Madhara ya kutafuna mchele mbichi/udongo

Nitafute kwa muda wako hiyo ni sababu ya upungufu wa madini. Mwenzako alikuwa anatafuna kilo 1 mchele mbichi amepona kwa msaada wangu. Unique.

Sasa Mkuu kama unaweza kunisaidia kwa kupitia humu humu ndani na wengine wakafaidi matibabu hayo ingependeza zaidi. Nataka kuacha kabisa kutafuna mchele.

Please.
 
Nina dada yangu mmoja ana mimba ya miezi mitatu lakini huyu dada ni tofauti na hawa ambao nimewazoea (wanaokula ndimu na vitu vichachu) yeye hupenda kula unga wa mahindi au kutafuna sana mchele. Kwa siku humaliza hata kilo moja (makadirio).

Siku za mwanzoni nilihisi labda huwa anahisi njaa na ndo maana anafanya hivi lakini katika chunguza yangu hata akimaliza tu kula chakula baada ya nusu saa huingia jikoni na kuanza kutafuta mchele ili autafune, hivyo mama ana kazi ya ziada ya kuuficha mchele ingawa muda mwingine yupo radhi kununua kakilo ka moja ka unga/mchele ili awe comfortable.

Hali ya kupenda kula vitu hivi nahisi ina madhara hata kwa mtoto aliye tumboni, naomba ushauri wenu jinsi ya kuacha hii tabia manake naona anakoelekea si kuzuri hata kidogo
 
jamani mimi nina katabia ya kula mchele mbichi, yaani hii kitu nafanya mara kwa mara sometimes naweza kula hata nusu kikombe cha chai kilichojaa mchele. I just like something cruchy and the smell of it.

Naomba mnijulishe madhara na vipi naweza kuepukana nao.
 
Mchele hufanya tumbo kupata kazi kubwa sana kufanya mmengenyo (digestion) ambapo kunaweza sababisha constipation ambayo humbata na maumivu ya tumbo . Pia huenda unatatizo la bulimia jaribu kujichunguza utibu hilo tatizo naimani utaacha tu kula mchele.
 
kula mchele kunaweza kukakusababishia upate constipation, minyoo na magonjwa mengi yasababishwayo na minyoo kama vile amoebiasis na ascariasis hivyo inabidi ujitahidi kuacha kula mchele.
 
Nina tatizo moja kubwa wadau.Mimi sio mjamzito lakini huwa natafuna sana mchele mbichi nimeshajaribu kuacha lakini nashindwa kabisa. Naomba ufafanuzi wa sababu,madhara na tiba ya tatizo hili.Asanteni
 
Sina ujauzito l;akini nimekuwa na mazoea ya kutafuna sana mchekle mbichi.Nini sababu,madhara na matibabu yake?
 
Sina ujauzito lakini nina mazoea ya kutafuna mchele mbichi kwa saana.Naomba kujulishwa chanzo/sababu,madhara na tiba ya hili.
 
Wadau hebu tusaidiane kwenye hili,kuna dada mmoja hapa napofanyia kazi anapenda sana kutafuna mchele ikafikia stage akawa anaweka kwenye pochi na anatafuna siku nzima, sasa dada mwingine naye kadakia anatafuna balaa, mwanzoni nilidhani wana ujauzito lakini nikagundua kuwa hawana ila wanatafuna mchele mpaka inaogopesha, sasa kwa anayejua hakuna madhara yoyote kutokana na hii tabia ili niwa-caution waachane nayo mapema kabla hawajdhurika?
 
Inasemekana madhara yanayoweza kupatikana kwa kula mchele ni kama madhara yanayotokana na kula vitu kama mchanga..
 
Hello JF,

Namshukuru M/Mungu kwa pumzi isio na kipimo anayotujalia cku hadi cku..anaefahamu sababu ya kula udongo na mchele mbichi..na madhara yake plz anifahamishe!!

NB: Mtumiaji sio mama mjamzito!!!
 
Back
Top Bottom