JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
JokaKuu,
Acha kungangania ya kale hapa Jamvini kumewekwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani ina details za kutosha kuhusu swali la mafuta.
Acha uvivu hivi unajua sheria za manunuzi? Huyo unayemtetea aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco William Mhando ni kihiyo mwenye elimu ya kuungaunga aliyoipata Huko Cuba katika Hali ya kutatanisha. Alifuta Zabuni nyingi kwa visingizio vya hovyo na kuwapatia mafisadi wake wakiongozwa na Rostam Aziz, Yusuf Manji na hayo makampuni ya kichina kununua Vifaa vyenye Kiwango cha chini na kujipatia mabilioni ya fedha na management yake Makao Makuu na Mikoani. Hata nguzo za miradi ya REA zinakaguliwa na Wapambe wa Mhando ni fake na umri wake hazitakaa zaidi ya miaka mitano. JokaKuu soma ,
Mokerema,
..nimeisoma hotuba ya Mnyika and basically haina jipya kuhusu hii sakata ya Tanesco vs Wizara.
..mimi nimependekeza TARATIBU na SHERIA zizingatiwe katika kushughulikia matatizo ya Tanesco.
..sidhani kama huo ni utetezi kwa Mhando, ukizingatia kwamba una ushahidi usio na shaka kwamba anahusika na ufisadi.
NB:
..achana na personal attacks.