Mafuriko yafunika tena mji wa Kilosa

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,416
Wakuu Salaam,
Habari za kuaminika ni kuwa mji wa Kilosa tayari umefunikwa na mafuriko kama yale yaliyoukumba mji huo mwaka jana. Imearifiwa kuwa maji hayo tayari yamezingira mji wote na yameshaanza kuingia ndani ya nyumba za watu, na tayari watu wameshaanza kuhama na kurudi kwenye mahema waliyokuwa wakiyatumia wakati wa mafuriko ya mwaka jana.

Mji wa Kilosa na vitongoji vyake ulikumbwa na janga kubwa la mafuriko ambayo yalisababisha vifo vya watu wawili na kuwaacha maelfu ya wananchi bila makazi, kitu kilicholazimu wakazi wa mji huo kuishi kwenye makambi.

Mafuriko hayo yalisababishwa na kingo za mto Mkondoa (mto unaokatiza katikati ya mji huo) kubomoka na hivyo kuruhusu kiwango kikubwa cha maji kuingia kwenye makazi ya watu. Mto huo ulifurika baada ya mvua kubwa kunyesha katika mkoa wa Dodoma hasa wilaya za Kongwa na Mpwapwa ambako ndio chanzo cha mto huo.

Kingo za mto Mkondoa zilibomoka baada ya kuelemewa na maji. Hii imetokana na bwawa la kupunguza kasi ya maji ya mto huo lililopo maeneo ya Kidete (ambalo lilijengwa na wakoloni wa kijerumani) kukosa matengenezo/ukarabati kwa makumi ya miaka na kusababisha bwawa hilo kujaa tope na hivyo kutokuwa na uwezo wa kuhifadhi maji. Kitu kingine ni kukosekana kwa matengenezo ya kingo za mto huo "tuta" ambalo pia liliwekwa na wakoloni wa kijerumani.

Kingo hizo zimekuwa zikibomoka siku hadi siku huku viongozi wa wilaya akiwemo mbunge wa jimbo hilo Mh. Mustafa Mkullo wakikaa bila kuchukua hatua za makusudi za kuzuia maafa hayo.

Baada ya mafuriko ya mwaka jana, viongozi wa wilaya hiyo waliendelea kukaa bila kuchukua hatua stahiki za kuzuia maafa mengine, huku wakiacha maeneo ya kingo za mto zilizobomolewa bila ya kuzifanyia matengenezo hali wakijua kuwa mafuriko yakija hiyo ndiyo itakuwa njia ya maji kupita na kuingia kwenye makazi ya watu. Kwa hiyo mafuriko haya mapya si kwamba yamebomoa tena kingo za mto bali yamepita kwenye kingo zilizobomolewa na mafuriko ya mwaka jana na ambazo ziliachwa na uongozi wa wilaya bila ya kufanyiwa ukarabati, hali wakijua kuwa mto ukijaa ni lazima maji yataingia kwenye makazi ya watu, na kwamba suala la mto kujaa ni lazima hasa katika kipindi cha msimu wa mvua za masika.

Habari zaidi kwa kadri nitakavyozipata.
Wasalaam.
 
na baba yao Qaddafi anasulubiwa kabla hata hajawajengea misikitti aliyowaahidi.

poleni wana-kilosa
 
Inamaana ule ukingo wa ule mto walikuwa hawajaujenga hadi leo? Maana ilibainika chanzo cha yele mafuriko yaliyopita hivyo ilibidi lishughulikiwe kabla msimu mwingine wa mvua kuanza ama kutoa tahadhali za kiusalama kwa wakazi. Ama labda ni chanzo kingine kimeleta mafuriko?
 
Back
Top Bottom