wa gari kama yuko nje ya kituo anaruhusa ya kulala maeneo hayo. Ni kwa wale wenye fikra finyu tu anaefikiri kila gari la serikali likipaki mahali ambapo kuna huduma zaidi ya moja kama malazi, chakula, disco na warembo basi gari hilo linafukuzia warembo kabla hata hajafanya utafiti hata kama mahali penyewe pana usalama wa uhakika wa kampuni za ulinzi muda wote.

Mkuu cku ukiwa boss ndo utaona ulichokuwa unaandika ni utumbo coz unachoomba ni zuio la kutumia gari la kazi baada ya saa za kazi umesahau kuna wkt watu hukesha wakifanyakazi ama majadiliano kwa ajili ya ofisi wanazohudumu ili tu wewe unawaza wanastarehe hapo walipo.




habari za siku wakuu,

katika pita pita zangu kwa muda wa miaka karibu 10 sasa kwenye maeneo mbalimbali nchini, nimekuwa nikijiuliza maswali ambayo wakati mwingine nakosa majibu kutokana na unyeti wa masuala hayo, lakini moja ya masuala hayo ni pamoja na muda wa kuegesha magari.

Ni mara nyingi sasa nashuhudia magari ya serikali yanazagaa mtaani mara baada ya muda wa kazi za kawaida, sitaki kuamini kwamba serikali haijaweka utaratibu wa kuyadhibiti magari yake kwa muda yanayotakiwa kufanyakazi na muda yanayotakiwa kuegeshwa.

Kipindi cha miaka mingi kidogo iliyopita nakumbuka serikali ilikuwa imepiga marufuku baada ya muda wa kazi magari yake kutoonekana mitaani.

Hivi sasa mpaka nyakati za usiku hata kwenye kumbi za starehe yanaonekana, sasa sijui madhumuni ya magari haya kuegeshwe kwenye maeneo haya ninini? Na hatari iliyopo kwa magari kama haya kuwepo kwenye maeneo haya ni ipi? Je gharama za mafuta zinazotumika ambazo naweza kuziita sio za lazima nani anazibeba?

Naomba tulijadili hili kwa pamoja na pengine kama kuna ushauri wa kuipa serikali yetu ni vyema tukafanya hivyo kwasababu najua wengi wetu hapa mnafanyakazi katika maeneo haya/mliwahi kufanyakazi katika maeneo haya ili tujue kuwa anayetakiwa kuwajibika katika suala hili ni dereva au ni nani?
 
....issue hapa ni kuhusu mgt ya public resounces so ingekuwa vyema kama wanajamii wangepanua mada hii hivyo,kwa hakika magari za serikali yanatumika isivyo.Kwanini magari ya serikali yasilale katika eneo lake,usiku utakuta yanabadilishwa namba binansi....TZ acha tu.UKAWA wakiingia ninavyowajua,kwanza mtafuta bodaboda zenu.
 
Back
Top Bottom