Madaktari waliofukuzwa waula Namibia, Botswana, Rwanda na A.Kusini

MKL

Senior Member
Mar 2, 2012
126
77
Balozi za nchi hizo tajwa zimetoa ofa nono kwa madoctor woote waliofutiwa lesseni na wizara ya afya na TZ kwa ngazi zoote kuanzia seniors hadi intern, Intern wataandikishwa kama intern pindi wakifika kwenye nchi husika chini ya uangalizi wa Senior Doctors huku wakipewa mishahara na marupurupu yakuwatosha na wakimaliza shule wanapewa vyeti na lesseni za udoctor wa nchi walipo.

Wale masenior ambao wamenyangánywa lesseni wao wakifika wanaandikishwa kwenye chama cha madoctors wa nchi husika na kupewa lesseni mara moja na kupangiwa kazi ikiambatana na haki zoote wanazostahili.

Balozi za nchi hizi zinawaomba madocta woote wajiandikishe tayari kuajiriwa kwenye nchi watakazo kati ya hizo tajwa.
haya sasa kwa mara ingine tena TZ inaelekea kupoteza Brain zake kwa kile kinachoitwa mgomo ili hali walipa kodi wanateseka kwa kukosa watabibu.

Masini nchi yangu itatuchukua muda gani kuwapata madoctor kama hawa tena kama kweli wakiitikia mwito wa nchi hizi na wakaondoka.....?

Source: Raia Mwema Leo 18/07/2012 page 3
 
Ilionekana kama utani na masihara, bila kusahau maamuzi ya jeuri na vitisho, lakini impact yake ni kwa sisi wananchi wenyewe......Haya nendeni bwana, manake sisi kama sisi hatuna jinsi ya kuwazuia.
 
Kwanini daa tuwafutie ubalozi woote watakaowaiba madr wetu!
 
One day we will be matured enough to make decisions wisely. Kwasababu wengi hatukujua extent ya ubaya wa maamuzi tunayoyafanya pengine tulidharau uwezo na umuhimu wa madaktari.
 
Nabii siku zote hatambuliki kwao. Sioni sababu ya serikali kuamua kutunishiana misuli na watendaji wake. Serikali inaogopa pale itakapokubaliana na madaktari, basi walimu, wazee, trl, na wengine wataidai serikali. Kama serikali yc ccm ndio inachotaka basi itakipata soon
 
"Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri. Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo." (JK et al., 2012)
 
Bora waende wakafie mbele sasa kama walikuwa na hiyo option kwanini walikuwa wanagoma? si wangeacha kazi kimya kimya wakaenda huko kwenye mafano manono?
Uzalendo huwa unauma sana, usifikiri wote wanafurahi kwenda huko. Ni ujinga wetu. Sasa na sisi tukachukue wa Africa kusini tuwalete.

RIP CCM
 
bora waende wakafie mbele sasa kama walikuwa na hiyo option kwanini walikuwa wanagoma? Si wangeacha kazi kimya kimya wakaenda huko kwenye mafano manono?

labda watajitetea kuwa walitaka watusaidie sisi ndugu zao!
 
Ni kiburi tu cha wanasiasa; wanafikiria udaktari ni "kama fani nyingine" tu. Gharama ya madaktari wetu kuondoka ni kurudisha huduma ya afya kwa miaka kadhaa nyuma. Lakini kwa vile tatizo lenyewe halijashughulikiwa bado kutakuwa na mgongano wa madaktari na serikali in the future. Hii yote ni matokeo ya sera zilizoshindwa za CCM.
 
Porojo hizi sasa zinakera. Ndugu wengine tunafanyakazi kwenye mojawapo ya balozi ulizotaja. Acha uongo, si tabia nzuri!
 
"kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri. Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo." (jk et al., 2012)

mkuu! Jk aliongea kwa hasila si wakumsikiliza sana tuangalie kanchi ketu kenyewe haka matatizo ni mengi tumsaidie jk!
 
Back
Top Bottom