Elections 2010 Madiwani Arusha kuanza vikao kwa mvutano

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Madiwani Arusha kuanza vikao kwa mvutano


Na Omari Moyo, Arusha

KIKAO kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kinaanza tayari kuunda Kamati za kudumu za halmashauri, huku kambi ya
upinzani ikisema hawatakubali hadi nafasi ya naibu meya ijazwe.

Akizungumza mji hapa jana Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw. Estomih Chang’a amlisema kwamba tofauti kati ya madiwani wa CHADEMA na halmashauri zimemalizika kupitia semina elekezi iliyofanyika Februari 6 na 7, mwaka huu.

Alisema kuwa katika semina hiyo, yalizungumzwa mambo mengi muhimu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, na kukubaliana na mambo ya msingi na kwamba kikao cha madiwani cha leo ni cha kuunda kamati za kudumu za halmashauri.

Mkurugenzi Chang’a alisema kwamba, katika uundwaji wa kamati hizo utashirikisha madiwani wa pande zote, ili kamati hizo ziwe na nguvu na kuleta ufanisi wa kiutendaji kwa ajili ya maendeleo ya mji wa Arusha.

“Hiki ni kikao cha baraza la madiwani cha kuchagua kamati za kudumu za halmashauri..ambazo ni lazima ziteuliwe kabla ya kuanza kwa baraza la madiwani hivi karibuni,â€� alisema Chang’a.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Bw. Estomiah Mallah (CHADEMA) alisema kwamba watahudhuria kikao hicho bila na kusikiliza hoja zitakazotolewa ila hawatakubaliana na ajenda yeyote mpaka atakapochaguliwa naibu meya.

Bw. Mallah alisema kwamba haiwezekani kuteuliwa kwa kamati za kudumu za halmashauri wakati nafasi ya naibu meya ipo wazi, na kwamba ijazwe kwanza ndiyo shughuli hiyo iendelee.

“Hatuwezi kukubaliana na lolote kuhusiana na kuteuliwa kwa kamati hizo, mpaka nafasi ya unaibu itakapojazwa..na hilo ndilo jambo la msingi,â€� alisema Bw. Mallah.

Aliyekuwa Naibu Meya wa Jiji hilo, Bw. Michael Kivuyo alijiuzulu kutokana na mgogoro wa umeya unaondelea mjini hapa.

 
PHP:
Akizungumza mji hapa jana Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw. Estomih Chang’a amlisema kwamba tofauti kati ya madiwani wa CHADEMA na halmashauri zimemalizika kupitia semina elekezi iliyofanyika Februari 6 na 7, mwaka huu.
 
Alisema kuwa katika semina hiyo, yalizungumzwa mambo mengi muhimu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, na kukubaliana na mambo ya msingi na kwamba kikao cha madiwani cha leo ni cha kuunda kamati za kudumu za halmashauri.
 
Mkurugenzi Chang’a alisema kwamba, katika uundwaji wa kamati hizo utashirikisha madiwani wa pande zote, ili kamati hizo ziwe na nguvu na kuleta ufanisi wa kiutendaji kwa ajili ya maendeleo ya mji wa Arusha.

Hivi semina kweli yaweza kumaliza tofauti zilizopo au ni kujidanganya tu..........................
 
CHADEMA wamtia matatani Meya Arusha


na Grace Macha, Arusha


amka2.gif
MVUTANO juu ya uhalali wa taratibu zilizomuweka madarakani Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo (CCM) umechukua sura mpya baada ya madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kumpa siku 30 Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Estomih Chang'a, kutoa taarifa na vielelezo vya wajumbe walioshiriki mkutano wa kwanza wa kawaida vinginevyo watamburuza mahakamani.
Madiwani wa CHADEMA waliyasema hayo jana walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya City Link wakiwa na viongozi wao wa wilaya na mkoa wakibainisha kuwa tayari wameshamuandikia mkurugenzi huyo barua kupitia mwanasheria wao, Albert Msando tangu Januari 31 , mwaka huu.
Msando alisema amefikia hatua hiyo baada ya wateja wake kupinga maelezo kuwa walihudhuria kwenye mkutano huo huku akiambatanisha nakala ya majina ya madiwani waliohudhuria mikutano hiyo ambapo hakuna majina ya madiwani wa CHADEMA.
Kwa mujibu wa barua ya wakili huyo ambayo Tanzania Daima inayo nakala yake, endapo jambo hilo halitatekelezwa watawashitaki mkurugenzi pamoja na halmashauri ili kupitia mahakama waweze kutoa nakala halisi ya mahudhurio ya wajumbe siku ya Desemba 17 na 18 , 2010 pamoja na kupata tafsiri ya muongozo juu ya ni wakati gani mkutano wa kwanza wa kawaida wa halmashauri hiyo ulifunguliwa.
Pia watataka kupata muongozo ni wakati gani idadi ya wajumbe walifikisha akidi ili kuwezesha mkutano huo uanze kwa mujibu wa sheria pamoja na uhalali wa kuendelea kwa mkutano bila akidi hiyo kufikiwa.
Wakili Msando katika barua hiyo anaeleza kuwa mkutano huo maalumu haukuanza wala haukufunguliwa kama ilivyo kawaida ya mikutano hiyo, jambo alilomtaka mkurugenzi kuthibitisha endapo ulifanyika kwa kile alichosema kuwa mkutano huo usingeweza kuanza mpaka pale madiwani wanapokuwa wamekwisha kula kiapo.
 
Back
Top Bottom