maneka
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 823
- 1,176
Wadau awali ya yote niwatakie heri ya mwaka mpya 2021! Mungu azidi kutubariki na kutuongezea neema na baraka zake, uwe mwaka wa mafanikio kwa wana JF wote na familia zetu.
Wadau, nawiwa kumwangukia Mh. Rais wetu mtetezi wa wanyonge, asiyependa kuona manunguniko ya watu wake, mpenda haki na mcha Mungu. Kumuomba huruma kwa watumishi, kuwa ile nyongeza ya kamshahara ka kila mwaka kana maana kubwa sana kwa mtumishi asikapuuze maisha ya wengi yalibebwa na kanyongeza hako alikoona hakana maana.
Kama haitoshi MADARAJA ya watumishi kuanzia 2014 yamekwama, watumishi hawana furaha kabisa sema tu ni ile ukiwa mbele ya mwenye mamlaka unajichekesha kinafiki, uhalisia ni kwamba nyoyo za watumishi walio wengi zinavuja machozi ya huzuni, simanzi, manung'uniko, kisasi, majuto nk! Kwa hiyo Mh. Rais binafsi kwa ujasiri nilionao unaotokana na haya ninayosema kupitia hapa ningetamani nije personally nikueleze ili uone uzito wa kulitekeleza hili haraka ili kukumbusha usemi wako "maendeleo hayana chama, si ndiyo ndugu zangu!"
Mh. Rais nakuomba wambie wabunge waanze upya kujadili sheria inayo halarisha chama cha walimu (CWT). Hiki ni jini linalo nyonya damu ya walimu wa Tanzania. Kama kweli chama kina msaada kwa walimu, kura ya maoni ipigwe ili walimu waeleze kwa kura ya siri kama kina manufaa kwao au ni genge la wanyonyaji. Hadi inafikiriwa eti serikali yako inaweza kuwa nyuma ya dhuruma hii ya makato yasiyo eleweka yanakwenda wapi na faida ya nani? Kwa nini serikali inahusishwa ni kwa sababu kila walimu wanapolalamika juhudi hainekani kuungwa mkono na serikali yako!!!!?? Sasa sheria ipitiwe upya.
Mh. Rais, wastaafu ni kundi lingine linaloonekana kupuuzwa kwa kutopewa mafao kwa wakati. Hali inayopelekea matapeli kuwadhurumu kwa kupitia mgongo wa kuwasaidia pindi wanapo kaa muda mrefu bila mshahara. Na inasemekana baadhi ya watumishi wasio waaminifu huchwlewesha mafao ya watumishi hao ili kuandaa mwanya wa kuwatapeli mafao yao. Hili nakuomba sana Mh. Rais ilitazame kwa jicho la huruma sana na haraka sana. Wazee wetu wametumikia Nchi hii kwa muda mrefu tena kwa uaminifu na Uzalendo wa hali ya juu sana, si vema wakaadhirika kiasi hiki tunacho shuhudia.
Yapo mengi ila kwa leo 01.01.2021. niishie hapa, kama utanikaribisha IKULU au kwenye kale kaofisi kako uliko tumia kuwasiliana na Mkulu mwenzio kwa simu siku chache za mwishoni mwa mwaka jana, nitakueleza mengi.
Kabla ya kunikaribisha nisaidie haya kwanza ili tuanze vizuri mwaka mpya 2021.
Wale wazee wa kuponda kila wazo la mtu subirini pembeni kwanza Uzi wenu nauandaa, kiherehere sipendi. MIMI HUWA SIJARIBIWI. HIIIIIIII!
HERI YA MWAKA MPYA MH. RAIS.