Mafuriko Dar: Ujumbe kwa Nehemia Mchechu na Prof. Tibaijuka

KISUKALI

Member
Feb 28, 2010
70
8
Wadau,
Nianze kwa kutoa Pole kwa wenzetu wote waliofikwa na Maafa, pia niwapongeze waliosaidia juhudi za Uokoaji na wanaoendelea kuwasaidia na kuwafariji Wahanga wa Janga hili.
Kisha niwapongeze Watanzania kwa juhudi zao za kupenda kujijengea Nyumba zao bila kusubiri kufanyiwa hivyo.
Sasa niulize swali, hili SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) Liko wapi? Hivi liliundwa Kwa Madhumuni gani? Je linastahili lawama wakati wa matukio kama haya?
Naomba tujadili.
 
hili lipo kwa sasa kwa wale wenye mpunga tu kama huna mkwanja itakuwa kwako..

na hao walikufa kwenye mafuriko ni kutoka na uziba njia za maji na jingine ni umasikini hawana hela za kupanda dala dala ndio maana waka jenga hapo jangwani sababu ni karibu na mjini..
 
Wadau,
Nianze kwa kutoa Pole kwa wenzetu wote waliofikwa na Maafa, pia niwapongeze waliosaidia juhudi za Uokoaji na wanaoendelea kuwasaidia na kuwafariji Wahanga wa Janga hili.
Kisha niwapongeze Watanzania kwa juhudi zao za kupenda kujijengea Nyumba zao bila kusubiri kufanyiwa hivyo.
Sasa niulize swali, hili SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) Liko wapi? Hivi liliundwa Kwa Madhumuni gani? Je linastahili lawama wakati wa matukio kama haya?
Naomba tujadili.
They need to reform their Vision and Mission.
 
mkuu unataka waathirika wa mafuriko wapelekwe meru residential apartments?
lakini kwa upande mwingine acha hawa wananchi wakome kwa sababu wamezoea kudanganywa na ubwabwa mweusi na maji ya azam,vitumbo vikijaa wanaachia vitambulisho vyao vya kura.acha shida iwakamate mpaka miaka mitano ikiisha watapata chembechembe za akili.
 
Today at Movenpick Hotel, once again National Housing Corporation (NHC) has officially announced the sale of New Units to be built at Ubungo, This was announced today by the Mr David Shambwe who is the Director of Business Development at National Housing Corporation. David started by inviting Tanzanian residents and non - residents who are interested to purchase the house in our newly constructed apartments at Ubungo surburb of Kinondoni Municipality.The project is expected to be completed within 9 months. The Selling Price for an apartment is TZS 67,946,567.86 (VAT exclusive). There are 80 units only available for sale.

Mkuu yaliyopo juu nimenukuu toka Tovuti ya NHC pia nimekuta ni shirika lililokabidhiwa majukumu mapya baada ya mashirika mawili kuunganishwa Msajili wa majumba na shirika la nyumba. Nalo limetakiwa kuwa na mwelekeo wa Kibiashara zaidi kuliko Huduma. Na bila shaka hilo ndio linalopelekea Bei ya vyumba viwili na sebule za kuungana na jiko na choo/bafu kimoja kuwa Tzsh 68m = na wastani wa $ 45,333.
Jiulize ni wangapi kati Watanzania wa kawaida wataweza kuambulia hizo Flat on their life time? Kipato cha kawaida mnakielewa. Nadhani shirika hili lisibebe jina la shirika la taifa, liwe Shirika la Biashara ya Nyumba (au fulani hivi) Na liundwe Shirika la nyumba la taifa litakalokuwa na wajibu wa kujenga Nyumba zinazokidhi mahitaji ya Nyumba kwa Maana halisi ya Mahitaji ya Nyumba.

Wana JF hebu tulijadili hili la waathirika wa mafuriko.Nimekuwa nafatilia taarifa za habari naona makampuni na watu binafsi wanajitolea kwa moyo kuwapa msaada wenzetu walioathiriwa na mafuriko. Ni swala jema na la kujivunia kwamba Watanzania bado tuna moyo wa kujitoa na kuwasaidia wenzetu. Kitengo cha maafa cha Mizengo Pinda ambaye yuko likizo nahisi nacho kiko likizo.
Sasa kwa swala la makazi, hata kama watapewa viwanja kama JK alivyosema, sidhani kama wana uwezo wa kujenga nyumba mpya.Maisha yao yameathiriwa sana kuanzia kisaikolojia mpaka kifedha.

Nadhani ule mpango wa NHC wa kujenga nyumba na kuwakopesha wananchi kwa kutumia mikopo maalum ya benki ndo ulitakiwa uanzie hapa. NHC ingejenga nyumba za bei nafuu then hawa watu wapangishwe na wasaidiwe kupata mikopo hiyo bank na serikali iwaguarantee.

Jamani kwa sisi wa kipato cha chini, nadhani tunajua ilivyo kazi kujenga nyumba. Mtu alishajikusanya mpaka akaweka kajumba kake japo ni bondeni lakini alikuwa anaishi vema na familia yake (na serikali ilishamuwekea na umeme). Sasa mvua imepiga na vitu vimesombwa na Mungu bariki nyumba haijabomoka, unadhani mtu huyu atakubali kuhama aache kajumba kake akachukue uwanja mtupu huko kusikojulikana???
Hebu serikali yetu ingawa sio sikivu basi angalau kupitia kwa wana JF walio karibu na Baba Riz , Prof. Tibaijuka na mteule wa Luhanjo (Nehemia Mchechu) wawafikishie wazo hili. La sivyo tutaendelea kuona mafuriko kila mwaka mvua zikipiga.
Nawasilisha
 
Mkuu wazo zuri lakini wengi wanaoishi hasa pale jangwani siamini kama wanakopesheka! Labda useme serikali iwajengee na kuwapa bure manake tukisema NHC itumie pesa za mkopo toka bank halafu iwajengee nyumba na kuwakopesha basi tutakuwa tunaichimbia kaburi. Pili mkuu kuna changamoto nyingine kwamba watu wanaoishi maeneo yalipatwa na mafuriko wapo karibu na maeneo ya mjini ambako ndipo kuna shughuli zao za kuwapatia kipato. Wapo karibu na mjini hivyo huwa wanenda kwa miguu tu hawapandi daladala! Ukiwatoa hapo na kuwapeleka huko inakosema serikali tayari kuna mgogoro mwingine: nauli ya kuwafikisha mjini; Tshs. 1200 kwa siku! Serikali inabidi iwatafutie shughuli za kufanya huko huko watakakoenda.
 
Keep dreaming

Umeme hatuna

infrastructure hakuna

pesa hatuna

watu wa mabondeni unafkiri wanapenda kuishi kule?
 
wazo zuri lakini fedha za NHC sio za Nehemia Mchechu wala Tibaijuka twende taratibu sio kwamba kwa kila atakayefanya makosa katika kuyapanga maisha yake atachota kwenye hazina yetu bila utaratibu. tukifanya hivyo kila mtu atakimbilia mabondeni ili apate fidia au ajengewe nyumba
 
Mhhhh! Haya bwana!

Huyo mtu anayeishi ikuru hakuna jambo linalompa taabu kabisa, labda asikie ya babu seya. Haya ya mafuriko, njaa, elimu, ukabila, upendeleo, migomo ya mafuta, nk. kwake siyo taabu kabisa. kwa ujumla hatuna mtawala wala kiongozi. Muhimu wahindi bado wanaleta nguo toka uchina na tunaficha uchi basi!
 
wazo linazungumzika wadau watakuwa wamekusikia lakini bila utafiti NHC wasiingie kichwa kichwa wanaweza kupata hasara kwenye mradi huu ni vema wakajipanga kimkakati ili baadaye wasije wakatuhumiwa kwamba waliwekeza kwenye hasara kwa nia ya kuliibia shirika
 
hata mnaoishi majumbani familia zimewashinda lakini mko wepesi kuikosoa Ikulu. Familia bora huzaa taifa bora
 
ukivunja kanuni kubwa kwenye familia kanuni hiyo itatafuta namna ya kukuvunja wewe na falimia yako na kama itakukosa itavunja kizazi chako na baadaye taifa legelege. si kila jambo ni la serikali
 
