Madaktari Ocean Road watoa tamko kuunga mkono Mgomo; Waweka vifaa chini

ukweli ni kwamba watendaji wamechoka kuburuzwa na politicians, madockta mmelianzisha, maticha tuko njia moja,
 
Wana bahati mimi siyo Rais walahi ningewakomesha..

JK ana huruma na uvumilivu uliozidi kweli aise JK una hekima sana.

Ungewafanya nini Mkuu? Malizia basi post yalo iwe na maana! Au ndio wale wale, "Serikali ipo kwenye Mchakato?"
 
Hongereeni, tupo pamoja na wala msikate tamaa na msiogope vitisho. Hata wana wa Israel kabla ya kuiridhi nchi ya Kanan, waliipata pale Misri.
 
Wana bahati mimi siyo Rais walahi ningewakomesha..

JK ana huruma na uvumilivu uliozidi kweli aise JK una hekima sana.

Hilo la uvumilivu wasema wewe na wewe ndiwe walijua tu ila kwetu ni uzembe, ujinga na upumbavu usiovumilika hata kidogo
kwakuacha suala kama hili kuwa sugu namna hii na sasa inatutesa waTZ
 
kwa mtu wenye akili ndogo kama mimi nafikia kuona kinyume nyume kwamba ni kama kosa ni serikali kukaa meza moja na hawa jamaa wauaji meza moja wakati wa mgomo wa kwanza. Wamemshika baba yao sharubu na sasa wanataka kuzikata Jk angesimama kidete angefukuza wote hawa liwalo na liwe haina tofauti na wakigoma bado wagonjwa wanakufa sawa tu na kuwafukuza
 
Nawapongeza sana madaktari kwa msimamo wao kuna watu humu wanalichukulia jambo hili kisiasa na kimzaha badala ya kutafuta suluhu wanasema fukuza eti wakome serikali italeta toka India, wanafikiri India ni kwenda kuwachota kama maji. Tunajionea kadri serikali inavyowatisha madaktari na kuwabeza ndivyo hospitali zingine zinavyozidi kujiunga na Kikwete kesho asipotumia busara akifuata baadhi ya mawazo potofu ya watu ya kishabiki atazidi kutia petrol kwenye moto.
 
Tunawaomba radhi sana wagonjwa wetu wapendwa kwa usumbufu utakaojitokeza katika kipindi hiki cha mpito. Ni matarajio yetu kuwa huduma zitakuwa BORA ZAIDI baada ya kipindi hiki kigumu.
Safari hii hakitakuwa kipindi cha mpito, nyie ndo mtapita...mnakera sana.
 
Kama viongozi wetu wameshindwa kutimiza wajibu wao na ndo tulitegemea wawe mstari wa mbele kutuongoza ktk kuikomboa Tz sasa wamekuwa mstari wa mbele kutuangamiza
 
Madaktari hawana haki ya kumshinikiza Rais kumwachisha kazi waziri asiye na tuhuma yoyote.

Hawa madaktari wachukuliwe hatua kali sana iwe fundisho, hao interns wote waliogoma wafukuzwe na hao madaktari wote wafukuzwe haraka sana, hata kusikilizwa wasisikilizwe, na serikali ihakikishe hata wakiondoka nje ya Tanzania, wasipate kazi huko.
 
kwa mtu wenye akili ndogo kama mimi nafikia kuona kinyume nyume kwamba ni kama kosa ni serikali kukaa meza moja na hawa jamaa wauaji meza moja wakati wa mgomo wa kwanza. Wamemshika baba yao sharubu na sasa wanataka kuzikata Jk angesimama kidete angefukuza wote hawa liwalo na liwe haina tofauti na wakigoma bado wagonjwa wanakufa sawa tu na kuwafukuza

kweli wewe ni mama porojo!!!,,, akinenacho mtu ndicho kinachomtokea, kama ulivoamua kujiita mama porojo, na kweli unamwaga porojo
 
Madaktari hawana haki ya kumshinikiza Rais kumwachisha kazi waziri asiye na tuhuma yoyote.

Hawa madaktari wachukuliwe hatua kali sana iwe fundisho, hao interns wote waliogoma wafukuzwe na hao madaktari wote wafukuzwe haraka sana, hata kusikilizwa wasisikilizwe, na serikali ihakikishe hata wakiondoka nje ya Tanzania, wasipate kazi huko.

wafukuzwe and then what!!!???? Way foward!!!????
 
hii ni wazi kwamba wasomi wa tanzania wanawasaliti wasiosoma.
Anyekusaliti ni raisi wako uliyemchagua kwa kipande cha kanga. Hili liwe somo kwetu kuchagua viongozi wanaoweza kututetea. Madaktari wnagoma anaacha kuongea nao anaongea na wazee wa Dar.Stupid nnon sense
 
sawa ninyi mnaona mungu mjinga kuwapa hicho kipaji coz mnawatesa sana wagonjwa hebu fikiria kama mama ako au baba ako yupo ocean road je ungegoma?hebu fikirien mnapoteza.watanzania wangapi? I hate all doctors
 
Tunaomba wagonjwa katika hospitali za serikali wahamishiwe hospitali binafsi kwa vile ndiko walikoelekezwa kupewa huduma na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam maana naye ni kama waziri wa afya pia. Umbumbumbu huu ni hatari, wagonjwa wanaelekizwa pa kutibiwa na mkuu wa mkoa...Tanzania yetu hii!!!
 
Madaktari hawana haki ya kumshinikiza Rais kumwachisha kazi waziri asiye na tuhuma yoyote.

Hawa madaktari wachukuliwe hatua kali sana iwe fundisho, hao interns wote waliogoma wafukuzwe na hao madaktari wote wafukuzwe haraka sana, hata kusikilizwa wasisikilizwe, na serikali ihakikishe hata wakiondoka nje ya Tanzania, wasipate kazi huko.
Kwa hiyo rais ana haki kuwalazimisha madaktari kufanyakazi.
 
Kikwete ana changamoto kubwa zaidi ya uongozi wake wakati huu kuliko wakati mwingine wowote ule. Akicheza vibaya tu historia itamhukumu vikali sana. Kwa kuangalia kwa hara tu tunaweza kuona kuwa inclination ya watu wa serikali ni Rais kuja na msimamo mkali kama ule wa mbayuwayu. Msimamoj ambao wengi - mashabiki wa serikali - wangependa kuuona ni Rais anawapiga mkwara wa ngugu na hata kuwatimua madaktari wote na kuzungumza kwa ukali kuwa "serikali haiwezi kulazimishwa" na hivyo akatoa masaa machache kwa madaktari wote kurudi kazini au watafukuzwa kazi na "kufutiwa leseni" na hata chama chao "kufutwa". Huu utakuwa ni msimamo utakowafanya watu wapige makofi na kushangalia rais kuwa kaonesha ukali na uongozi.

Hata hivyo utakuwa ni msimamo mbaya zaidi kwa sababu unategemea kama madaktari wataogopa na kufyata. Hilo ndilo tarajio lenyewe.

Kwa sababu kama madaktari watamgomea Rais, na kusema kuwa hawatishiki basi mgomo utaendelea na hapo Ikulu itabidi ijioneshe haiadhiriki na kuwafukuza kazi madaktari wote na kutangaza kazi. Well hapo ndio kosa kubwa zaidi litakuwa limetokea!

Manesi nao watagoma kuuonesha mshikamano na wananchi watazidi kulipigia mgongano huu. Mwisho wa siku LAZIMA SERIKALI ITAKAA CHINI NA MADAKTARI!

Lakini, kama Kikwete atalalamika sana kesho na kuonesha kuonewea na madaktari na kukumbushia uongozi wa nyuma ulivyofanyiwa na kuwa yeye anaonewa na akalia na kunung'unika (ili kupata simanzi) lakini mwisho akasema kwa uchungu na masikitiko kuwa serikali imekubali kujiuzulu kwa dr mponda na dr nkya ili kuokoa maisha ya wananchi zaidi atakuwa amejidhoofisha lakini atakuwa amejipa nguvu vile vile. Atakuwa amejidhoofisha kwa sababu sasa hatoweza tena kuwabeba viongozi wanaolalamikiwa lakini atakuwa amejipa nguvu kwa sababu viongozi wabovu watajua kuwa watatoswa wakilalamikiwa!
 
Back
Top Bottom