Karibuni kwenye chama cha wanywa juisi!!
Ungemalizia..wanywa juice za asili.
Karibuni kwenye chama cha wanywa juisi!!
Sijui kati ya RED BULL an Coca cola/Pepsi nani ana madhara zaidi. Hizi nazo zinakwangua kila kitu tumboni. Inasemekana hata kutu zinasafisha
Uncle, bora hata na wewe umesema hili.
Tulikua tunafufua gari ya zamani home, kuna bolt zilikua ngumu kufunguka kutokana na kutu.
Basi nikashangaa yule fundi anaagiza soda aina ya Pepsi - akamwagia ile bolt. Binafsi nikashangaa, nikamuuliza kanini anamwagia Pepsi na sio breke fluid kama wengi tulivyozoea?
Akananiambia "Subiri, we utaona!" Kusema kweli ile bolt ilifunguka!
Nimekuwa mwoga hata wa kunywa Pepsi, since that day nakunywa Fanta and Stoney Tangawizi... lol
......lakini bora hivi vinywaji tunaviona na twaweza kuchukua hatua kirahisi hasa kuwaelimisha watoto wetu.
Mimi tatizo langu ni hili la hawa wadudu wa HIV/AIDS ambao siwaoni na wako ktk sehemu muhimu ktk maisha yangu sijui nifanye vipi. Mtoto mlembo unamuona (kama hujaoa lakini), ukimtazama usoni ...ah.... unakosa kuamini. Kondomu, tunaambiwa ni nzuri lakini nilienda mexico mwaka 2006 ktk purukushani mtaani nikaambiwa ...ah... wewe vipi? au ndo umenipandikiza ukimwi.....mimi ni salama kaka.....jisikie huru....hii ni mexico.....mzee kama mende vile....sasa mimi nashindwa hata kujua nitakwepa lipi na nitaangamizwa na lipi.
Wadau wote hapa jamvini,ahsanteni kwa hilo angalizo.Ila nafikiri la msingi ni kwa kila mmoja wetu kusambaza huu ujumbe kwa watu wengi zaidi na mamlaka husika na mada kama hii hapa TZ.yaani red bull na redds zote hazifai.