Mafunzo kwa Vitendo(Field) kwa Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza Yafutwa

Mouber

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
216
216
Leo kumeibuka taharuki kwenye mitandao ya kijamii baada ya taarifa kutolewa na kituo cha habari cha Chennel Ten kuwa hakutakuwa na Mafunzo kwa Vitendo yaani BTP ama Field kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kuanzia mwaka huu. Taarifa ambayo imetolewa na Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako.

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 14 katika kipindi cha habari za saa kinachopeperushwa na Channel Ten.

Sababu za kutokuwaruhusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwenda field ni kile kinachosemwa kuwa ni kutokuwa na ukomavu katika taaluma yao.

Source: Channel Ten
 
BTP (block teaching practice) haya ni mafunzo kwa njia ya vitendo kwa wanafunzi wa ualimu wa ngazi ya cheti na diploma. mm naunga mkono mawazo ya prof maana utoto ni mwingi sana kwa wanafunzi hawa.

chuo kikuu kuna TP na PT i.e (teaching practice kwa wanaosomea ualimu) na (practical train kwa kozi wanaosomea zisizo za ualimu). huku ningempinga vikali prof.
 
Anawafutia wanachuo wanaopata mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada na cheti anaacha wanaopata nafunzo katika ngazi ya chuo kikuu wakati nao husoma mbinu za ufundishaji wakiwa mwska wa pili na sio mwaka wa kwanza.Hili nalo ni tatizo kubwa,waziri na ametumia mamlaka yake vibaya.Kama ana lengo la kufuta na afute hadi kwa wanachuo wanaochukua shahada za ualimu kwasababu ya wao kusoma teaching methodologies wakiwa mwaka wa pili,kuacha waendelee ni kuacha pesa za field kwenda bure.
 
Leo kumeibuka taharuki kwenye mitandao ya kijamii baada ya taarifa kutolewa na kituo cha habari cha Chennel Ten kuwa hakutakuwa na Mafunzo kwa Vitendo yaani BTP ama Field kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kuanzia mwaka huu. Taarifa ambayo imetolewa na Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako.

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 14 katika kipindi cha habari za saa kinachopeperushwa na Channel Ten.

Sababu za kutokuwaruhusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwenda field ni kile kinachosemwa kuwa ni kutokuwa na ukomavu katika taaluma yao.

Source: Channel Ten
habari umeiandika kwa kukimbia sana ,wakati hata hujaielewa vizuri ,ungemskiliza kwa umakini ndio ukimbie kuandika jf
 
Hawajakomaa vipi,Laprofesseri hawa wanatupeleka wapi,kule field si kwa vitendo zaidi na kunauwezekano hata JKT mwakani isiwepo nchi iko ICU kiuchumi hazina imekauka ukiambiwa changanya na za kwake.
Kwa hili serikali haichomoki hata kama haijachomeka@Kikwete
 
Back
Top Bottom