Mafuriko makubwa yatokea wilayani Dumila,barabara ya Morogoro-Dodoma yafungwa

dionsio

Senior Member
Oct 11, 2013
169
29
Kumetokea mafuriko makubwa huko Dumila na kusababisha kutopitika kwa barabara ya Morogoro-Dodoma. Mpaka sasa watu ni wengi na magari pia. Mkuu wa mkoa anaelekea eneo la tukio.

SOURCE: RADIO ONE

===== Updates ======
Serikali imefunga barabara ya Moro-Dom kwa muda usiojulikana kufuatia kubomoka daraja la Dumila, yashauri wasafiri kutafuta njia nyingine.

Source: Mwananchi breaking news

View attachment 133730
 
dah bahati mbaya ni radio, tungepata picha ingekuwa bomba. najisemea tu jamani.
 
Mleta mada km ana haraka vile?? MAFURIKO mvua imenyesha kwa masaa mangapi? km imeanza usiku mpaka muda huu au imeanza alfajiri? NATUMAI HIYO SOURCE ALIYOISEMA IMEELEZA HAYO NINAYO ULIZA! RUDI ULEKEBISHE ULICHOPOST!
 
Malizia,DARAJA LINALO CONNNECT DUMILA NA MOROGORO CHALI!wa DODOMA huko huko na wa MORO huko huko.
 
Kumetokea mafuriko makubwa huko Dumila na kusababisha kutopitika kwa barabara ya Morogoro-Dodoma. Mpaka sasa watu ni wengi na magari pia. Mkuu wa mkoa anaelekea eneo la tukio.

SOURCE: RADIO ONE

"Topic: Mafuriko makubwa yatokea wilayani Dumila"

Si kweli kuwa Dumila ni Wilaya, Dumila ipo ndani ya Wilaya ya Kilosa http://www.minube.net/map/tanzania/morogoro/dumila

Hapa unatakiwa kurekebisha
 
dumila.jpg Pic credit: UMOJA VILLAGE
 
Want jamii mliopo eneo la tukio. Sisi tumekwama hapa Morogoro tunaomba update ya half ya barabara.
 
Habari mbaya kwa wasafiri wote wategemeao barabara kuu ya kati...
 
Mabasi yote yaliyokua yanatokea dar yameamriwa kurudi morogoro hakuna dalili za safari kwa leo
 
Nimesikia kuwa daraja la pale Dumila, barabara kuu ya Morogoro - Dodoma limesombwa na maji na kuadhiri usafiri wa barabara. Ninaomba mwenye taarifa kamili na sahihi atujuze zaidi.
 
Back
Top Bottom