wazo linazungumzika wadau watakuwa wamekusikia lakini bila utafiti NHC wasiingie kichwa kichwa wanaweza kupata hasara kwenye mradi huu ni vema wakajipanga kimkakati ili baadaye wasije wakatuhumiwa kwamba waliwekeza kwenye hasara kwa nia ya kuliibia shirika
Mkuu NHC wako kibiashara zaidi busara inaelekeza kwamba wasijiingize kwenye hili hata kidogo hata wafanye utafiti gani. Kama serikali inataka kuwajengea nyumba basi utumie wakala wake wa majengo. Yaani NHC ikope pesa ijenge nyumba kisha iwakopeshe wasiokopesheka!
 
Nehemia Mchechu ana ubora wa juu kuwa kiongozi wa NHC kama ni kweli alibebwa na Luhanjo basi hapa alipatia kumbeba kwa nafasi hii. kwa muda mfupi Nehemia kaonyesha uongozi tofauti na waliomtangulia. nehemia ni mzalendo wa kweli na haogopi kujenga maadui anapotekeleza wajibu wake au anapotetea taifa lake.... tafadhali nakuomba fuatilia nyendo zake utakubaliana na mimi
 
mkuu unataka waathirika wa mafuriko wapelekwe meru residential apartments?
lakini kwa upande mwingine acha hawa wananchi wakome kwa sababu wamezoea kudanganywa na ubwabwa mweusi na maji ya azam,vitumbo vikijaa wanaachia vitambulisho vyao vya kura.acha shida iwakamate mpaka miaka mitano ikiisha watapata chembechembe za akili.

Hapana mkuu baada ya kuelimishwa jujuman nimeitafuta NHC Web. Huko Meru mkuu hakuingiliki, Ubungo ni Tzsh 68,000,000 kwa Vyumba mbili Meru ni tzsh 175,000,000 kwa Vyumba tatu. Kweli Tanzania kuna pesa na wapo walionazo lakini ndio walewale 1% walioonekana US kumiliki kila kitu na 99% Kulala hoi.
Nakubaliana jjman shirika hili liwe la biashara hiyo ya nyumba za 1% na sie 99% tupatiwe litakaloendana na hali halisi.
 
wazo zuri lakini fedha za NHC sio za Nehemia Mchechu wala Tibaijuka twende taratibu sio kwamba kwa kila atakayefanya makosa katika kuyapanga maisha yake atachota kwenye hazina yetu bila utaratibu. tukifanya hivyo kila mtu atakimbilia mabondeni ili apate fidia au ajengewe nyumba

Naweza kukuelewa labda kwa kuwa hawa jamaa wa mabondeni hawana mtetezi. Kama ni suala la utaratibu, vipi wale wa EPA? walichota na wakaambiwa warudishe? je utaratibu ulifatwa? Wabunge wameongezewa posho juzi tu na wote tunajua kuwa utaratibu haukufatwa lakini kuna hatua yoyote iliyochukuliwa? Hawa wananchi tokea wanaanza kuenga miaka zaidi ya 20 serikali inawaangalia na naamini hata wakati wa uchaguzi kuna vituo vya kupigia kura huwa vinafunguliwa na tume maeneo hayo. hata chama cha magamba kina watendaji wa kata maeneno hayo. Nadhani bado kuna ,maswali mengi hapo hatuwezi kusema wananchi ndo wana makosa peke yao
 
Mkuu NHC wako kibiashara zaidi busara inaelekeza kwamba wasijiingize kwenye hili hata kidogo hata wafanye utafiti gani. Kama serikali inataka kuwajengea nyumba basi utumie wakala wake wa majengo. Yaani NHC ikope pesa ijenge nyumba kisha iwakopeshe wasiokopesheka!

Kimbunga umesema sana hapo: NHC limetawazwa kuwa shirika la Kibepari kwa maana halisi Kinadfharia na Kitendo kufanyia kazi Mawazo kama haya tutahitaji shirika jingine lipewe Mwangozo tofauti.
 
Back
Top Bottom