Madhara ya kutafuna mchele mbichi/udongo

Ozee

Member
May 11, 2011
31
1
Jamani, naomba mnisaidie kama kuna mwenye kufahamu madhara ya kutafuna mchele mbichi na jinsi ya kuacha kuutafuna..
 
1. jinsi ya kuacha ni kuamua kuacha kula.
2. madhara ni kwamba unapotafuna kuna uwezekano usitafune punje zote au hautatafuna wote so vile vipunje vinakuwa kama vimawe na vitajitunza kwenye appendix kama vimawe, kuna hatari appendix ikajaa na ukatakiwa ufanyiwe upasuaji.
punguza then acha, pika ule mpunga bana
 
Binafsi nimeshafanyiwa hiyo operation ya appendix kama miaka mitano iliyopita ila sikuwa na tabia ya kula mchele.

cha ajabu kuanzia mwaka jana nimeanza hii tabia ya kupenda kutafuna mchele najitahidi kuacha naweza nikavumilia siku mbili tatu lakini nikipita karibu na ulipo mchele nikasikia ile harufu basi lazima nitauchokonoa nitafune na nninapotafuna najisikia raha. ila mpaka naogopo sasa ninachofanya najitahidi kununua karanga nakaanga naweka ndani, nakaanga bisi naweka ndani ili nikisikia ile hamu ya kutafuna mchele basi nichukue bisi au karanga au matunda nitafune ile nipotezee ile hamu ingawa wakati mwingine bado vinanishinda nitajikuta tu nimechukua mchele hata kido nikatafuna.

Nilimuuliza mtu mmoja akaniambia kuwa nini upungufu wa starch hivyo nijitahidi kula starch kwa wingi hasa ugali wa mhogo. aliniambia madhara ya mchele ni pamoja na kupata appendix au vile vichembechembe pia vinaweza kusababisha matatizo ya koo. nafikiri wataalamu akina Njiwa, Mzizi mkavu, Riwa na wengineo watatusaidia.
 
Mchele mbichi si mzuri jamani hasa kwa wanawake kwani husababisha ute mzito ukeni.hivyo hufanya mwanamke asiwe na radha.
 
Kuna kipindi nlikua nakula zaidi ya vikombe viwili au hata vitatu kwa siku...kazi kuuloweka tu.Ila siku hizi ni mara moja moja sana nikiwa napika wakati wa kuosha naacha funda moja kwenye maji...
 
Eating raw rice may be a form of a disorder called pica. Pica is an appetite for non-foods (e.g., paper, coal, chalk etc.) or an abnormal appetite for some things that may be considered foods, such as food ingredients (e.g., fllour, raw potato, raw rice, starch). Exposure to infectious agents via ingestion of contaminated rice is a potential health hazard associated with pica, particularly if the rice is unwashed. It is usually indicative of some form of underlying nutritional deficiency. A doctor can evaluate and perhaps start a dose of vitamin or mineral supplements. Pica is a also a habit which would require psychologic counselling or aversion therapy for a cure of the behavioural disturbance. This is not an inherited problem, but it can often be learned by a child from a mother.

Read more at:Is eating raw rice a harmful habit? » DoctorNDTV Queries
 
madhara ni kwamba unapotafuna kuna uwezekano usitafune punje zote au hautatafuna wote so vile vipunje vinakuwa kama vimawe na vitajitunza kwenye appendix kama vimawe, kuna hatari appendix ikajaa na ukatakiwa ufanyiwe upasuaji.
punguza then acha, pika ule mpunga bana

Mkuu sidhani kama appendicitis inakuwa caused na kula mchele mbichi, 99% ya huo mchele na mawe yatakuwa passed out kwenye stool...

angalia extract ya cause of appendicitis

The causes of appendicitis are not well understood, but it is believed to occur as a result of one or more of these factors: an obstruction within the appendix, the development of an ulceration (an abnormal change in tissue accompanied by the death of cells) within the appendix, and the invasion of bacteria. Under these conditions, bacteria may multiply within the appendix.

The appendix may become swollen and filled with pus (a fluid formed in infected tissue, consisting of while blood cells and cellular debris), and may eventually rupture. Signs of rupture include the presence of symptoms for more than 24 hours, a fever, a high white blood cell count, and a fast heart rate. Very rarely, the inflammation and symptoms of appendicitis may disappear but recur again later.

In most cases, a blockage inside the appendix probably starts a process in which the appendix becomes inflamed and infected. If inflammation continues without treatment, the appendix can rupture. A ruptured appendix spills bacteria-laden intestinal contents into the abdominal cavity, causing peritonitis, which may result in a life-threatening infection. A rupture also may cause an abscess (a pus-filled pocket of infection) to form. In a woman, the ovaries and fallopian tubes may become infected, and the resulting blockage of the fallopian tubes may cause infertility. A ruptured appendix also may allow bacteria to infect the bloodstream - a life-threatening condition called sepsis
 
Habari ya Maandalizi ya Sikukuu ya Eid El Fitr!

Naomba msaada wenu, maana hapa ndipo mahali sahihi pa kuuliza na kujibiwa majibu yanayostahili na yenye msaada.
Mimi ni mwanamke, nina shida moja, ninapenda sana kuloweka mchele kwenye kikombe na kutafuna hata robo kilo kwa siku. Nimejitahidi kuacha lakini nimeshindwa, huwa naweza kuacha kutafuna kwa siku mbili kisha nikarudia tena. Hivi karibuni nilisafiri nje ya nchi, na katika tembeatembea kwenye mall nikaukuta mchele mweusi tiii (black rice) nikaununua nikawanaloweka kwenye maji na kutafuna. Hata nikikuta pepeta, nazo siachi nachukua na kutafuna. Izingatiwe kuwa sina ujauzito wala nini. Na hata nilipokuwa mjamzito sikuutamani hata kuuona. Ajabu!!

Naomba msaada Wanajamii mnisaidie mambo yafuatayo:-

1. Madhara ya kutafuna mchele uliolowekwa
2. Jinsi ya kuacha kutafuna
3. Faida yake (kama zipo).
 
Habari ya Maandalizi ya Sikukuu ya Eid Naomba msaada wenu, maana hapa ndipo mahali sahihi pa kuuliza na kujibiwa majibu yanayostahili na yenye msaada. Mimi ni mwanamke, nina shida moja, ninapenda sana kuloweka mchele kwenye kikombe na kutafuna hata robo kilo kwa siku.

Nimejitahidi kuacha lakini nimeshindwa, huwa naweza kuacha kutafuna kwa siku mbili kisha nikarudia tena. Hivi karibuni nilisafiri nje ya nchi, na katika tembeatembea kwenye mall nikaukuta mchele mweusi tiii (black rice) nikaununua nikawa naloweka kwenye maji na kutafuna. Hata nikikuta pepeta, nazo siachi nachukua na kutafuna.

Izingatiwe kuwa sina ujauzito wala nini. Na hata nilipokuwa mjamzito sikuutamani hata kuuona. Ajabu!! Naomba msaada Wanajamii mnisaidie mambo yafuatayo:-

1. Madhara ya kutafuna mchele uliolowekwa

2.Jinsi ya kuacha kutafuna

3. Faida yake (kama zipo).
 
Ukiamua kuacha utaacha. I was just like you; na nimeacha kwa kuwa nimeamua. Ila sidhani kama kuna madhara labda kama mchele una mchanga.
 
Ukitaka kuacha anza kupunguza kiasi cha mchele unaokula kwa siku kidogo kidogo hadi ambapo utafanikiwa kuacha
 
Mwombe mtu uliye karibu naye awe anakutegeshea mchanga au kokoto kwenye kikombe unacholowekea!! Mwelezee nia yako na time unazopenda kutafuna, ili awe anakuvizia na kukutegeshea mchanga na kokotoa. Ikiwezekana kiroba kizima cha mchele aki-contaminate na kokoto!!

Njia hii, kama nyinginezo yaweza kufanya kazi iwapo unania ya kuacha. Maana kuna jamaa yetu mmoja alikuwa anapenda kutafuna kucha kwa saana tu bila mafanikio ya kuacha, ila alituomba kama kuna mbinu tunayoifahamu ya kuweza kumsaidia na tufanye hivyo. Basi, watu tukaamua kufanya kweli... Jamaa alipokuwa amelala, tulipaka vidole vyake vyote na kinyesi cha bata! Tukamshtua jamaa toka usingizini, na kama ilivyo kawaida yake akasogeza dole gumba la kushoto mdomoni, lakini akashtuka kuona tumeliwekea plaster, hivyo hakulitia mdomoni moja kwa moja. Tukamwambia abandue plaster, kubandua akakutana na kinyesi cha bata. Na tulifanya hivyo kwa vidole vyake vyote alivyopendelea kula kucha. Prank ikawa imefanya kazi, maana mpaka leo hii jamaa hatafuni kucha tena!!
 
Nitafute kwa muda wako hiyo ni sababu ya upungufu wa madini. Mwenzako alikuwa anatafuna kilo 1 mchele mbichi amepona kwa msaada wangu. Unique.
 
Fanya hivi chukua :- mchele 6kg sukari 3kg roweka naa tumia mchanganyiko kuanzia alfajir 5:00, 10:00, 01:00, 04:00, 8:00, onyo usitumie maji, wa chakula kingine. Tumia dozi hii kwa siku 7. Ukimaliza dozi hutakaa uguse mchele tena
 
Back
Top Bottom