Madaktari Ocean Road watoa tamko kuunga mkono Mgomo; Waweka vifaa chini

mayoscissors

JF-Expert Member
Nov 24, 2009
975
471
Baada ya kikao cha madaktari wanaofanya kazi katika taasisi ya saratani ya ocean kuhusu mgomo unaoendelea wa madaktari kote nchini, tumeazimia mambo yafuatayo:

1. Sababu za mgomo wa madaktari ni za msingi.
2. Maamuzi na majibu ya serikali hayatoshelezi,hayaridhishi na hayakidhi mahitaji ya madaktari.
3. Kutokana na haya tajwa hapo juu,sisi madaktari wa ocean road tunaungana na madaktari wote nchini kusitisha utoaji huduma mpaka hapo ufumbuzi utakapopatikana.

Tunawaomba radhi sana wagonjwa wetu wapendwa kwa usumbufu utakaojitokeza katika kipindi hiki cha mpito. Ni matarajio yetu kuwa huduma zitakuwa BORA ZAIDI baada ya kipindi hiki kigumu.

Wenu katika utumishi wa umma,
MADAKTARI WA OCEAN ROAD.
08/03/2012
 
Tumewasikia tutakuja Aga Khan Hospital au Regency Hospital. si ndio mnataka hivyo.
 
kabla ya kwenda kukutana na wazee wa gerezani kesho, jk apeleke w.akw.ere ocean road kupiga mionzi wagonjwa wa kansa...sijawahi ona serikali ya mafirauni kama hii!
 
Jamani hii inasikitisha sana, imagine mgonjwa wa saratani anaposoma habari hii. Pinda do something.
 
Wana bahati mimi siyo Rais walahi ningewakomesha..

JK ana huruma na uvumilivu uliozidi kweli aise JK una hekima sana.
 
badala ya kushughulikia tatizo kwa kuongea na madaktari wao wanabaki kusambaza propaganda kwa wananchi kitu ambacho kinachochea mgomo zaidi
 
Wana bahati mimi siyo Rais walahi ningewakomesha..

JK ana huruma na uvumilivu uliozidi kweli aise JK una hekima sana.
eti walahi ...ungefanya nini unadhani wale ni wakwea nazi wa bagamoyo kuwa utapata wengine kesho..
 
Wana bahati mimi siyo Rais walahi ningewakomesha..

JK ana huruma na uvumilivu uliozidi kweli aise JK una hekima sana.
Mtu akiwa zoba unamsifu ana hekima! Nadhani si ajabu nawe waweza kuwa zoba kama yeye.
 
Baada ya kikao cha madaktari wanaofanya kazi katika taasisi ya saratani ya ocean kuhusu mgomo unaoendelea wa madaktari kote nchini,tumeadhimia mambo yafuatayo:
1. Sababu za mgomo wa madaktari ni za msingi.
2. Maamuzi na majibu ya serikali hayatoshelezi,hayaridhishi na hayakidhi mahitaji ya madaktari.
3. Kutokana na haya tajwa hapo juu,sisi madaktari wa ocean road tunaungana na madaktari wote nchini kusitisha utoaji huduma mpaka hapo ufumbuzi utakapopatikana.

Tunawaomba radhi sana wagonjwa wetu wapendwa kwa usumbufu utakaojitokeza katika kipindi hiki cha mpito. Ni matarajio yetu kuwa huduma zitakuwa BORA ZAIDI baada ya kipindi hiki kigumu.

Wenu katika utumishi wa umma,
MADAKTARI WA OCEAN ROAD.
08/03/2012

Asante kwa taarifa,mtatukuta ahera.mmesoma kwa kodi zetu sasa mmetusaliti
 
tatizo si madaktari tatizo ni wananchi sisi hatuna mkataba na madaktari bali tunamkataba na serikali ambayo ndio tumeiweka madarakani hivyo basi tunatakiwa tuwaambie serikali wahakikishe tunapata huduma ya afya pasipo kujua kuwa madaktari wamegoma au lah....hatuna mkataba na madaktari bali tunamkataba na serikali wakishindwa kutoa huduma ni wakati wa kuiwajibisha
 
Back
Top Bottom