Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

Status
Not open for further replies.
Kosa la Muhando liko wapi hapo sasa?

Kuna kifungu kwenye Sheria ya Manunuzi ya Umma kinakataza ofisi ya umma kufanya manunuzi kwenye kampuni ya mtumishi wa umma (wa ofisi hiyo) au mshirika wa mtumishi wa umma kwa suala la ushindanishi hapo haliingii kabisa. Ni kosa kifungu hiko kikiunganishwa na kifungu cha 31 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa cha matumizi mabaya ya madaraka.
 
Nimeattach hapa chini.
Sijui kama unazungumzia kipande hiki hapa au..
6) All members of the evaluation committee shall sign the Code of Ethics provided under the Regulations made under the Act,declaring that they do not have a conflict of interest in the procurement requirement.

Au kuna kipande kingine maana hapa naona kiapo tu cha hiyo evaluation committte na sii nani haruhusiwi kupewa kisheria..Hapa sioni kitu mkuu wangu tuna viapo toka kwa rais, bungeni, majaji sisi wenyewe tukisimamishwa kizimbani hii yote haina maana ikiwa kuna ruksa ktk kufanya jambo fulani maadam usikamatwe. Kuapa hakuna maana yoyote zaidi ya kumtakaza alokuwa ktk committee hii kuwa Yeye hana conflict of interest ndani ya kile kinachohitajika (procurement requirement). Wamesema specific member wa avaluation kutokuwa na conlfict of interest wapi...Nje ya hapo kama sina tugaje shi lolo ni mwendo mdundo..

Kifupi mkuu wangu mimi simtetei Mhando kwa lolote ila naitetea Tanesco siku zote. Sina haja ya kujua kafanya nini sijui tenda ya mkewe wakati tunaliwa mabillioni na hawa viongozi wetu kwa kupitia wizara zao. Nachosema mimi madudu ya Tanzania ni mengi sana, imefikia huwezi kumchambua kuku ukamla..Viongozi wetu wanasiasa ndio chanzo cha migogoro yote ya Tanesco na hatutaweza kumpima kiongozi yeyote kwa makosa yalotokana na Siasa. Hata mimi ukiniweka Tanesco nitatafuta kujijenga tu maana najua huwezi kuliokoa shirika hilo..

Halafu hii ni committe nzima haina mtu mmoja hivyo maadam tender sii yake yeye mtu mtu anaweza kukwepa kama Mkapa alivyokwepa uwajibikaji kwa sababu iliyosajiliwa ni Kampuni sio jina lake..Kampuni becomes a legal entity na pia yeye hakuwa ktk evaluation committe...Huu ujanja ujana wa Azimio la Zanzibar ndio nisoupenda. tupige marufuku kisheria kwa kuweka miiko na maadili wazi kwa kila mtu kufuata na sio kuweka vikao vya tume na kuwapa viapo wakati wanazidi kutumaliza... SHERIA ichukue mkondo wake.​
 
Kwa maelezo ya magazeti yetu ni vema unaposoma ujitahidi kukaa jirani na maziwa maana sumu ni nyingi unaweza kupandisha presha. na pili sioni kwa nini unamchukuliaa kuwa ni mhalifu kwa mtazamo wa wajasilimali (magazeti) hebu tumuone kama mtuhumiwa.

Usemayo ni sahihi....hata hivyo, pamoja na ukweli kwamba mara nyingi huwa stori za magazeti yetu huwa si za kuaminika; lakini ni ngumu sana kwa gazeti kama Raia Mwema lidai kwamba limeongea na Mhando wakati hawajaongea!! Si Raia Mwema.....hapa sina shaka yoyote kwamba ni kweli Raia Mwema limeongea na Mhando otherwise; tuhuma zilizotolewa na gazeti hilo ni nzito hivyo Mhando hana budi kukanusha suala la yeye kuongea na Raia Mwema!!

Na kwavile nipo convinced kwamba ni kweli Mhando ameongea na Raia Mwema; basi sina shaka kwamba ni Mhando mwenyewe aliyekiri kwamba Santa Clara Co. Ltd inaendeshwa na Mkewe!!! Alichokanusha Mhando ni kuambiwa hiyo kampuni ni "ya familia".....hili, Mhando amekanusha na amedai si ya familia bali ni "ya mkewe"!! Kwamba, kampuni ya familia ilishauzwa 2011 na kununulia na akina Veronica William, Fred William na mwenzao mmoja! Raia Mwema wameshasema wazi kwamba Fred na Veronica ni watoto wa Mhando....hapa William Mhando akanushe!!! Na kama nilivyoeleza kwenye post moja wapo; majina ya wakurugenzi wa kampuni hiyo ni pamoja na Fred William na Veronica William! Suala la wao kutumia majina mawili tu wala si la bahati mbaya, bali walitaka kuficha identity yao....kwamba ni Mhando Family...yaani ni upuuzi mtupu; ni sawa kujificha kwa mbuni-kichwa kichakani, kiwiliwili hadharani!!!
 
Kosa la Muhando liko wapi hapo sasa?

punguza upofu wa kuchambua hoja, ni kivipi kampuni ina mwaka na mtaji wa 10 mil ipewe zabuni ya 800 mil iweze kuwajibika ipasavyo?hapa hakuna kampuni zilizoshindanishwa, kuna utata na tashwishwi kubwa inaacha maswali mengi bila majibu.Pia hii hoja kuwa kampuni iliuzwa, haitoshi kuipa zabuni kubwa na nani anaweza kununua kampuni dhoofu namna hiyo , kwanini asisajiri yake mpya? , sababu mtaji si kigezo pekee, bali pia uzoefu na mizania mizuri.hapo mhando hawezi kukwepa kama kulikuwa na mgongano masilahi.Pia kusema mkewe alikuwa ni murugezi mtendaji tu kama mwajiriwa, haitoshi kutoa ushawishi aipndelee kampuni hiyo kupewa hiyo zabuni.hivyo ndugu yangu unaposoma hoja ,jaribu kuchambua mada/hoja kimakini.
 
Sijui kama unazungumzia kipande hiki hapa au..

Naam

Au kuna kipande kingine

For starters tuanze na hicho, ingawa vipo vingine no doubt.

maana hapa naona kiapo tu

Usiseme "kiapo tu", kuna kiapo cha declaration ya conflict of interest.Mhando aliapa hivi? Alisemaje kuhusu conflict of interest? Usikiminimize kiapo kwa kukiita "tu".Kitu kikubwa ethically hiki. Ni kiapo.

cha hiyo evaluation committte na sii nani haruhusiwi kupewa kisheria.

Hapa sijakupata, nani haruhusiwi kupewa sheria?

Hapa sioni kitu mkuu wangu tuna viapo toka kwa rais, bungeni, majaji sisi wenyewe tukisimamishwa kizimbani hii yote haina maana ikiwa kuna ruksa ktk kufanya jambo fulani maadam usikamatwe. Kuapa hakuna maana yoyote zaidi ya kumtakaza alokuwa ktk committee hii kuwa Yeye hana conflict of interest ndani ya kile kinachohitajika (procurement requirement). Wamesema specific member wa avaluation kutokuwa na conlfict of interest wapi...Nje ya hapo kama sina tugaje shi lolo ni mwendo mdundo..

Wananchi wenyewe tuna minimize checks za viapo vya ku declare conflict of interest, hao viongozi tutegemee wafanyeje?

Jibu swali, Muhando ali declare conflict of interest kama sheria inavyotaka?

Kifupi mkuu wangu mimi simtetei Mhando kwa lolote

But unamtetea Mhando kwamba hakufanya makosa bila hata kutuambia kwamba ka declare conflict of interest au la!

ila naitetea Tanesco siku zote.

Kwa lipi jema sana inalofanya? Mgawo wa umeme?

Sina haja ya kujua kafanya nini sijui tenda ya mkewe

Attitude kama hii ndiyo inayoendeleza impunity kwa viongozi, wananchi hawajali, sasa kwa nini viongozi waogope kuiba?

wakati tunaliwa mabillioni na hawa viongozi wetu kwa kupitia wizara zao.

Hata deal kama hizi mbili tu zinatuingiza katika mabilioni tayari, so what's the difference?

Nachosema mimi madudu ya Tanzania ni mengi sana,

Kama ni mengi sana that is even the more reason kutolea macho kila moja yayo, madogo kwa makubwa.Si kudharau impropriety inayo involve mamia ya mamilioni ya shilingi za umma.

imefikia huwezi kumchambua kuku ukamla.

Tunahitaji uchambuzi zaidi, sio kusema "huwezi kumchambua kuku ukamla" maendeleo yanataka kugangamala, usiogope challenges za kuendelea.

Viongozi wetu wanasiasa ndio chanzo cha migogoro yote ya Tanesco

Kwangu mie rushwa ni rushwa tu, whether kutoka kwa mwanasiasa au mtendaji. Milioni mia nane ikitafunwa ni milioni mia nane tu, huwezi kusema anayokula mwanasiasa ni zaidi ya anayokula mtendaji.

na hatutaweza kumpima kiongozi yeyote kwa makosa yalotokana na Siasa.

Makosa ni makosa tu, hizo habari za siasa or not ni excuses tu.Mhando ana kampuni ya familia yake anajichukulia zabuni kiulaini mnataka kumteteaje?

Hata mimi ukiniweka Tanesco nitatafuta kujijenga tu maana najua huwezi kuliokoa shirika hilo..

Ahaa, kumbe tatizo ndio liko hapa.Kiufupi wewe rushwa haikuumi kwa sababu unatokwa mate ukingojea zamu yako.

Halafu hii ni committe nzima haina mtu mmoja hivyo maadam tender sii yake yeye mtu mtu anaweza kukwepa kama Mkapa alivyokwepa uwajibikaji kwa sababu iliyosajiliwa ni Kampuni sio jina lake.

Yeye kama mtendaji wa TANESCO ali declare any conflict of interest?

Kampuni becomes a legal entity.

Na conflict of interest declaration is a legal requirement.

Huu ujanja ujana wa Azimio la Zanzibar ndio nisoupenda.

Hapana, unaupenda bwana.Sio wewe uliyesema unatokwa mate na hizi deals na ukipata nafasi utakula hivi hivi?

tupige marufuku kisheria

Tupige marufuku kisheria mara ngapi? Sheria ya procurement si hiyo, umeisoma? Huyu bwana ka declare conflict of interest kama sheria ianvyotaka?

kwa muweka miiko na maadili wazi kwa kila mtu na sio kuweka vikao vya tume na kuwapa viapo wakati wanazidi kutumaliza... SHERIA ichukue mkondo wake. [/LEFT]

Unakuwa apologist wa mafisadi tu, sheria ipo, unaifumbia macho.
 
Azimio La Zanzibar limetoa ruksa na mwanya kwa viongozi kufanya biashara.. hakuna kosa hata kama shirika hilo lingekuwa kla Mhando mwenyewe maadam amefuata masharti ya Tanesco. Na ndio maana Mkapa alifungua ofisi yake Ikulu kabisaaa isiwe taabu.. Hadi siku mtakapo badilisha sheria hizi sidhani kaa tunayokesi ya kujibu..

Usemayo Mkandara ni sawa kabisa.....hakuna dhambi yoyote kwa kiongozi ama awe wa umma au vinginevyo kufanya biashara....by the way, kama ulivyosema, tayari Azimio la Zanzibar lilishatoa baraka hiyo! Hata hivyo, ukitumia busara ya kawaida kabisa; isiyomuhitaji hata mwenye kuwa nayo kuwa na nyongeza ya shahada ya chuo kikuu ; utagundua kwambaMhando inaelekea alishajiandaa kuitumia nafasi yake kama MD ili kujinufaisha!! Kilichotokea ni matokeo tu ya mchakato ambao aliufanya hatua kwa hatua!

Ukiangalia maelezo yake, utagundua kwamba kampuni ya Santa Clara Co. Ltd ilikuwapo kabla hajawa MD wa TANESCO...na wakati huo ilikuwa ni kampuni ya familia! Na kwavile ilikuwa ni kampuni ya familia, basi sina shaka yoyote ile kwamba mmoja wa Directors wake alikuwa ni yeye mwenyewe!!

Baada ya Mhando kupata u-MD, akaona hiyo ndiyo fursa ya kujinufaisha kupitia kampuni yake. Lakini kwavile yeye mwenyewe alikuwa ni Director wa hiyo kampuni; akaona haitakuwa sahihi kuendelea kuwa mmoja wao na hapo bila shaka ndipo akapata wazo la kuwamilikisha(mwenyewe anaita waliuza) kampuni hiyo wanawe! Na kwavile alishafahamu malengo ya mchakato huo, ndipo bila shaka akaamua watoto hao wasitumie jina la ukoo (Mhando) katika usajili huo mpya (bila haikuwa usajili mpya, bali ni ama change of board of directors, or change of company name au vyote viwili kwa pamoja) na badala yake watumie tu jina la "William"! Hii alilenga kuficha kwamba kampuni hiyo ina mkono wake jambo ambalo lisingeleta picha mzuri wakati anataka kuitumia kampuni hiyo kujipa tender za TANESCO!!

Hivyo basi, ukiangalia mchakato huu, utaona wazi kwamba tayari Mhando alishakuwa na dhamira ya uhalifu kabla hata hajafanya hivyo!! Kama angekuwa mtu safi aliyekusuadia kufanya mambo kwa uwazi basi wala hakuwa na sababu ya kubadilisha umiliki wa kampuni na kama ilikuwa ni lazima afanye hivyo basi hakuwa na sababu za kuficha majina ya ukoo wa wamiliki...!! Majina ya Directors yangebaki ni "u-Mhando" wao lakini linapokuja suala la kuomba kazi TANESCO basi ana-declare interest in advance!!! Look here, wakati anapewa u-MD, akaambiwa inabidi mke wake aache kazi TANESCO kwa ajili ya kuogopa mgongano wa kimaslahi....hii ilitosha kabisa kuwa RED FLAG kwa Mhando kwamba jambo linalohusiana na mgongano wa kimaslahi lazima lizingatiwe....badala yake akaamua kwa makusudi kukwepa dhana ya conflict of interest kwa kuficha umiliki halisi wa kampuni yake!!
 
Usemayo ni sahihi....hata hivyo, pamoja na ukweli kwamba mara nyingi huwa stori za magazeti yetu huwa si za kuaminika; lakini ni ngumu sana kwa gazeti kama Raia Mwema lidai kwamba limeongea na Mhando wakati hawajaongea!! Si Raia Mwema.....hapa sina shaka yoyote kwamba ni kweli Raia Mwema limeongea na Mhando otherwise; tuhuma zilizotolewa na gazeti hilo ni nzito hivyo Mhando hana budi kukanusha suala la yeye kuongea na Raia Mwema!!

Na kwavile nipo convinced kwamba ni kweli Mhando ameongea na Raia Mwema; basi sina shaka kwamba ni Mhando mwenyewe aliyekiri kwamba Santa Clara Co. Ltd inaendeshwa na Mkewe!!! Alichokanusha Mhando ni kuambiwa hiyo kampuni ni "ya familia".....hili, Mhando amekanusha na amedai si ya familia bali ni "ya mkewe"!! Kwamba, kampuni ya familia ilishauzwa 2011 na kununulia na akina Veronica William, Fred William na mwenzao mmoja! Raia Mwema wameshasema wazi kwamba Fred na Veronica ni watoto wa Mhando....hapa William Mhando akanushe!!! Na kama nilivyoeleza kwenye post moja wapo; majina ya wakurugenzi wa kampuni hiyo ni pamoja na Fred William na Veronica William! Suala la wao kutumia majina mawili tu wala si la bahati mbaya, bali walitaka kuficha identity yao....kwamba ni Mhando Family...yaani ni upuuzi mtupu; ni sawa kujificha kwa mbuni-kichwa kichakani, kiwiliwili hadharani!!!
Mimi naomba hivi, kila kampuni nchini ionyeshe kina nani wenye tender na wamezipata vipi na nini uhsiano wao na viongozi wa pale.. Tupite kila wizara na idara hadi mashirika halafu tuone kama atabakia mtu.. Maana ukweli ni huu asilimi 80 ya mashirika yote yenye tender serikalini huwapatia watu wao na kwa kuwepo kwao committee hizi tutake tusitake. Ajira tu huwezi kupata bila kuwa na refa ndani ya humanresources halafu tumekuwa wepesi kutafuta mchawi mmoja tu. Hili Linchi limeoza jamani limeoza, linanuka rushwa, ufisadi na uchenzi wote..

Viongozi wote huwtafuta ndugu na jamaa wanaowaamini na kuwaanzia kampuni hii haina JK na Ridhwan, Mhando na Vero, Mwinyi na mkewe, mwanaye au mjukuu. Kama leo kwelitunatafuta ukweli nbasi tunaanza na Mhando halafu tunashuka chini kwa kila kiongozi halafu tuone ukweli upo wapi?..
 
Mimi naomba hivi, kila kampuni nchini ionyeshe kina nani wamiliki wake na tender zaop wanzipata wapi... maana ukweli ni huu asilimi 80 ya mashirika yote yenye tender serikalini hupata kutokana na watu wao kuwepo ktk committee tutake tusitake. Ajira tu huwezi kupata bila kuwa na refa halafu wepesi kutafutamchawi mmoja tu. Hili Linchi limeoza jamani limeoza, linanuka rushwa, ufisadi na uchenzi wote..

Viongozi wote huwtafuta ndugu na jamaa wanaowaamini na kuwaanzia kampuni hii haina JK na Ridhwan, Mhando na Vero, Mwinyi na mkewe, mwanaye au mjukuu. Kama leo kwelitunatafuta ukweli nbasi tunaanza na Mhando halafu tunashuka chini kwa kila kiongozi halafu tuone ukweli upo wapi?..

Kama nchi imeoza hivyo hiyo ni sababu tosha ya kuongeza scrutiny, sio kulegeza kamba.

Idea ya kufanya overhaul ya system nzima kuchunguza hizi deals si mbaya. Labda ndo tutatia adabu.
 
Mimi naomba hivi, kila kampuni nchini ionyeshe kina nani wenye tender na wamezipata vipi na nini uhsiano wao na viongozi wa pale.. Tupite kila wizara na idara hadi mashirika halafu tuone kama atabakia mtu.. Maana ukweli ni huu asilimi 80 ya mashirika yote yenye tender serikalini huwapatia watu wao na kwa kuwepo kwao committee hizi tutake tusitake. Ajira tu huwezi kupata bila kuwa na refa ndani ya humanresources halafu tumekuwa wepesi kutafuta mchawi mmoja tu. Hili Linchi limeoza jamani limeoza, linanuka rushwa, ufisadi na uchenzi wote..

Viongozi wote huwtafuta ndugu na jamaa wanaowaamini na kuwaanzia kampuni hii haina JK na Ridhwan, Mhando na Vero, Mwinyi na mkewe, mwanaye au mjukuu. Kama leo kwelitunatafuta ukweli nbasi tunaanza na Mhando halafu tunashuka chini kwa kila kiongozi halafu tuone ukweli upo wapi?..

What ru insinuating bro?! Let me guess, and correct me if am wrong....!! Kwamba, as far as hali yenyewe ndiyo hiyo basi tumwache Mhando tusimsakame simply because hiyo ndo halisi!!!
 
Kama nchi imeoza hivyo hiyo ni sababu tosha ya kuongeza scrutiny, sio kulegeza kamba.

Idea ya kufanya overhaul ya system nzima kuchunguza hizi deals si mbaya. Labda ndo tutatia adabu.
Maneno yako kweli lakini mkuu wangu, kwa mti ulooza unachimba shina lake na kukata mizizi, tena sisi hata hiyo mizizi unakoka moto na kuichoma kabisa kuhakikisha mti huo unakufa pasipo kuacha mbegu mbaya.

Kinachonishinda miye na kufikiri kwa Watanzania ni kwamba wanakata matawi makavu yalikauka hawa kina mhando wakifikiria yasije waangukia ilihali mti ulooza unaweza angusha nyumba nzima wakati wao wamelala ndani..
 
Mti uliooza ni CCM, JK na fikra nzima kwamba hatuwezi kuwa na ufanisi zaidi unaoendeshwa kwa kuwajibika zaidi kwa kila mmoja wetu.
 
