Madaktari kuuza damu kwa wagonjwa mahututi ni ubinadamu?

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,974
785
Damu ya kuongeza wagonjwa mahututi inauzwa ingawa kanuni ya tiba inakataza kufanya hivyo kwani hata wanaojitolea damu hawauzi damu yao kwa hospitali husika. Benki ya damu ni kwa ajili ya dharura lakini ukifika na mgonjwa madaktari watakuambia lipa mathalan elfu 50,000 ili mgonjwa wako aongezewe damu kama huna fedha unatakiwa kwenda kutafuta ndugu na jamaa wa kujitolea damu hata kama ipo lakini wakati huo mgonjwa kabakiza muda wa nusu saa damu itakwisha mwilini na asipopata damu daktari anakuambia atakufa. Ukitoa fedha damu inaletwa mara moja.


My take: - mazingira ya kugoma kwa maelezo kwamba serikali iboreshe mazingira ya kazi ni kweli?

- Kama wanaojitolea damu bure wangekuwa wanauza bei yake ingekuwa ya juu kupita kiasi
tusingeiweza wengi na tungekufa.

- Je mazingira bora ya kazi ni tiketi ya pekee ya mgonjwa kupata huduma bora?
Je huduma bora ni vifaa vya kazi pekee au inaambatana na roho ya daktari na muuguzi?
 
Ndugu yangu alikufa kwa kukosa fedha ya kulipia damu Muhimbili sitasahau siku hiyo, tulimtuma ndugu mmoja kwenda kuchukua fedha akachelea lakini mgonjwa wetu alikufa tukimwangalia.
 
wakubali wasikubali ukweli unabaki kuwa udaktari ni wito!
kinachotusumbua kwa sasa ni kwamba madaktari wengi wameitikia au wamekubali kufanya kazi ya udaktari kama sehemu ya mshahara hawana mawazo ya msaada na roho za watu
mbaya zaidi kila sehemu wana siasa wameingia na kutuharibia mpango mzima wa maisha yetu
fikiria kinachowagomesha kwa sasa ni siasa na si maslahi tena. tunaelewa vizuri kuwa wanatumiwa ili yatokee lakini ipo siku anayetuchumia shida hizi mungu atamuumbua nafsi yangu inaumia mno sina uwezo ila tukaze buti
 
kuna baadhi ya madaktari hawana utu hata kidogo japo wengi tunasahau huduma mbovu waliowahi kutupa sisi wenyewe, ndugu au rafiki.
 
MOI walimnyima mgonjwa wangu aliyeumia kwenye ajali kumfunga chuma (supporter) linalotakiwa ku-balance miguu kwenye kitanda hadi nilipotoa 20,000 walianza kwa kusema vyuma vimekwisha kama nataka wanifanyie maarifa niwape 20,000. Nilipotoa wakaweka chuma.
 
Damu ya kuongeza wagonjwa mahututi inauzwa ingawa kanuni ya tiba inakataza kufanya hivyo kwani hata wanaojitolea damu hawauzi damu yao kwa hospitali husika. Benki ya damu ni kwa ajili ya dharura lakini ukifika na mgonjwa madaktari watakuambia lipa mathalan elfu 50,000 ili mgonjwa wako aongezewe damu kama huna fedha unatakiwa kwenda kutafuta ndugu na jamaa wa kujitolea damu hata kama ipo lakini wakati huo mgonjwa kabakiza muda wa nusu saa damu itakwisha mwilini na asipopata damu daktari anakuambia atakufa. Ukitoa fedha damu inaletwa mara moja.


My take: - mazingira ya kugoma kwa maelezo kwamba serikali iboreshe mazingira ya kazi ni kweli?

- Kama wanaojitolea damu bure wangekuwa wanauza bei yake ingekuwa ya juu kupita kiasi
tusingeiweza wengi na tungekufa.

- Je mazingira bora ya kazi ni tiketi ya pekee ya mgonjwa kupata huduma bora?
Je huduma bora ni vifaa vya kazi pekee au inaambatana na roho ya daktari na muuguzi?

Mkuu unajua Madaktari wa sasa wanafikiri kwamba taaluma hiyo sasa ni ya kuabudiwa. Siyo damu pekee mkuu, hata dawa utaambiwa haipo na kuelekezwa maduka ya kununua yanayomikiwa na hao Madaktari. Hivi tukisema mazingira mabaya wanayajenga wao wenyewe tutakosea? Wauze damu, wahamishe madawa na vifaa vingine bado wanadai mazingira mazuri yapi hayo?
 
Madaktari ni wasanii hali yao ni bora kuliko sekta nyingi serikalini lakini wengi wetu tunatawaliwa na ajenda za kisiasa katika kuunga au kupinga mgomo wao
 
Ndugu yangu alikufa kwa kukosa fedha ya kulipia damu Muhimbili sitasahau siku hiyo, tulimtuma ndugu mmoja kwenda kuchukua fedha akachelea lakini mgonjwa wetu alikufa tukimwangalia.

Usifikiri uamuzi wa baadhi wale wenye uwezo wao wanapoamua kupeleka wagonjwa wao India ni kwamba tatizo ni Serikali, Madaktari wetu ni noma, hata mimi mgonjwa wangu wa kisukari alitaka kufia Amana kisa siwezi kwenda nae wodini kabla hajaandikisha , mpaka wananchi wenye hasira kali walipoamua kumvaa Daktari mmoja aliyekuwa karibu.
Mimi ningefurahi kama hao waliogoma wangefutiliwa mbali kabisa.
 
Hivi ukiambiwa kumtolea ndugu yako damu kwa nini iwe shida? Ni mambo mangapi serikali wanasema ni bure wakati watu wanalipia. Si tulisikia madaktari wakimwambia Pinda siku waliyokutana nao pale muhimbili kuwa serikali inajidai huduma bure wakati wakienda hospitali wanaambiwa wabebe cloves zao, syringe zao na madawa yao. Mnawasingizia hao madaktari kwa kuwa wao ndio wanaoonana ana kwa ana na wagonjwa hivyo kubebeshwa lawama. Sasa wamesema LAWAMA BASI, mnahangaika!

Kama kweli ulienda hospitali ukatozwa rushwa ni wajibu wako kuripoti na kumuwajibisha aliyekutoza rushwa ( Sasa unataka madaktari wawasaidie kugoma kwa sababu wanatoza rushwa). Fanya sehemu yako ya wajibu kuwawajibisha wala rushwa wote na wote wasio na tija kwa Tanzania.
 
Tatizo tunaelekeza lawama ndipo sipo. Hii yote ni kutokana na kutokuwa na regulations nzuri ambapo lawama zote ziende kwa serikali. Sehemu zote haya mambo yapo sana tu TRA, Bank, kila sehemu you mention them. Ni kwa sababu inapotokea kwenye afya ambapo tunaamini ndipo kwenye maslahi makubwa kwenye maisha ya binadamu tunashangaa. Serikali imeenda wapi? haiyaoni haya mambo?

Kama mtu katuibia billioni 42 mchana kweupe na serikali imeuchuna leo unalalamika kunyimwa damu! Imefika mahali kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake, tusilalamike kabisa maana yale mambo ya msingi serikali haiwekezi ila kwenye usaniii ndio kunakowekezwa pesa. Tutakufa kwa ujinga wetu na tutaishia kulalamika tu maisha yetu yote huku tukiangamia mmoja baada ya mwingine.
 
Ni ukuku.

Kuku bwana wana nidhamu. Unajua hawa Madaktari sasa wamevua taaluma zao sasa sijui tuwape majina gani. Sijui wanapoulizwa wanafanyakazi wanadiriki kusema ni Madaktari. Wanaharakati wanatekeleza majukumu yao kupitia migongo yao , Wanasiasa halikadhalika, wao je nini jukumu lao?
 
serikali haijui kwamba inapambana na vichaa walioamua kuua

Kama sisi ni VICHAA na kweli mioyoni mnaamini hivyo...mnatutaka wa nini basi? Mbona tukigoma mnachonga chonga? Tangu lini mtu akajali kichaa anapogoma?

Na by the way, kwa nini tuitwe vichaa and all other stupid names tunapogoma?! Kwqa nini tusipogoma mnakuja kwetu kutaka uduma kama sisi ni vichaa?!

Nawashangaa kweli waTanzania...bila aibu mnakasirikia na kuchukia maDaktari, kuwatukana, kuwasengenya...huku mwenye kosa (serikali) akipiga miluzi ya fedheha kwa 'ujuha' wenu kwani anajua hamuwezi mfanya chochote! mnaishia kutibu dalili wakati ugonjwa wenyewe mnaendelea kuulea. Shame on you wote mlio na fikra duni kama hizo hapo juu!
 
Madaktari wetu ni wakatili aisee ukishaingia kwenye himaya yao lazima wakutoe upepo. Na hili sio swala la malipo ni swala la ethics kwa sababu naamini wanajua situation kwenye sekta ya afya kabla hawajaingia huko.
 
Wengi wa mliochangia uzi huu wa madaktari kuuza damu mnaonekana ni watu wa serekalini, kwa kweli inanisikitisha sana na hapo ndio ninaamini kwamba serekalini kuna watu wenye uwezo mdogo wa kutatua matatizo zaidi ya majungu, unafiki, ushirikina nk, ambayo ndio yametufikisha kwenye umaskini huu na kadhia la madaktari kuuza damu.

Badala ya kujadili nini kinasababisha madaktari kuuza damu na nini kifanyike mnakuja na propaganda za kipumbavu. Nyinyi ndio wale mnaokaa kwenye vyumba mnajadiliana mikataba ya raslimali nyingi za nchi hii kuwa siri kama madini ili muweze kupata 10% ambayo hata hao Donors mnaojipendekeza kwao wanawashangaa na kuwadharau.

Ni hivi tatueni matatizo yaliyopo ndio mkondo wa sheria uchukuliwe kwa hao wanaouza damu. Ila mimi siiamini kama maendeleo ya Tanzania yatapatikana na aina ya nyinyi watumishi wa serekali ambao mnaamini sisi watanzania ni maskini na hatuwezi kuendelea mpaka tusaidiwe.

Mtabaki kuiba mali ya umma muonekane matajiri mbele ya maskini wanaowazunguka na kuongea kiswanglish ili kuwakoga maskini wanaowazunguka huku mkikutana na wazungu kwakuwa mnajinyenyekeza wanaishia kuwapa mikakati ambayo itaendelea kutufanya sisi masikini daima.

Shame on you msio tatua tatizo la msingi mnabaki kutuonyesha udhaifu wenu wa kushindwa hata kudhiti uwizi wa damu mahospitalini.
 
Swali dogo la kujiuliza: WHO RUNS THE BLOOD BANK? Yeyote anayejua hospitali yoyote Tanzania ambapo daktari ndio in-charge wa blood bank aseme hapa! Maana sio kila mfanyakazi hospitalini basi ni daktari! Wakati niko Muhimbili nimeshaona mara kibao watu wanakuja muulizia mfagia ward (sio hata nurse) wakiulizia dokta fulani! Sasa hu6yu mtu akifanya ujinga wowote ule, basi ni dokta kafanya...hata akifumaniwa mtaani huko kwenye uwazi wataandika daktari bingwa kafumaniwa!

Zote hizo ni chuki zinazotokana na ukweli kwamba...not everybody can be a doctor, hata tukilipwa hela ndogo, tukiwa maskini...still, not everybody can be a doctor! You will hate that fact for the rest of your miserable life!
 
Back
Top Bottom