Mafunzo ya silaha kwa vijana wa kitanzania huko ethiopia

HOMOSAPIEN

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
745
271
Nilikuwa naangalia Taarifa ya habari ya ITV tarehe 3/7/2012 mara nikamuona kijana mmoja akitoa ushuhuda wa kuwa alikuwa anachimba dhahabu huko Mara karibu na mgodi wa North Mara mara wakatokea watu na kuwashawishi kuwa wana mgodi wao huko Kenya na wangependa kuwachukua huko kuwapa ajira ya kuchimba madini na vijana 3 wakakubali na wakaenda huko lakini walipofika kaskazini mwa Kenya wakapitishwa katika njia wasizojua tena usiku na kuishia katika mapori ya Ethiopia huko waliwakuta waTZ wengi wakifundishwa kutumia silaha idadi yao zaidi ya elfu 50.Nao wakaanza kupewa hayo mafunzo katika hali ya taabu sana,mtoa ushuhuda anadai yeye alitoroka na kufanikiwa kurudi TZ na amewaacha wenzake huko kwa mtazamo wake wako vijana wa TZ kam laki 5 hivi wakiendelea kupewa mafunzo hayo,naomba mnisaidie huu siyo mpango mbaya kwa nchi yetu?vyombo vya usalama vinazichukuliaje taarifa hizi?mbona sijasikia hata kiongozi mmoja akikanusha au kuguswa na jambo hili?au kulifuatilia kwa kuwa limetolewa hadharani,wasiwasi wangu ni kupuuzwa kwa taarifa kama hizi ambazo kama ni kweli zinaweza kutuletea hatari kubwa hata kama malengo ya mafunzo hayo siyo kwetu ni Somalia Djibuti Uganda Kenya n.k
 
Taarifa yako ni nzuri na Useful.
Nilipoona shida ni pale kwenye namba ya vijana hao.
Kuna mahala umesema Hamsini elfu, na kisha tena ukasema Laki Tano. Weka sawa takwimu zako!
 
Taarifa yako ni nzuri na Useful.
Nilipoona shida ni pale kwenye namba ya vijana hao.
Kuna mahala umesema Hamsini elfu, na kisha tena ukasema Laki Tano. Weka sawa takwimu zako!
Bado yuko sahihi kwani laki tano ni zaidi ya elfu hamsini
mwanzo kasema kawakuta vijana zaidi ya 50,000
halafu akasema kama laki tano hivi, bado yuko palepale.
 
500،000: kwa namba hii kila mwana jf angekuwa anamjua angalau,kijana mmoja ambaye yuko kwenye jeshi hilo. Naamini kuna vijana wengi wa Tz wako kwenye majeshi mbalimbali-sudan, congo, ethiopia , al shabaab, boko haram , al qaeda, janjaweed n.k na ushahidi upo( e.g.gailan)
 
Waoh, hata kama angekuwa mmoja still ni tatzo because,
moja kwenye jumuia ya kimataifa ni rahisi kuonekana tunasaidia vikundi haramu, jumlisha na kachumbari ya our new "friends" Iran
mbili tunaweza kuingia kwenye migogoro na nch husika mana siamin kama wapo kwenye majesh halal ya nch hzo,
tatu wakirudi huku itakuwaje?kiusalam mana wakimwagika kitaa plus hawana ajira na maujuzi kibao patanuka apa,
my take
chombo husika washugulikie haraka mana ni tatizo kubwa kuliko linavoonekana kwa sasa
 
Nafikiri wakirudi watatumia uzoefu wao kufyeka msitu wa mabwepande.
 
Mi NILIANZA KUJIULIZA KWAMBA KAMA KWELI KUNA VIJANA WENGI KIASI HICHO BASI HILI NI JESHI KABISA
TUKIWAONGEZA NA WA BODA BODA HAPO NAJUA NI KWERE NA NI HATARI KUBWA.
 
Kwa cku zijazo, amani yawezabaki kuwa historia... Naiona hatari, nilishaandaa andaki kwa ajili ya familia yangu. Mim¨¬ binafsi sitakimbia wala kujificha. Nitakabiliana na hali face 2 face
 
Hizi habari si za kupuuza,mafunzo ya karate kwenye misikiti,vijana kupelekwa nje kwa mafunzo kama haya,si dalili nzuri.
 
Nilikuwa naangalia Taarifa ya habari ya ITV tarehe 3/7/2012 mara nikamuona kijana mmoja akitoa ushuhuda wa kuwa alikuwa anachimba dhahabu huko Mara karibu na mgodi wa North Mara mara wakatokea watu na kuwashawishi kuwa wana mgodi wao huko Kenya na wangependa kuwachukua huko kuwapa ajira ya kuchimba madini na vijana 3 wakakubali na wakaenda huko lakini walipofika kaskazini mwa Kenya wakapitishwa katika njia wasizojua tena usiku na kuishia katika mapori ya Ethiopia huko waliwakuta waTZ wengi wakifundishwa kutumia silaha idadi yao zaidi ya elfu 50.Nao wakaanza kupewa hayo mafunzo katika hali ya taabu sana,mtoa ushuhuda anadai yeye alitoroka na kufanikiwa kurudi TZ na amewaacha wenzake huko kwa mtazamo wake wako vijana wa TZ kam laki 5 hivi wakiendelea kupewa mafunzo hayo,naomba mnisaidie huu siyo mpango mbaya kwa nchi yetu?vyombo vya usalama vinazichukuliaje taarifa hizi?mbona sijasikia hata kiongozi mmoja akikanusha au kuguswa na jambo hili?au kulifuatilia kwa kuwa limetolewa hadharani,wasiwasi wangu ni kupuuzwa kwa taarifa kama hizi ambazo kama ni kweli zinaweza kutuletea hatari kubwa hata kama malengo ya mafunzo hayo siyo kwetu ni Somalia Djibuti Uganda Kenya n.k
Sasa mkuu HOMOSAPIEN ulitaka wakifuatilia walete jamvini kukwambia mpaka sasa hivi tupo mpakani mwa kenya tunafatilia hizi habari tulizozipata katika vyombo vya habari hivyo taarifa za kiinterejensia tutawaletea karibuni ni wapi tumefikia!!Je Kweli mkuu ndicho ulikuwa unasubiri hapa jamvini??au unataka kuvitukana vyombo vya usalama kuwa havijui kazi yao mpaka wewe umeleta uzi humu wakati wahusika wamekaa kimya??je ndivyo ilivyo??nakusubiri.....
 
Naamini kama wangekuwepo huko kweli, watu wanaojali Usalama hapa duniani [America] wangeshainyooshea kidole Tanzania mapema sana, hata kabla sisi hatujastukia.
 
Hapana Mkuu KakaKiiza Nimeshindwa tu kuelewa kwanini wakuu wamekaa kimya sana wakati jambo lenyewe ni nyeti kwa usalama wetu,Hizo meli za Iran kupeperusha bendera ya TZ waziri kasema jambo je hili la nguvukazi ya kijeshi mbona Mkuu anayeshughulikia hasemi jambo hata kusema tu nashtuka na habari hizi hata kama hazina ukweli, ujue KakaKiiza waswahili wanasema"panapofuka moshi pameficha moto".
 
Hizi habari si za kupuuza,mafunzo ya karate kwenye misikiti,vijana kupelekwa nje kwa mafunzo kama haya,si dalili nzuri.

Sishangai taarifa Kama hii tena humu ndani kwani ni Kama ile taarifa ya Dr SLAA na makontena ya kura kumbe vipodozi na nyinginezo kwahiyo kuna mambo si yakuyaweka sana akilini ni muhimu kwa Dr SLAA hizi mpelekeeni hana jipya sasa amemaliza kwahiyo ...

Mkumbusheni aanze na EPA na KAGODA NA MEREMETA Hatumsikii jamani tumezimiss hizi agenda...

Ah kumbe jana alitoka na kutaka kuuliwa Doh hivi Yule unahitaji intelligence kweli si SAMBA MOJA TU kwisha au LEMA SIJUI NI INTELLIGENCE gani inahitajika hao usalama waniajiri mimi...
 
Kazi ya wanaUsalama wa TZ ni kuakikisha majambazi ya ccm yanaendelea kuiba na kupeta mitaani... Mambo kama haya hayawahusu kabisa...
 
Naamini kama wangekuwepo huko kweli, watu wanaojali Usalama hapa duniani [America] wangeshainyooshea kidole Tanzania mapema sana, hata kabla sisi hatujastukia.

subiri, wakati ukifika hao unaowaita USA watanyoosha kidole, kumbuka kuwa kwao uwepo wa watanzania huko ni mtaji mkubwa sana wa kuifanya nchi ibuluzwe kama castrated bull.
 
Back
Top Bottom