Mafuta ubuyu iaminiwe TFDA

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi

SERIKALI imesema Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ndiyo taasisi pekee yenye dhamana ya kutoa taarifa kwa umma juu ya usalama wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba, yakiwamo mafuta yatokanayo na mbegu za ubuyu

Katika taarifa yake kuhusu usalama wa mafuta hayo Serikali inaitaka jamii kujiepusha na matumizi yake kwani yana tindikali za Cyclopropenoic Fatt Acids (CPFA) ambayo si salama kwa matumizi kama chakula au dawa.

Utafiti uliofanywa kwa wanyama duniani unaonesha kuwa matumizi ya mafuta ya ubuyu yana athari za kiafya na kuonesha kupungua kwa ukuaji wa panya kwa asilimia 50 na kwa kuku wa mayai kutaga na athari kwenye figo.

Taarifa hiyo iliyotolewa juzi na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi inatokana na makubaliano ya kikao cha wataalamu wa taasisi za Kitengo cha Tiba Asilia na Mbadala, Idara ya Kinga na Mfamasia Mkuu wa

Wizara,Taasisi ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali,Taasisi ya Tiba Asili Muhimbili, COSTEC, Shirika la Viwango (TBS), Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) na TFDA.

Alisema mafuta hayo yana kiwango kikubwa cha tindikali za mafuta za (CPFA) zinazoweza kusababisha athari za kiafya endapo mafuta hayo yatatumika bila kusafishwa.

"Hakuna viwango vya kitaifa au kimataifa ambavyo mafuta hayo yangetumika kama vigezo vya kuamua usalama na ubora wake kwa matumizi ya binadamu, vile vile hakuna teknolojia nchini inayotumika kusindika mafuta hayo yenye uwezo wa kuondoa tindikali hiyo," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.[/FONT]

Akizungumzia utafiti uliofanywa kwa wanyama, alisema athari nyingine zinazoweza kutokea ni kuathiri vimeng'enyo vinavyosaidia uchakataji wa tindikali za mafuta mwilini na kusababisha ukondefu.[/FONT]

Huku taarifa zaidi za kisayansi zikionesha kuwa matumizi ya kiwango kikubwa cha mafuta hayo pamoja na vyakula vilivyochafuliwa na sumu kuvu aina ya aflatoxin B1 ambayo inazalishwa na ukungu katika baadhi ya vyakula kama mahindi na karanga, huongeza uwezekano wa kupata saratani ya ini.

Hivyo wataalamu hao walikubaliana kuwa mafuta hayo yanaweza kutumika kama malighafi katika viwanda vinavyoweza kuyasafishakama ilivyo sehemu nyingine duniani yenye teknolojia hiyo.

Matumizi ya mafuta ya ubuyu kama tiba yamesababisha mvutano na malumbano baada ya TFDA kutangaza kuwa na athari kwa matumizi ya binadamu.

chanzo. Habari Leo

Tafadhalini Msinywe hayo Mafuta ya Ubuyu muwe munajipakaa mwilini tu.
 
Hii habari nimeisikia jana sana kwenye vyombo vya habari. Nadhani hata kujipakia sasa tutaogopa mkuu.
Kwanza kupaka paka mafuta anasa hapa Dar labda kama upo Dodoma, Mbeya, iringa, Arusha au Kilimanjaro
 
Washamba tu, hao wauzaji wa hayo mafuta wameandika kwenye label za mafuta ya ubuyu kuwa ni mazuri kunywa kumbe TFDA walikuwa hawajaona miaka yote hiyo? wazugaji tu ni sawa wale watu wa wizara na nimr walioenda kwa babu kuchunguza dawa yake wakaanza na kikombe.

Tuwadai TFDA kwa kuacha hii bidhaa iuzwe miaka yote tamko waje walitoe majuzi wangapi wameathirika?

Siwaamini
 
Huyu mwandishi ameshindwa kutu-link na wale waliopinga onyo la TFDA na sababu zao. Mwenye kuwafahamu na sababu zao tafadhali. niliwahi sikia kauli za wagonjwa wa Ocean rd instute for cancer, lakini sijui pia kama lilikua tamko la uongozi.

tragedy of the commons
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom