Magari ya mwendo kasi yameshindwa kazi abiria wanapata tabu

so sad" Hakika ... ndio shida ya kuwa na wateuliwa vichaa", kama baba yao stone cold"...

wabongo tumezoea shida " maisha ya luxury na sisi wapi na wapi that's why tunashindwa kuendesha miradi yote yenye manufaa kwa Taifa hili ... ni sawa sawa na rai aliyezoea Kula mihogo .makande .ugali" siku ukija kumpa piza au mandi ale Lazima ataharisha tu
 
Huu mradi jins unavyoendeshwa ni AIBU.

Rais au Wazr wa TAMISEMI anapaswa awafute kaz viongozi wa DART kwa ujinga wanaofanya na kutesa Wananchi.

Mradi huu phase 1 umetumia mabillion ya kodi zetu

Wanipe Mimi ili kukomesha huu ubabaishaji unaofanywa na UDART
bakhresa Aliutaka Huu Mradi Wakamtosa
Wana Gar 70 Zipo Tpa Wameshindwa Lipia Ushuru
 
Na hapo yalienda mahakamani kupinga wasiletewe upinzani/competition ya aina yoote ile sababu walidai kazi wanaieweza, a ca se of de ja vu?!
 
Hali ya usafirishaji wa abiria kwa kutumia njia maalumu za mwendokasi inazidi kuwa ngumu, hasa kwa abiria wanaotumia usafiri huo kutoka Mbezi ya Kimara kwenda mjini. Mradi wa njia hizi ulikuja kama suluhu ya kutatua kero ya foleni kwa wakazi wa maeneo hayo, huku tukitegemea kwamba baadaye wangetanua huduma hii kwa njia zingine kuu za jiji.

Matarajio ya kutatua changamoto hizi yamefifia baada ya kuona uozo mwingi katika utawala na uongozi wa mabasi haya.
1.Abiria wanasubiri zaidi ya saa nzima vituoni.
2. Magari yanajaza sana abiria kupita uwezo wake.
3. Mifumo ya malipo(kwa kutumia kadi za kielektroniki) umesitishwa ghafla hivyo kila kitu kimerudi analojia.
4. Watu huingia kama ng'ombe kwenye hayo magari.


Sasa kama management ya UDART/DART imeshindwa kujiongoza katika hili, kwa nini serikali isiingile kati?

Kama hili "dogo" tu limetushinda, tutaweza kweli kusimamia "speed train" kweli? Au tutafanyana kafara tu.

Tukubali tukatae watanzania tumefeli katika kusimamia taasisi zetu. Tufanyeje?
 
IMG-20181010-WA0060.jpg
 
Watanzania ustaarabu hatujawahi kuuweza, sisi size yetu ni ileile system ya zamani
 
Mradi huu ni wa wazungu wabongo hatuuwezi , basi linatoka kivukoni mpaka kimara linaacha abiria kivukoni eti linawahi abiria kimara
Leo Asubuhi madereva wa magari ya mwendokasi wamegoma wakidai kuboreshewa maslai yao na walichofanya ni kuweka magari kwe njia ya kutokea hivyo magari mengi yameshindwa kutoka na kutaoa huduma hivyo kusababisha adha kubwa kwa wananchi.

Mradi huu una matatizo mengi sana lakini hadi sasa si waziri mkuu au waziri Jaffo wameweza kutatua hata tatizo moja.

mradi huu una matatizo kati ya UDART na Max com ndio maana tiketi za kielectronic azitolewi kwa sasa na kupelekea wizi mkubwa unao endelea kwenye mradi

Mradi huu una matatizo kati ya DART na UDART ndio maana hadi sasa magari zaidi ya sabini yamekwama bandarini.

Mradi huu una matatizo kati ya wakatisha tiketi na UDART ...

Mradi huu una matatizo mengi sana kuhusu haki za wafanyakazi...

Mradi huu una matatizo ya kuharibiwa kwa miundombinu.

Mh Rais tunaomba uingilie kati kunusuru mradi huu maana wateule wako wameshindwa kabisa
 
Haya mabasi sijui life span yake itakuwa miaka mingapi...
Kupanga foleni ili kila mtu audumiwe kwa muda aliofika ni mtihani mkubwa sana TZ na Afrika kwa ujumla...

Hii picha ina maelezo mengi sana kubwa ni roho ya UMIMI...itatufanya tubaki hivi hivi miaka nenda rudi
 
Back
Top Bottom