What ru insinuating bro?! Let me guess, and correct me if am wrong....!! Kwamba, as far as hali yenyewe ndiyo hiyo basi tumwache Mhando tusimsakame simply because hiyo ndo halisi!!!
Noo sivyo hata kidogo isipokuwa Haramu yoyote inatakiwa iwe kwa watu wote kwa sababu ofisi zote za serikali tender wanapewa ndugu, marafiki na jamaa zao. Kosa la Mhando ni kosa vitabuni lakini ktk utekelezaji viongozi wote wanawapa tender jamaa zao hili sio swala la what am I insinuating - it's the fact.. Na sisemi Mhando achwe laa hasha lakini ni ujinga mtupu kwa sababu wanaomshitaki ndicho wao kinachowaweka mjini.. Hii ni sawa na ile hadithi ya Maria Magdalena ambayo kila mtu alitaka auawe kwa sababu ni Malaya kwa sababu Umalaya ni haramu.. Yesu akawaambia kati yenu aliye msafi awe wa kwanza kumpiga jiwe!..

Yesu hakuwa na maana Umalaya ni poa tu, ni wasafi au alimpongeza Maria kwa umalaya wake laa hasha... Lakini message ilikuwa very clear na rahisi kabisa. Mwanamke hawezi kuwa malaya pasipo kuwepo wanaume aliyetembea naye kwa fedha au vyovyote na kama hawa wanaume wana hakika Maria ni Malaya ina maana ni wao walilala naye... They were wrong and sinners as Maria mwenyewe.. Sijui kama umenielewa.
 
Noo sivyo hata kidogo isipokuwa Haramu yoyote inatakiwa iwe kwa watu wote kwa sababu ofisi zote za serikali tender wanapewa ndugu, marafiki na jamaa zao. Kosa la Mhando ni kosa vitabuni lakini ktk utekelezaji viongozi wote wanawapa tender jamaa zao hili sio swala la what am I insinuating - it's the fact.. Na sisemi Mhando achwe laa hasha lakini ni ujinga mtupu kwa sababu wanaomshitaki ndicho wao kinachowaweka mjini.. Hii ni sawa na ile hadithi ya Maria Magdalena ambayo kila mtu alitaka auawe kwa sababu ni Malaya kwa sababu Umalaya ni haramu.. Yesu akawaambia kati yenu aliye msafi awe wa kwanza kumpiga jiwe!..

Yesu hakuwa na maana Umalaya ni poa tu, wasafi au alimpongeza Maria kwa umalaya wake lakini message ilikuwa very clear na rahisi kabisa. Mwanamke hawezi kuwa malaya pasipo kuwepo wanaume aliyetembea naye kwa fedha au vyovyote na kama hawa wanaume wana hakika Maria ni Malaya ina maana ni wao walilala naye... They were wrong and sinners as Maria mwenyewe.. Sijui kama umenielewa.

Nimekuelewa kwa 101%......ur concern is ow clear!!! Labda tu nishindilie msumari kwa kusema kwamba as far as Mhando ndo tushampata basi tuanze na huyu huyu na tusimpe nafasi ya kupumua!!! Panapotokea majambazi watano wameenda kufanya uhalifu, kisha wakakurupushwa na wananchi wenye hasira; basi atayevishwa tairi la gari na kupigwa moto ni yule aliyeshindwa kukimbia na badala yake akaangukia mikononi mwa wananchi! Wale wanne waliokula kona, nao siku yao ipo!!! Sina shaka yoyote kwamba, Mhando ameangukiwa na jumba bovu; lakini kwavile ni mwenyewe ndie alicheza michezo ya hatari barazani mwa gofu basi hata akifilia mbali ni haki yake.
 
Lakini lazima uelewe kinahcofanyika mkuu wangu. Unamwondoa Mhando ili nimweke Mkandara ambaye nataka kumpa deal ndugu yangu ambaye anakubaliana/kutokubaliana na bajeti ya wizara ya nishati na madini ambayo kuna washikaji/ maadui fulani na fulani in the process of Ufisadism...

Kwa hiyo wewe macho yako kwa Mhando na Tanesco, wenzako wanatazama vilivyomo ndani ya bajeti kuna ulaji gani, vizuizi gani, kina nani watakuwa wadeni wa Tanesco ktk tender, uzalishaji wa kampuni hii yenye matumizi kuliko mapato..Think large bro.. usipigwe changa la macho!
 
Lakini lazima uelewe kinahcofanyika mkuu wangu. Unamwondoa Mhando ili nimweke Mkandara ambaye nataka kumpa deal ndugu yangu ambaye anakubaliana/kutokubaliana na bajeti ya wizara ya nishati na madini ambayo kuna washikaji/ maadui fulani na fulani in the process of Ufisadism...

Kwa hiyo wewe macho yako kwa Mhando na Tanesco, wenzako wanatazama vilivyomo ndani ya bajeti kuna ulaji gani, vizuizi gani, kina nani watakuwa wadeni wa Tanesco ktk tender, uzalishaji wa kampuni yenye matumizi kuliko mapato..Think large bro.. usipigwe changa la macho!

Upo sahihi kabisa!! Lakini kwavile bado haijathibitika kwamba Maswi (Katibu Mkuu) anamuondoa Mhando kwa ajili ya maslahi yake (yeye Maswi) basi hukumu iliyopo mbele ya Pilato na ambayo inapaswa kutolewa hukumu ni hii ya Mhando!! Na ingawa Maswi anatuhumiwa kuibeba Puma Energy; uzuri ni kwamba Maswi ametoa utetezi unaoonesha kwamba inagawje anaibeba kampuni hiyo lakini anafanya hivyo kwa manufaa ya taifa....utetezi wake una mashiko!!! Utetezi wa Mhando, at least katika suala hili unaonekana ni uetetezi usio na mashiko yoyote na ambao huwezi kuzani kwamba unatolewa na Injinia Msomi! Si kwamba hajui jinsi ya kujitetea, bali ni kwavile hana grounds za kujitetea na ku-prove kwamba he's innocent na yanayofayika ni hujuma tu dhidi yake!
 
kuibeba Puma energy ni kwa maslahi ya Taifa? Mimi naweza jenga hoja ya maana kwa nini tunaihitaji IPTL
au Dowans kwa manufaa ya Taifa..Nothing new mkuu wangu toka Maswi, mhando, waliopita hadi Ngereja na wengineo kote kumeoza .. wazungu wanasema kata mti panda mti...
 
Mkuu wangu wangu hebu nipe busara ya haya mambo haya.....kuhusu kampuni mbili; Kampuni X na Puma Energy! Kampuni X ndiyo ilipewa tenda ya kuiuzia mafuta mazito TANESCO. Hata hivyo, kampuni X inaenda kununua mafuta Puma Energy kwa bei ya chini na kisha kwenda kuyauza kwa TANESCO kwa bei ya juu! Hata hivyo, kampuni X ilishindanishwa kwenye tenda ya uzaji mafuta na Puma Energy! Hata hivyo, bodi ya TANESCO ikaona Puma Energy haina vigezo na hivyo kutoa tenda hiyo kwa kampuni X ambayo ilikuwa inanunua mafuta kwa hao hao Puma Energy! Alichofanya Katibu Mkuu Maswi, ni kusimamisha hiyo tenda ya kampuni na kuwapatia Puma Energy ambao wanauza mafuta kwa bei ya chini kwa TANESCO kuliko ilivyokuwa awali! Huo ndio utetezi wa Maswi.....sasa Mhando na wenzake wakanushe madai haya ya Maswi! Na kama yanayosemwa na Maswi ni sahihi, ni kwanini basi nisione amefanya hivyo kwa maslahi ya taifa?! Kosa lililofanyw na Maswi ni kuipa tenda kampuni ambayo ilishindwa kwenye ushindani....sasa ni nini basi kilicho bora kwa Mtanzania wa kawaida kama mimi kati ya kuuzuiwa mafuta kwa bei ya juu kutoka kwa kampuni ambayo ilishinda tenda (kihalali!?) au kuuziwa mafuta kwa bei ya chini toka kwa kampuni ambayo haikushinda tenda?! Nisaidie mkuu wangu! Kwangu nitabaki na dhana kwamba Maswi alichukuwa uamuzi wenye maslahi kwa taifa hadi pale itapoelezwa kwamba madai ya Maswi ni uongo!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom