Pilipili ina madhara yoyote mwilini?

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Mimi ni mtumiaji mzuri sana wa pilipili. Kila nipatapo chakula basi huwa nahakikisha pilipili haikosekani. Je eti matumizi ya pilipili nyingi yana madhara yoyote mwilini?

Wataalamu wa afya na lishe nipeni ushauri.
 
Nliskia (sina uhakika) yawezasababisha vidonda vya tumbo in a long run japo hata mi napenda kula pia.

Labda wahindi watupe data maana nasikia wanatengeneza mpaka juice ya pilipili.
 
Nahisi ingekuwa na madhara, wahindi na wachina wote wangeshakufa.
 
Mimi ni mtumiaji mzuri sana wa pilipili. Kila nipatapo chakula basi huwa nahakikisha pilipili haikosekani. Je eti matumizi ya pilipili nyingi yana madhara yoyote mwilini? Wataalamu wa afya na lishe nipeni ushauri.
Faida ya Afya ya Kula Pilipili

Japokuwa Pili pili inaliwa na watu wa jamii mbali mbali duniani, faida na Afya ya kula pilipili wengi hawazijui au hazijulikani na watu wengi.

Kwenye pilipili kuna kemikali iitwayo Capsaicin, ambayo ndio inayo sababisha muwasho na joto la pilipili.

Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu:
Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari. Hii ni kwa mujibu wa timu ya watafiti katika Chuo Kikuu cha Tasmania, utafiti iliyochapishwa katika American Journal of Clinical Nutrition, mwezi Julai 2006.

Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.

Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili

Pilipili usaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi!

Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye tumbo (Stomach Cancer)

Pilipili usaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.

Kula pilipili usaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu.


Pilipili said:
* Red chillies are very high in Vitamin C and pro Vitamin A.

* Chili peppers rates high in the content of Vitamin B, especially Vitamin B6.

* Chilies are a high storehouse in potassium, magnesium and iron, while they are low in sodium content.

* They are also high in protein content, and an excellent source of fiber.

* Chilies are known to prevent the formation of blood clots, and have the property to break down existing clots.

* The consumption of chillies triggers the release of ‘feel good' endorphins, which result the ‘good' attitude towards general well being.

* The use of chillies in the diet increases the breakdown of carbohydrates during rest periods.

* It also contributes in the reduction of obesity as it increases metabolism and helps to burn the calories faster, including the burning of fats.

* Chillies lower the risk of diabetes, and scientific research has shown that regular intake of chillies could improve insulin control by over 55%.

* Eating chillies is known to help in alleviating pain in arthritis as it helps to reduce the inflammation.

* Chillies help in easing the nasal congestion conditions, and are thus effective as a cure for sinus. This is because the ‘hotness' in the chillies help to dislodge the mucus layer lining the nasal cavity.

Cubanelle_Peppers.jpg

 
wana JF naomba mnieleweshe, hivi kula sana pilipili kuna madhara? na kama yapo ni yapi?
 
Ukiondoa tatizo kwa wenye vidonda vya tumbo, Ukizidisha sana utapatwa muwasho mbaya sehemu ya haja kubwa wakati wa kujisaida.
 
Pilipili haina madhara kabisa na isitoshe ukiwa na madhara inakujulisha, hii pilipili ni "early warning system" kwa ugonjwa wowote tulionao mwilini. Mfano, ukila pili ikakuwaka moto tumboni, basi ujuwe una matatizo humo tumboni. Ukila pilipili ikakuwasha kwenye matokeo ya haja, ujuwe kuna athari huko ulipowashwa, ni hivyo hivyo kwa mengine.

Zaidi ya hayo kuna mada ilitolewa humu (kama sikosei na xpaster) kuhusu faida za pilipili. Nna uhakika kuwa pilipili haina madhara bali ina faida kubwa sana kwenye mwili wetu.

Kwa kusema hayo. Naomba ieleweke kuwa "too much of anything is harmful", hata dawa za kutibu ukizitumia isivyopaswa zitakudhuru na hii ni hata kwa pilipili na kingine chochote kile, itumie pilipili kwa raha na si kwa karaha.

Kuna raha zaidi ya kuwashwa?
 
Pilipili haina madhara kabisa na isitoshe ukiwa na madhara inakujulisha, hii pilipili ni "early warning system" kwa ugonjwa wowote tulionao mwilini. Mfano, ukila pili ikakuwaka moto tumboni, basi ujuwe una matatizo humo tumboni. Ukila pilipili ikakuwasha kwenye matokeo ya haja, ujuwe kuna athari huko ulipowashwa, ni hivyo hivyo kwa mengine. Zaidi ya hayo kuna mada ilitolewa humu (kama sikosei na xpaster) kuhusu faida za pilipili. Nna uhakika kuwa pilipili haina madhara bali ina faida kubwa sana kwenye mwili wetu. Kwa kusema hayo. Naomba ieleweke kuwa "too much of anything is harmful", hata dawa za kutibu ukizitumia isivyopaswa zitakudhuru na hii ni hata kwa pilipili na kingine chochote kile, itumie pilipili kwa raha na si kwa karaha. Kuna raha zaidi ya kuwashwa?
ahsante kwa maelezo mkuu.
 
Hakika hakuna raha zaidi ya kuwashwa...!
Faida ya kula pilipili kwanza ina virutubisho,pili huongeza mapigo ya moyo kwa muda hii huipa mazoezi,tatu huongeza kasi ya kuzunguka damu mwilini,nne kama alivyosema mdau hapo juu hukueleza matatizo mwilini ukiona mdomo,koo,tumbo,haja kubwa/ndogo zinawaka ujue hapo kuna tatizo na sio pilipili,nne husaidia kuleta hamu ya kula chakula na pia hamu ya kujamiiana.
 
Mi na pilipili dam dam, Bora nikose mboga ila pilipili iwepo.
We uporoto hayo ya kweli? Hasa hilo la mwisho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom