Maduka ya watu wa Bara yachomwa Zanzibar; yadaiwa ni kampeni dhidi ya Muungano!

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Kwa kile kinachoonekana kama chuki dhidi ya watanganyika vijana wa kizanzibari wamechoa maduka huko unguja ya wafanyabiashara wenye asili ya bara na kusababisha hasara ya zaidi ya milioni 400.

Hawa wameuchoka muungano, hivi na sisi tukiamua kwenda hapo kariakoo itakuwaje?

Source: Radio TBC at 4PM

taarifa ya habari ITV

Last edited by a moderator:
Mh! Wanatupeleka kubaya hawa. hakuna haja ya kulipa kisasi, utoto unawasumbua, wakikua wataacha. Hata kama hawautaki Muungano sidhani kama hii ndio njiia muafaka yab kueleza hisia zao
 
Kwani nyie wabara mnatumia njia gani muafaka kuuenzi huo Muungano? Viongozi wenu huwa hawaelewi wanapooneshwa hisia za matakwa ya watu kwa maneno hadi wapewe intro kwa vitendo.

Wenzenu hawautaki Muungano ninyi mnalazimisha WHAT FOR?

Let this MUUNGANO thing dissolve peacefully.
 
Maisha yamewashinda hawana lolote hao, idadi ya wapemba na wa Unguja ni kubwa zaidi ya wabara walioko huko so watakula hasara zaidi wakijifanya hawautaki muungano
 
Kwani nyie wabara mnatumia njia gani muafaka kuuenzi huo Muungano? Viongozi wenu huwa hawaelewi wanapooneshwa hisia za matakwa ya watu kwa maneno hadi wapewe intro kwa vitendo.

Wenzenu hawautaki Muungano ninyi mnalazimisha WHAT FOR?

Let this MUUNGANO thing dissolve peacefully.

Kama walitaka kufikisha ujumbe wao kwa viongozi na ni jasiri wangeenda moja kwa moja kwa viongozi kuwaambia. Kuwatumia watu wengine wasio na hatia kufikisha ujumbe ni njia mojawapo ya kuonyesha ni jinsi gani ulivyo coward
 
source. radio tbc at 4PM Kwa kile kinachoonekana kama chuki dhidi ya watanganyika vijana wa kizanzibari wamechoa maduka huko unguja ya wafanyabiashara wenye asili ya bara na kusababisha hasara ya zaidi ya milioni 400. hawa wameuchoka muungano. hivi nasisi tukiamua kwenda hapo kariakoo itakuwaje?

Mi naenda kulipa pale Lindi-Ilala sasaiv-
 
Jana walichoma muswada wa katiba mpya, leo wamediriki kukuchomeeni hata maduka yenu, kesho mjiandae kuchowa ninyi wenyewe. Mungu ibariki Tan.....!!
 
mbona walishachoma baa za watanganyika kama 4 hivi miezi miwili iliyopita..
 
Mh!hakuna anayelazimisha kuwepo kwa muungano baina yetu sie wananchi mbali ya viongozi wanaoendelea kufanya unafiki kwa faida zao wenyewe,kwa maana hyo sie wananchi tusianze kuumizana sisi kwa sisi,maadui zetu ni viongozi tuwafate wao na kama bakora tuwachape wao kama vpi tuwafate hukohuko juu,ndo hayo tu....
 
Jamani nyie Wazanzibar mbona mnawaumiza wananchi wenzenu!!?msifanye hivyo maana mkimaliza kuchoma maduka ya watu wa bara mtayarudia makabila yenu mwisho wa siku mtamalizana wenyewe kwa wenyewe na hiyo itakuwa ni kanuni ya dhambi ya kubagua.
 
Si si eeem! Si si eeem! Si si eeem! Dhambi ya ubaguzi ukishaianza?
 
Ishu siyo muungano wala Watanganyika. Ishu ni kwamba kila binadamu anapo kuwa na matatizo lazima watafute scape goat. Zanzibar umasikini mwingini na wananchi hawajui nani wa kumlaumu. Sasa frustrations zao wana zitoa kwa Watanganyika. Ni kama Wasouth Afrika wanao ua wageni kisa hawana kazi wakati wanajua fika chanzo cha umasikini wao sio hao wageni. Zanzibaris are frustrated people.
 
Jamani nyie Wazanzibar ...msifanye hivyo
Duuh, cheki Bara wanavyobembeleza Muungano! Watu wamechoma mali unasema "jamani msifanye hivyo."

hivi ni ishu ya muungano au kuna kingine??
Bara bado wako kwenye denial masikini, hawaelewi somo, wenzenu hawataki Muungano!

mwada-wachanwa-430x320.jpg
 
Kwani nyie wabara mnatumia njia gani muafaka kuuenzi huo Muungano? Viongozi wenu huwa hawaelewi wanapooneshwa hisia za matakwa ya watu kwa maneno hadi wapewe intro kwa vitendo.

Wenzenu hawautaki Muungano ninyi mnalazimisha WHAT FOR?

Let this MUUNGANO thing dissolve peacefully.

Huu muungano haukuasisiwa na hao wenye maduka. Kwa nini watolewe kafara kwa maamuzi ya kisiasa ambayo hawana mamlaka nayo?

Bunge la muungano linaanza mwezi wa 7, nasubiri kwa hamu kumsikia Hamad Rashid pamoja na wabunge wote toka Zanzibar (bila kujali ni wa chama gani) watoe tamko rasmi bungeni. Naomba nisisitize hili maana watu wa bara wamekuwa kama watoto yatima huko Zanzibar mara makanisa yanachomwa moto, mara bar. Lakini sijawahi kumsikia mbunge yeyote toka Zanzibar akitoa kauli bungeni. Sasa tunataka kauli rasmi kupitia kwa wawakilishi wao bungeni. Narudia, kauli rasmi bungeni na hata kama wataongelea nje lakini bungeni lazima watoe kauli rasmi. vinginevyo nao wanaunga mkono haya maangamizi.

Tanzania Bara wapo wapemba wengi kuliko hata huko kwao Pemba!. Itakuwaje watu wa bara wakaamua kufanya fujo kama hizi?
 
To hell,watavuna wanachokipanda!tatizo nyani haoni kundule,wana mawazo mgando na maisha ya kukurupuka bila kutathmini ya mbelen!but just look before you leap!
 
watavuna wanachokipanda!...but just look before you leap!
Tanzania Bara kila wakiongelea Muungano hawaongelei upande wao, faida na hasara za Muungano kwao wao Bara, wanabaki kuongelea hasara watakazozipata Zanzibar Muungano ukivunjika. Mnawafanya kama Zanzibar vitoto vidogo na nyinyi ndio mnajua kinachowafaa Zanzibar. Why?

Kama Zanzibar ndio watakaoumia Muungano ukivunjika kwa nini Bara ndio tunaobembeleza?
 
Huu muungano haukuasisiwa na hao wenye maduka. Kwa nini watolewe kafara kwa maamuzi ya kisiasa ambayo hawana mamlaka nayo?

Bunge la muungano linaanza mwezi wa 7, nasubiri kwa hamu kumsikia Hamad Rashid pamoja na wabunge wote toka Zanzibar (bila kujali ni wa chama gani) watoe tamko rasmi bungeni. Naomba nisisitize hili maana watu wa bara wamekuwa kama watoto yatima huko Zanzibar mara makanisa yanachomwa moto, mara bar. Lakini sijawahi kumsikia mbunge yeyote toka Zanzibar akitoa kauli bungeni. Sasa tunataka kauli rasmi kupitia kwa wawakilishi wao bungeni. Narudia, kauli rasmi bungeni na hata kama wataongelea nje lakini bungeni lazima watoe kauli rasmi. vinginevyo nao wanaunga mkono haya maangamizi.

Tanzania Bara wapo wapemba wengi kuliko hata huko kwao Pemba!. Itakuwaje watu wa bara wakaamua kufanya fujo kama hizi?

Kwani nawe unaingia bungeni?, au umempata wa kumpa hii hoja akaulize?. Maana yasije yakaishia humu humu tu.
 
Back
Top Bottom