Mafunzo kwa Walimu wa Sayansi wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu yaingia doa

Equitable

JF-Expert Member
Dec 24, 2021
2,010
5,449
Niipongeze serikali yetu kwa kutoa mafunzo kwa waalimu wa sayansi na hisabati nchi nzima. Zoezi hili zuri liwakumbuke na walimu wa art pia.

Ajabu wilaya ya Maswa mkoani Simiyu walimu wengi wa sayansi na hesabu hawajaenda kupata haya mafunzo. Sababu hazijaelezwa ila inasemekana rushwa kwa wakuu wa shule imepita.

Sasa najiuliza, waliopata mafunzo wamepewa mbinu bora za kufundisha kutoka "Content based " kwenda "Competence based"? Naimani ni kuwa watafundisha tofauti na wale ambao hawakupata mafunzo.

Swali: Je, wanafunzi waliofundishwa na walimu mahiri watapewa mtihani sawa na wale waliofundishwa na walimu wasio na mafunzo?

Naomba serikali iangalie hili kwa makini.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom