Boflo
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 4,384
- 4,409
Pia soma >Kwanini Madaktari huandika mwandiko usiosomeka? Husababishia vifo watu 7000 kwa mwaka Marekani
Habarini za leo wajameni!
Jana nilikwenda Pharmacy nikakuta mtu analalamika kwamba amekwenda kwenye Pharmacy karibia tatu wameshindwa kutambua baadhi ya majina ya dawa alizoandikiwa na Doctor kwa sababu ya mwandiko (hand write).
Alipofika kwenye Pharmacy ambayo na mimi nilikuwepo akampa Mfamasia ile karatasi, na yeye akamwambia mimi sina hiyo dawa, jamaa akamwambia yule dada naomba uniandikie vizuri jina la hiyo dawa hapo chini ili nikienda kwengine huenda nikaipata.
Kwa kuwa wanashindwa kuisoma vizuri, yule dada hakuweza kuandika akazuga zuga akamwambia we nenda tu kawaonyeshe watakupa.
Badilikeni Madaktari mnasumbua watu na miandiko yenu.
Last edited by a moderator: