LordJustice1
JF-Expert Member
- Jan 19, 2011
- 2,263
- 530
Kwa suala la Muungano Watanzania Bara si kweli kuwa wanaupenda ndiyo maana hawajaenda mahakamani ila ni kuwa hawajali. Rais wa Muungano anaonekana wazi ni Rais wa bara japo Nyerere alionekana ni Rais wa Tanzania yote kwa matendo. Watu wa Zanzibar kwa sababu ya kufanana mitizamo ni rahisi kuamua maamuzi yanayofanana tofauti na bara. Wazanzibari ni wachache na unapozungumza suala la nchi yao wanaacha kutazama "Yanga na Simba" wanakusikiliza unachosema. Huku bara mambo ni tofauti kidogo. Huku bara Maaaskofu na Masheshe wakisema "acheni!" ni rahisi watu kusikiliza bila kuweka maswali mengi (kama ilivyokuwa imani katika dunia ya nchi za kiarabu ambayo sasa inaanguka), Zanzibar wanamsikiliza yule anayesema yale wanayoamini tu na si U-Shehe wake.
Si kweli kwamba Wazanzibari hawapendi ushehe wa mtu, ndio maana chokochoko za Muungano huwa zinaanzia misikitini!