SoC02 Madhara yatokanayo na shughuli za kilimo karibu na mto

Stories of Change - 2022 Competition

Anold Mlay

New Member
Aug 30, 2022
1
0
MAZARA YATOKANAYO NA SHUGHULI ZA KILIMO KARIBU NA MTO

Shughuli za Kilimo katika nchi zinazoendelea ni kama uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hizo. Shughuli za kilimo katika nchi mbali mbali hufanyika karibu na vyanzo vya maji ili kurahisisha upatikanaji wa maji, ambayo hutumika hususani katika kipindi cha umwagiliaji wa mazao. Ufanyikaji wa shughuli za kilimo karibu na vyanzo vya maji hususani mito bila kuzingatia utunzaji wa vyanzo vya maji husabisha maadhara na athari mbalimbali katika chanzo husika cha maji. Madhara haya husababishwa na sababu mbali mbali,mojawapo ikiwa ni utumiaji wa tekinolojiajia duni kipindi cha usafirishaji wa maji kutoka kwenye mto kwenda kwenye maeneo ya kilimo, sababu ya pili ni kutozingangatia sheria za mazingira inaosema34. Bila kuathiri kifungu cha 57 cha Usimamizi wa Mazingira Sheria, Waziri anaweza, kwa amri iliyochapishwa kwenye Gazeti la Serikali, kukataza shughuli za kibinadamu zitakazofanywa zaidi ya mita sitini kutoka kwenye bomba la maji au hifadhi au chanzo cha maji. ” Sheria hii inazuia ufanyikaji wa shughuli zozote za kibinadamu mita sitini(60) pembezoni mwa mto au chanzo chochote cha maji kutokana na athari ambazo zinasababishwa na shughuli za kibinadamu katika chanzo husika. Ukiukwai wa sheria hii, hupelekea watu kufanya shughuli za kilimo pembezoni mwa mto na kusababisha athari mbalimbali katika mto mfano mzuri Picha 1 inaonyesha ufanyikaji wa shughuli za kilimo pembezoni mwa mto Ngerengere unao patikana Tanzania,mkoa wa Morogoro katika eneo la kata ya Mazimbu.

20220830_135329.jpeg


Picha 1: SHUGHULI ZA KILIMO PEMBEZONI MWA MTO NGERENGERE

Mmomonyoko wa udongo katika kingo za mto ni moja ya athari inayo chochewa na ufanyikaji wa shughuli za kilimo karibu na mto hususani kipindi cha kuandaa eneo la kilimo(shamba) kwaajili ya kupanda mazao. Matumizi ya vifaa vya kilimo kama trekta na jembe la mkono kwaajili ya kulimia huchochea mmomonyoko wa udongo kwa kiwango kikubwa. Picha 2 hapo chini inaonyesha mmomonyoko wa udongo katika kingo za mto Ngerengere unaopatikana katika mkoa wa Morogoro kata ya Mazimbu, kulingana na shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali kinacho endelea pembezoni mwa mto huo.

20220830_135541.jpeg


Picha 2: MMOMONYOKO WA UDONGO KATIKA ENEO LA MTO NGERENGERE KUTOKANA NA SHUGHULI ZA KILIMO

Mmomonyoko wa udongo katika kingo za mto husababisha kupungua kwa kina cha mto na hivyo kupelekea mto kujaa na kufurika kipindi maji yanavyo kuwa mengi hususani kipindi cha mvua kubwa na hivyo kusambaa katika makazi ya watu na kuleta adhari kama mafuriko katika makazi ya watu. Katika kata ya Mazimbu mtaa wa Mazimbu Darajani ambako mto Ngerengere unapita, eneo la mtaa huo unao onekana kwenye Picha 3 huadhiriwa na mafuriko yanayo sababishwa na kufurika kwa mto Ngerengere kutokana na kupungua kwa kina cha mto huo ambako hupelekea kujaa kwa urahisi na hatimaye maji kuacha mkondo wake na kusambaa kwenye makazi ya watu wa mtaa wa Mazimbu darajani.

20220830_140152.jpeg

Picha 3: ENEO LA MTAA WA MAZIMBU DARAJANI AMBALO HUATHIRIWA NA MAFURIKO YANAYO TOKANA NA KUFURIKA KWA MTO NGERENGERE KIPINDI CHA MVUA KUBWA.

Shughuli hizi za kilimo huusisha pia utumiai wa mbolea za viwandani kwaajili ya kukuzia mazao Pamoja na viwatilifu kwaajili ya kuulia wadudu waharibifu wa mazao shambani. Athari a kwanza ya Mbolea na Viwatilifu huwa na kemikali ambazo huathiri viumbe hai waishio majini(mto), athari hizo ni kama kupungua kwa kasi ya kuzaliana ya viumbe hao na pia kupotea kabisa kwa viumbe hao. Athari ya pili ni uchafuzi ambao hupelekea kupungua kwa ubora na usafi wa maji yam to kwaajili ya matumizi mbalimbali katika jamii hii husababisha madhara kwa jamii ambazo zinategemea chanzo husika cha maji kwaajili ya shughuli mbalimbali za majumbani.

Mazara yatokanayo na shughuli za kilimo karibu na mto ni makubwa sana na yanahitaji jamii kubadilika na kuweka umakini katika swala hili ili kuhakikisha tunakuwa na maendeleo endelevu katika jamii yetu kwa kuhakikisha utunzaji wa mito yetu kama chanzo muhimu cha maji katika jamii zetu.Umakini huu utaongezeka kupitia asasi zinazo husika na usimamizi wa mazingira na utekelezwaji wa sheria mbali mbalimbali za utunzaji wa mazingira,pia utoaji wa elimu kwa jamii husika hususani kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira na madhara yanayo sababishwa na baadhi shughuli mbali mbali za kibinanadamu hususani kilimo karibu na mto ili jamii iweze kuelewa na kubadilika.
 
Back
Top Bottom