Unaposema sisi wenyewe na huku ukimfanya Karume kama sisi sote unamaanisha nini? Halafu hili la kuondoshwa Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais wa Tanzania lilifanywa na Katiba ya 1977?Muungano mlisaini wenyewe, Karume akakubali kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Nyerere akiwa Rais! Mabadiliko ya 11 ya Katiba ya JMT, 1977 ndiyo yaliyoondoa nafasi ya Makamu wa Rais kuwa moja kwa moja Rais wa Zanzibar! Kama Wazanzibari wasingeupenda Muungano wasingekimbilia mahakamani kupinga mabadiliko hayo ya 11! Pia malamiko mengi ya Wazanzibari ni ya "kutaka haki zaidi" kwenye Muungano badala ya kuuvunja! Otherwise, wangeshajitenga zamani!
Iwapo haki haipatikani basi si bora huo Muungano ukavunjika?