Mafunzo ya kilimo cha kisasa cha greenhouse

LEX STEELE

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
224
110
Nimepitia threads zenu wazalendo lakini naona mnatwanga majio kwenye kinu tuu. Mimi nataka nifanye kilimo kwa mapigo haya....kisanyansi, eka chache kwa kuanza....orders zangu ni za ndani na nje ya nchi...mnasemaje? Hapa ninao mizungu iko tayari kuingia ubia hata kwa 50/50

Leteni startup break downs na ipi itafaa kwa Tanzania...kama kuna mtu yuko serious ku share ideas niko tayari e-mail yangu ni:

kilimokwanza2013@gmail.com

images

===========================================
@Lasway.Jr POST

KILIMO CHA KISASA CHA GREENHOUSE (BANDA KITALU) NA FAIDA ZAKE

Na
Engineer Octavian Justine Lasway
Irrigation And water resources engineer
0763347985

info@greenagricultureskills.com
Green Agriculture
Ndugu Msomaji karibu tena leo tujuzane kuhusu banda kitalu yaani Green house

Nini Maana ya Green House?
Green house ni hali nuai(artificial environment) ya kimazingira iliyotengenezwa kwa ajili ya uhitaji fulani wa kitu(zao) ambacho hakiwezi/kinaathirika kikiishi katika mazingira halisia au hakiendani na mazingira halisia na ningependa ujue ya kuwa green house sio ile nyumba bali ni ile hali ya ndani inayotengezwa na ile nyumba.

Hali mbali mbali zinaweza kutengenezwa na green house kama maeneo ni ya joto sana na unataka kulima mazao yanayostawi sehemu za baridi unaweza kutengeneza green house ambayo italeta hali ya baridi na pia kama upo maeneo ya joto na unataka kulima mazao mazao yanayostawi sehemu za baridi unaweza kutengeneza green house kwa ajili ya kuleta hali ya baridi na ukafanya kilimo chako bila shida yoyote tena kwa ufanisi mkubwa

NOTE: katika ununuzi wa materials hakikisha ununua kwa mtu mwenye uelewa ili akupe material inayoendana na eneo lako ili upate matokeo mazuri hasa nylon cover kwa nchi za tropical ni ile yenye standard ya 200micron

Greenhouse(Banda Kitalu)
Hii ni teknolojia ya kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo yataisaidia mimea/mazao kumea vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea hii inapandwa kwenye banda, au nyumba maalumu. Teknolojia hii inatumika hasa kuikinga mimea usiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa.

Mazingira haribifu ni kama upepo mkali, baridi kali, mvua kubwa, au mvua za mawe, mionzi mikali ya jua, joto kali , wadudu pamoja na magonjwa. Hayo ndio mazingira ambayo teknolojia hii inaleta suluhisho, kuhakikisha mimea inastawi vizuri bila ya kuathiriwa na moja ya matatizo hayo yaliyotajwa.

Teknolojia hii ilivumbuliwa huko kwenye nchi za baridi, zaidi ya karne moja na nusu (miaka 150) iliyopita. Nchi zilizopo ukanda wa baridi, mazao ya kitropiki (mazao yanayo pendelea joto) ilikua haiwezekani kabisa kulimwa maeneo hayo ya ukanda wa baridi.

Ndipo hapo wazo la kuvumbua Greenhouse lilipoibuka. Nchi hizi walianza kutumia teknolojia hii maana nyumba hii ya kitalu ilikua ina uwezo wa kutunza joto, na hivyo wakaanza kulima mazao ya ukanda wa joto kama mbogamboga (nyanya, hoho) na matunda. Pamoja na teknolojia hii kuanza kitambo kidogo katika nchi zilizoendelea, lakini kwa upande wa nchi zinazoendelea bado teknolojia hii ni mpya kwa watu wengi.

Teknolojia hii pia inatumika katika nchi za joto, japo kuna utofauti kati yake na zile za nchi za ukanda wa baridi na tofauti yake ni kwenye materilas zinazotumika kutengengenezea hasa polycover tujue kuwa katika dunia yetu kila ukanda una kiwango chake cha mionzi ya jua inayofika eneo husika kwa hiyo green house materilas zinazotumika katika nchi za baridi zina microyn tofauti na zile zinazotumika ukanda wa tropiki mfano kwa tanzania tunatumia polycver yenye 200 micron kuendana na hali ya hewa yetu na usipotumia material ya aina hyo mimea yako itaungua au kutokukua vizuri ndio maana tunashauri ufanye kazi na wataalamu ili upate uhakika wa kile kitu unachokifanya kwa manufaa yetu sote

FAIDA ZA GREENHOUSE
1. Mavuno yanakua mara 10 hadi 12 zaidi ya kilimo cha eneo la wazi,ikitegemea aina ya mazao yanayolimwa humo, aina greenhouse pamoja na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya greenhouse.

2. Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka. Maana Greenhouse inaweza kuzuia visababishi vya uharibifu wa mazao kama wadudu waharibifu na wale waletao magonjwa kwa mimea.

3. Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha mwaka, maana huhitaji kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.

4. Uwezo wa kuzalisha kipindi ambacho sio cha msimu (off- season) kwa vile kipindi hiki watu wengi hawazalishi kutokana na mazingira kutoruhusu, ukiwa na greenhouse una uwezo wa kuzalisha kipindi hicho na ukapata bei za mazao ziko juu na unapata faida kubwa

5. Ufanisi katika utumaji wa dawa, viwatilifu katika kudhibiti kwani wakati mwingne dawa hazitumiki kabisa kwenye green house.

6. Matumizi bora ya maji kwani drip irrigation system ndio hutumika kwenye green house na ina ufanisi mkubwa katika ufikishaji wa maji kwa mimea na hupunguza upotevu wa maji

7. Uwezo wa kutunza mimea inayozalishwa maabara kutokana na teknolojia ya tishu (tissue culture technology) mimea inapotoka maabara kabla haijapelekwa shambani inatunzwa kwanza kwenye greenhouse maalumu kwa ajili ya kuzoea mazingira ya nje kwanza. wataalamu wa SUA wanafanya sana hii

8. Uwezo wa kupanda mimea bila kutumia udongo (Hydroponic). Kutokana na changamoto ya magonjwa na vijidudu vya kwenye udongo kama Nematodes, ndipo uvumbuzi wa teknolojia ya kupanda mimea kwa kutokutumia udongo ulipotokea

MFUMO WA UMWAGILIAJI KWENYE GH

mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone yaani drip irrigation system ndio unatumika sana katika green house kwani ndio mfumo rahisi na wenye ufanisi mkubwa sio tuu katika kuhakikisha mmea wako unapata maji shahiki bado katika kubana matumizi ya maji pia,

katika mfumo huu tunaweza kuweka mbolea moja kwa moja kwenye mfumo wako na mimea ikapata mbolea kwa njia hii (fertigation) mbolea inawekwa kwenye tank la maji lakini hii ni vizuri ukapata ushauri wa kitaalamu ili tukuambie namna ya uwekaji wa mbolea na kiwango cha kuweka

ARDHI, UDONGO KWENYE GH

Ni muhimu kapima udongo kabla ya kuwaza kulima pia hata kwenye kilimo hiki cha kutumia green house ni vizuri kupata data za udongo katika mambo yafuatayo

kwanza kabisa data za udongo husaidia katika kufanya design ya mfumo wa umwagiliaji ili mimi mtaalamu niweze kukuambia utamwagilia kwa muda gani na baada ya siku ngapi ( irrigaton time and irrigation intervval mfano mwagilia masaa matatu kila baada ya siku mbili) na calculation zinafanywa kuendana na uhitaji wa maji katika zao lako na uwezo wa udongo wako kubeba maji .

katika green house kuna kitu tunakiita soil develpment yaani ni kuuandaa na kuuongezea udongo rutuba kwa kutumia mbolea asilia na mchanganyiko wa madini mengine ili udongo uweze kuwa na uwezo wa kuupa mmea mahitaji yake lakini ni vizuri kupima udongo ili mtaalamu aweze kujua ni kiwango gani za mbolea na samadi na vitu vingine vinahitajika katika udongo wako ili mazao yaweze kustawi vzr kwa wateja wetu huwa tunawapa offer ya soil test bure ili waweze kumudu gharama katika uwekezaji huu

Baadhi ya Nchi zinazofanya vizuri kilimo cha Greenhouse.
Kuna nchi zaidi ya 50 katika dunia ambapo kilimo kinalimwa kwenye greenhouse. Tutaangalia baadhi ya nchi ambazo zimekua zikifanya vizuri kupitia teknolojia hii.

Tuanze na Marekani, Marekani ina eneo takribani 4000 hekta ambazo zina greenhouse kwa ajili ya kilimo cha maua, Marekani kupitia kilimo hicho wanapata pato la zaidi ya Dola bilioni 2.8 (zaidi ya trilioni 5 hela za Tz) kwa mwaka.

Nchini Hispania inakadiriwa zaidi 25,000 hekta na Italia ni hekta 18,500, zimefungwa greenhouse kwa kilimo cha pilipili hoho, strawberry, matango, maharagwe machanga, pamoja na nyanya Canada greenhouse ni kwa kilimo cha maua na mboga mboga wakati ambapo hazilimwi kwingine. Mazao maarufu yanayolimwa kwenye Greenhouse za Canada kama nyanya, matango na hoho.

Uholanzi ni zaidi ya hecta 89,600 zipo nchini ya greenhouse. Uholanzi sekta ya greenhouse ndio iliyo bora zaidi duniani. Uholanzi ndio nchi inayoongoza kwa teknolojia hii na wamepiga hatua mbali sana. Yapo makampuni makubwa ya Kiholanzi yanayotumia teknolojia hii baadhi yao yapo hapa Tanzania katika kilimo cha maua, matunda, mbogamboga, pamoja na mbegu. Mfano : Kili Hortex, Multi flower, Mount Meru Flower, Enza Zaden, RJK ZWAAN (Q-SEM na AFRISEM)

Israel: 15000 hekta. Israel ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza maua (cut flowers) nje ya nchi. Japokuwa nchi ya Israel eneo lake ni kubwa ni jangwa. Pia Nchi ya Israel imekua moja ya nchi zilizopo mstari wa mbele katika teknolojia ya umwagiliaji na Greenhouse.

Uturuki: hekta 10,000 zinalimwa maua na mbogamboga kwa kutumia teknolojia hii ya Green house. Saudi Arabia: 90% ya mazao yanya na tango yanalimwa kwenye green house. Misri 10,000 hekta nyanya, matango na pilipili hoho. Teknolojia ya Greenhouse nchini China inakua kwa kasi sana kuliko nchi yeyote duniani.

Japokuwa teknolojia hii haijaanza muda mrefu kivile huko China lakini mpaka sasa zaidi ya hekta 48,000 tayari zimefungwa Greenhouse. Nchi nyingine zinzofanya vizuri barani Asia ni kama Japan (40,000hekta) na Korea kusini (21,000 hekta).

AINA ZA GREENHOUSE
Greenhouse zinagawanyika makundi mbalimbali kutegemeana na vigezo vifuatavyo:

1. Aina za Greenhouse kwa kigezo cha sura/umbile (shape)
Zipo aina aina 8 za greenhouse, hapa nitataja chache tu kwa majina yake ya kitaalamu

kwa hapa kwetu mara nyingi tunatengeneza gh za iana tatu ambazo zinafanya vizuri sana kama slant roof green house kama ilivyo kwenye picha hapa tunatumia mbao(miti) au chuma

a)Quonset Greenhouse

b) Saw tooth type

iii. c)Even span type greenhouse
iv. d)Uneven span type greenhouse

2. Aina za Greenhouse kwa kigezo cha Matumizi

a)Green house zinazoongeza joto (Hizi ni kwa maeneo ya baridi)

i b)Greenhouse zinazopunguza joto (hizi ni kwa maeneo ya joto)

3. Aina za greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake (construction)

a)Greenhouse za miti (Wooden framed structure)

i b)Pipe framed structure (Greenhouse zinazotumia mabomba)
Truss/Aluminium framed structure ( Geenhouse zinazojengwa kwa vyuma

4. Aina za Greenhouse kwa kigezo aina ya zana za ufunikaji (covering types)

a)Greenhouse zinazofunikwa kwa zana za Vioo (glass)- hizi zinatumika sana maeneo ya baridi kali, ili kutunza joto kwa muda mrefu ndani greenhouse

b)Greenhouse zinazofunikwa kwa mifuko ya nylon (polycover)

5. Aina ya Greenhouse kwa kigezo cha uwekezaji unaofanywa

Katika green house unaweza kulima mazao mengi hasa ya mbogamboga na matunda ambayo yana soko zuri na uapatikanaji wake ni adimu sana , kwa kuwa kilimo cha gh ni uwekezaji bora kwenye kilimo

ORGANIC FARMING(KILIMO HAI)
hiki ni kilimo ambacho huhiji kutumia kemikali zozote wala mbolea za viwandani yaani ni kilimo asili, kwa nchi za wenzetu mazao ya kilimo hai yana bei mara kumi zaidi ya mazao ya kilimo cha kawaida kwani kukua kwa teknolojia na uharibifu wa mazingira bidhaa za kilimo zimekuwa zikitumia kemikali nyingi sana ambazo huathiri afya ya binadamu moja kwa moja au madhara huonekana baadaye sasa ukiwa na green house utaweza kufanya kilimo hiki na familia yako ikatumia chakula safi ambacho hakijawekwa chemikali

kwa mahitaji ya kutengenezewa green house ya kisasa kwa bei nafuu wasiliana na mimi pia baada ya kukutengenezea structure yako hatutakuacha hivi hivi ila tutakupa mtaaalamu wetu ambae ni Agronomist Boniphace Mwanje(0719880905) aliebobea kwenye utaalamu mbegu,mbolea,madawa na utunzaji wa mimea na huduma nyingne za aina zote za umwagiliaji, kupima udongo, kuchora na kupanga ramani za mashamba na taasisi au kampuni

Engineer Octavian Justine Lasway
Irrigation And water resources engineer
0763347985
info@greenagricultureskills.com
Green Agriculture

Habari zenu

Kutokana na umuhimu wa kilimo katika nchi yetu nimeamua name nitoe mchango wangu kama mdau. Watanzania takriban asilimia 80 wameajiriwa au kujiajiri katika sekta ya kilimo yet bado wameanguka katika lindi la umaskini wakati ardhi ya kutosha na yenye rutuba tunayo.

Vijana wengi wamekuwa wakikimbilia mijini kutafuta kazi za kuajiriwa na mwisho wa siku kazi zenyewe hazipatikani wanaishia kuzurura tu mitaani. Wachache wameamua kufanya kilimo kidogo kidogo huku mijini kama vile vibustani na kadhalika, ingawa havina tija.

Watu ambao wamefanikiwa katika kilimo wenye mashamba makubwa wako vijijini ila waliofanikiwa katika kilimo ambao wako mijini wamefanikiwa katika mashamba madogo. Mashamba haya yanaitwa GREENHOUSE. Kilimo cha greenhouse kimewatoa watu wengi mmoja wao akiwemo mwanasiasa maarufu na jamaa mmoja nilimuona kwenye kipindi cha amka na badilika cha TBC1 akielezea kilimo chake, Mimi pia nina mjomba wabgu yuko kibaha amefanikiwa katika kilimo hiki.

Mimi kutokana na uzoefu wa mjomba wangu, nimeamua kutoa mafunzo haya ya kilimo bora cha kisasa cha greenhouse kwa ghara,a y ash. 15,000/- tu. Mafunzo haya nimeyaandaa katika kitabu (ebook) softcopy ambayo utaipata kwa kunipigia simu 0758 308193.

Katika kitabu hiki utajifunza yafuatayo:
  1. Jinsi ya kutumia eneo lako la hatua kadhaa na kuzalisha mazao yenye uwezo wa kukuingizia Zaidi y ash 600,000/- kwa mwezi
  2. Kupata gharama za kuanzisha mradi huu. Na gharama yake ni chini y ash. 500,000/- ingawa kwa kutumia ujanja Fulani unaweza anza hata kw ash. 250,000/-
  3. Si lazima uwe na eneo kubwa kuanza mradi huu, hata kama una hatua 5x8, unaanza.
Faida chache za greenhouse:
  1. Haihitaji gharama kubwa
  2. Si kilimo cha msimu, utaweza kuvuna mwaka mzima
  3. Mazao yako hayaliwi na wadudu wala magonjwa
  4. Unapata mazao mara 10 ya anayelima kwenye shamba la kawaida
  5. Na kadhalika
Karibuni sana tuelimike.

TAHADHARI USIDANGANYWE KIRAHISI NA HAWA WATU WANAO PROMOTE KILIMO CHA GREENHOUSE UTAFILISIKA!!!!!!
Tahadhari sana wa JF. Ukweli ni kwamba watu wanao-promote kilimo cha aina hii wanafanya hivyo ili kupata faida, bila kuwaambia watu ukweli kwamba kilimo hiki si rahisi kama wanavyofikiria.

Kilimo hiki kinawezekana maeneo ya baridi, lakini sehemu za joto kama hapa Dar utakuwa unatengeneza oven ya kupikia mazao uliyopanda badala ya greenhouse ya kufanya upate mazao mengi!!!

Watu huko Uganda wameshalizwa sana na hili suala la kilimo cha greenhouse. Usidanganywe!!! Kwanza, ili greenhouse yeyote ifanikiwe inatakiwa kiwango kikubwa cha ku-control joto, hata kutumia compyuta. Je wewe utaweza?

Kwa taarifa zaidi, soma makala hii hapa chini, na hakikisha unawatahadhalisha wengine.

Dont be Fooled!!! What you need to know before you invest in greenhouse
True, there is money in greenhouse farming. But it is not easy money, as the aggressive promoters of greenhouse technology would want farmers to believe.

To get the picture, look at abandoned greenhouse structures scattered around Kampala and neighbouring districts like Wakiso and Mukono. The owners are frustrated farmers who invested millions expecting quick returns, only to lose it all.

False promises
Lured by the high returns projected by fast-talking promoters masquerading as greenhouse technology experts, many aspiring farmers, especially the young corporate class, took bank loans, drew their savings, or liquidated fixed assets to invest in a greenhouse.

You cannot blame them for being gullible. The returns on investment projected by the greenhouse promoters are simply irresistible. One lady was assured of 400 per cent in profits within half a year. She invested Shs10m expecting Shs40m in six months. But instead she lost an entire crop of tomatoes to a wilt disease at the flowering stage.

The people who supplied the greenhouse structure and equipment, kept suggesting different chemical combinations, which the desperate farmer had to buy from them. She faithfully applied the chemicals but the tomatoes continued wilting as if they had been planted in a sauna.

Get knowledge
Finally, the truth hit her in the face like a basket of rotten tomatoes. The so-called greenhouse experts were actually gamblers, who were just using her as a guinea pig.

In greenhouse farming, like any other farming enterprise, knowledge is power. But most farmers only want to know how much it will cost and how soon they will recover their money.

The right people to ask would be fellow farmers, who are already into greenhouse production. There are a few successful greenhouse farmers in Uganda. Visit them. There are many in Kenya, who can be visited through organised tours.

For those with internet access, there is a lot of information available. You can have virtual tours of greenhouse projects in Asia and other parts of the world, which have similar climatic conditions as Uganda.

From them, you learn about the opportunities and challenges in greenhouse farming. Some offer short courses in greenhouse management and other vital practical skills.

Besides inadequate knowledge, lack of commitment is another reason why many greenhouses in Uganda fail. Many Ugandans engaged in greenhouse farming have full-time jobs elsewhere. The day-to-day management is left to workers, whose competence and commitment are questionable.

Conditions in a greenhouse are constantly changing so the need for close monitoring. Plant growth is determined by the controlled conditions inside the greenhouse. Temperatures and humidity have to be kept constant around the clock. A greenhouse can easily overheat in the hot sun, leading to total disaster.

In technically more advanced countries like Israel, conditions are regulated with the help of computers. However in Uganda and most African countries, this still has to be done manually. In such a situation, monitoring the greenhouse on phone or visiting for a few hours over weekend cannot work.

YOU HAVE BEEN WARNED!!!!
 
Nimepitia threads zenu wazalendo lakini naona mnatwanga majio kwenye kinu tuu.

Mimi nataka nifanye kilimo kwa mapigo haya....kisanyansi, eka chache kwa kuanza....orders zangu ni za ndani na nje ya nchi...mnasemaje?

Hapa ninao mizungu iko tayari kuingia ubia hata kwa 50/50

Leteni startup break downs na ipi itafaa kwa Tanzania...kama kuna mtu yuko serious ku share ideas niko tayari e-mail yangu ni:

kilimokwanza2013@gmail.com

images

Mkuu mimi napenda unijulishe kilimo cha green house ni nini. Nina heka zangu kadhaa nalimamahindi na mananasi bagamoyo nami naweza piga hii mambo. Ila hakuna umemem shamba kwangu. Maelezo tafadhali
 
mkuu mimi napenda unijulishe kilimo cha green house ni nini. Nina heka zangu kadhaa nalimamahindi na mananasi bagamoyo nami naweza piga hii mambo. Ila hakuna umemem shamba kwangu. Maelezo tafadhali

mi nilikuwa nasoma tu kwenye geograph gree house effects, hadi leo sijui ni nini
 
Kilimo cha greenhouse ni kulima kwenye aina ya majengo kama picha iliyo hapo juu. Na hasa kwenye maeneo ya baridi ambapo unajaribu kuweka kama temperature na humidity vifanane na hali ya hewa ya ukuzaji aina ya zao pindi linapolimwa kwenye hali yake halisi (tropics). Vile vile gh farming huwezesha kwa kiwango kikubwa kuzuia magonjwa ya mimea kwani ile ni controlled environment.

Ukulima wa kwenye greenhouse ni ghali sana na haulipi kwa hapa kwetu, kwani unaweza kuotesha mazao mengi shambani ambapo jua na humidity ambavyo huvigharamii unaweza kuvitumia. Maintenance ya hizo greenhouses vile vile ni kikwazo (si unajua tena sisi na issue ya maintenance ya majengo?). Angalia hata zile zilizoko vyuoni tu ambazo ni za experiments basi zinashindikana.

Ukulima wa gh kwa Ulaya unafaa sana na hasa kama maua ambayo unaweza kuuza kwa bei mbaya huko kwao.
 
Mkuu inategemea unalima nini, kama ni value products (mfano bangi) au mazao yenye market ambayo yapo scarce na sokoni hayapo au ni ya bei ya juu then tumia mfumo huu wa kulima; kama unavyojua

Net Profit yako ni baada ya kutoa running costs zote.., sasa kama unalima nyanya kwenye green house wakati jirani yako yeye kazimwaga tu hapo nje (kumbuka wewe itabidi uuze bei ya juu ili upate faida kama yeye) pia sababu ya Capital investment yako itakuchukua muda ku-break even.. (lakini kama una soko tayari na ushafanya hesabu na kuona inalipa kila la kheri...,

Kumbuka faida ni pamoja na yield kubwa zaidi na kuweza kulima kwa msimu mzima na urahisi wa ku-control magonjwa n.k., lakini gharama ni bigger advantage.., kwahio angalia sana unalima nini (maua yanaweza yakakulipa sababu yana soko nje ya nchi)
 
green house ina cost pesa nyingi kidogo kwenye initial investment tu,gaada ya hapo haina running cost kubwa ndo maana kenya wana ongoza kwa kutumia teknolojia hii katika kilimo cha nyanya
 
Nimepata shauku kubwa sana ya kilimo cha mboga mboga ,hasa cha green house ,nawaombeni makisio yote ya kujenga greenhouse ni kiasi gani
 
Mkuu Mvita,

Nina shauku kama ulivyo nayo wewe na nimeshaanza kuuliza kuhusu hiyo green house. Tembelea tovuti ya hawa jamaa wanaitwa Balton wana ofisi Dar na Arusha Balton Tanzania | The official website for Balton Tanzania Ltd wanatengeneza hizo Green house na kukupa training. Pia kuna Green house za ukubwa wa 8X15 (meters)Tsh.6,000,000 na 8X24 Tsh.8,000,000

Nimewasiliana na Dada moja anaitwa Claudia atakupa maelezo kamili namba +255 717 944 435. Naomba waliowahi kufanya hii kitu watujuze zaidi.
 
kuna uzi umeongelea kwa kina sana hii kitu na mhusika yupo... do your homework kwenye jukwaa la biashara
 
Search topic hii humu humu, imeletwa na mdau mamaNa very cheap,affordable and durable.
 
Last edited by a moderator:
Just Caution: angalia value ya kile unachotaka kukilima kwenye hii greenhouse na soko lake na bei yake utakayouzia. Sababu ya initial cost of investment (kutengeneza greenhouse) na labda maintanance na mambo mengine unaweza ukajikuta unahitaji kuuza mazao yako bei kubwa kuliko wengine wanaolima tu kawaida. Kwahio weka vitu Premium na ambavyo havipo sokoni kwa wingi au lima vitu wakati ambao sio msimu wake ili kuuza bei ya juu.

Tanzania tumebalikiwa na hali ya hewa nzuri tofauti na nchi nyingine
 
Mkuu Mvita,

Nina shauku kama ulivyo nayo wewe na nimeshaanza kuuliza kuhusu hiyo green house. Tembelea tovuti ya hawa jamaa wanaitwa Balton wana ofisi Dar na Arusha Balton Tanzania | The official website for Balton Tanzania Ltd wanatengeneza hizo Green house na kukupa training. Pia kuna Green house za ukubwa wa 8X15 (meters)Tsh.6,000,000 na 8X24 Tsh.8,000,000

Nimewasiliana na Dada moja anaitwa Claudia atakupa maelezo kamili namba +255 717 944 435. Naomba waliowahi kufanya hii kitu watujuze zaidi.

Nami nilikua pale Mwenge jana for the same issue.
Nilionana na Mhusika na maelezo aliyonipa ni kama hayo hapo juu.
Ila aliongezea kua katika hizo package zao wanatoa na Mbegu, Mbolea & Madawa bure (inclusive in the price). Pia wanakua na site visit mara kwa mara. Ila Tank la Maji na Stand yake ni gharama zangu mteja.

Aliniambia kua mfano kwenye greenhouse yao ya mfano iliyoko palepale mwenge, eneo la 8m x 15m liliweza kutoa Tani zaidi ya 15 kwa mwaka kama sijasahau.

Wakaniambia kua kuna watu wanajitengenezeaga Greenhouse zao za kienyeji, zile nyavu na plastic wanazotumia zinakua na joto linalounguza mimea, wao za kwao wanazitia dawa.

Pia akasema kua kuna mbegu za kulimwa ndani ya greenhouse ambapo ukilimia nje ya greenhouse hazitoota vizuri, na kuna mbegu za kawaida za kulimia nje ya greenhouse ambazo ukilimia ndani ya greenhouse hazitoota vizuri pia.

Kingine alichoniambia Udongo pia ni wa kuupima kujua kama una-support mbegu za aina gani, na pia madawa na mbolea za aina gani. Lakini na maji nayo ni ya kuyapima kujua kama yanafaa kwa umwagiliaji kwani kuna maji mengine either yameharibiwa na shughuli za binadamu za kila siku (mf. kemikali kutoka viwandani) au eneo lilipo lina kemikali " just in nature".

Jamaa tuliongea mengi sana juu ya kilimo cha greenhouse, sema tu napo kwenye kianzio cha 6Mil (Green house ndogoya 8m x 15m) pamekaa parefu kidogo.
 
Nimepata shauku kubwa sana ya kilimo cha mboga mboga ,hasa cha green house ,nawaombeni makisio yote ya kujenga greenhouse ni kiasi gani

Karibu sana ndugu, tufanye jitihada za kuwasiliana kwa simu nikupe ushauri wa kina na muongozo mzima wa ukulima wa namna hii na technology nzima ya shamba kitalu (greenhouse).

Soma thread hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...08513-jenga-greenhouse-kwa-gharama-nafuu.html yote utapata maelezo mengi ambayo nimeshayatoa na ukiwa na laziada tuwasiliane kwa thread hiyo ili kuhakikisha kila mfatiliaji anafaidika na maswali yako.

Karibu.
 
Just Caution: angalia value ya kile unachotaka kukilima kwenye hii greenhouse na soko lake na bei yake utakayouzia. Sababu ya initial cost of investment (kutengeneza greenhouse) na labda maintanance na mambo mengine unaweza ukajikuta unahitaji kuuza mazao yako bei kubwa kuliko wengine wanaolima tu kawaida. Kwahio weka vitu Premium na ambavyo havipo sokoni kwa wingi au lima vitu wakati ambao sio msimu wake ili kuuza bei ya juu.

Tanzania tumebalikiwa na hali ya hewa nzuri tofauti na nchi nyingine

Ndugu pitia thread hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...08513-jenga-greenhouse-kwa-gharama-nafuu.html nimeeleza mengi sana kuhusu hili swala.

Karibu sana.
 
Nami nilikua pale Mwenge jana for the same issue.
Nilionana na Mhusika na maelezo aliyonipa ni kama hayo hapo juu.
Ila aliongezea kua katika hizo package zao wanatoa na Mbegu, Mbolea & Madawa bure (inclusive in the price). Pia wanakua na site visit mara kwa mara. Ila Tank la Maji na Stand yake ni gharama zangu mteja.

Aliniambia kua mfano kwenye greenhouse yao ya mfano iliyoko palepale mwenge, eneo la 8m x 15m liliweza kutoa Tani zaidi ya 15 kwa mwaka kama sijasahau.

Wakaniambia kua kuna watu wanajitengenezeaga Greenhouse zao za kienyeji, zile nyavu na plastic wanazotumia zinakua na joto linalounguza mimea, wao za kwao wanazitia dawa.

Pia akasema kua kuna mbegu za kulimwa ndani ya greenhouse ambapo ukilimia nje ya greenhouse hazitoota vizuri, na kuna mbegu za kawaida za kulimia nje ya greenhouse ambazo ukilimia ndani ya greenhouse hazitoota vizuri pia.

Kingine alichoniambia Udongo pia ni wa kuupima kujua kama una-support mbegu za aina gani, na pia madawa na mbolea za aina gani. Lakini na maji nayo ni ya kuyapima kujua kama yanafaa kwa umwagiliaji kwani kuna maji mengine either yameharibiwa na shughuli za binadamu za kila siku (mf. kemikali kutoka viwandani) au eneo lilipo lina kemikali " just in nature".

Jamaa tuliongea mengi sana juu ya kilimo cha greenhouse, sema tu napo kwenye kianzio cha 6Mil (Green house ndogoya 8m x 15m) pamekaa parefu kidogo.

Mkuu tembelea thread hii hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...08513-jenga-greenhouse-kwa-gharama-nafuu.html, kuna mengi sana nimezungumzia kuhusu swala hili.
Karibu tufanye biashara.
 
Habari zenu

Kutokana na umuhimu wa kilimo katika nchi yetu nimeamua name nitoe mchango wangu kama mdau. Watanzania takriban asilimia 80 wameajiriwa au kujiajiri katika sekta ya kilimo yet bado wameanguka katika lindi la umaskini wakati ardhi ya kutosha na yenye rutuba tunayo.

Vijana wengi wamekuwa wakikimbilia mijini kutafuta kazi za kuajiriwa na mwisho wa siku kazi zenyewe hazipatikani wanaishia kuzurura tu mitaani. Wachache wameamua kufanya kilimo kidogo kidogo huku mijini kama vile vibustani na kadhalika, ingawa havina tija.

Watu ambao wamefanikiwa katika kilimo wenye mashamba makubwa wako vijijini ila waliofanikiwa katika kilimo ambao wako mijini wamefanikiwa katika mashamba madogo. Mashamba haya yanaitwa GREENHOUSE. Kilimo cha greenhouse kimewatoa watu wengi mmoja wao akiwemo mwanasiasa maarufu na jamaa mmoja nilimuona kwenye kipindi cha amka na badilika cha TBC1 akielezea kilimo chake, Mimi pia nina mjomba wabgu yuko kibaha amefanikiwa katika kilimo hiki.

Mimi kutokana na uzoefu wa mjomba wangu, nimeamua kutoa mafunzo haya ya kilimo bora cha kisasa cha greenhouse kwa ghara,a y ash. 15,000/- tu. Mafunzo haya nimeyaandaa katika kitabu (ebook) softcopy ambayo utaipata kwa kunipigia simu 0758 308193.

Katika kitabu hiki utajifunza yafuatayo:

  1. Jinsi ya kutumia eneo lako la hatua kadhaa na kuzalisha mazao yenye uwezo wa kukuingizia Zaidi y ash 600,000/- kwa mwezi
  2. Kupata gharama za kuanzisha mradi huu. Na gharama yake ni chini y ash. 500,000/- ingawa kwa kutumia ujanja Fulani unaweza anza hata kw ash. 250,000/-
  3. Si lazima uwe na eneo kubwa kuanza mradi huu, hata kama una hatua 5x8, unaanza.

Faida chache za greenhouse:

  1. Haihitaji gharama kubwa
  2. Si kilimo cha msimu, utaweza kuvuna mwaka mzima
  3. Mazao yako hayaliwi na wadudu wala magonjwa
  4. Unapata mazao mara 10 ya anayelima kwenye shamba la kawaida
  5. Na kadhalika
Karibuni sana tuelimike.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom