Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,852
- 12,088
Awali, memba huyo alidai Sheria ya Chuo inazuia kufanya mtihani bila kuwa na kitambulisho ‘active’, matokeo yake wapo waliolazimika kusogeza mbele mitihani yao ili wafanye Mitihani Maalum Septemba 2024 kwa madai hawajafanikiwa kupata Vitambulisho Vipya licha ya kukamilisha mchakato wa kujisajili mapema.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Rose Joseph anaelezea upande wa pili kilichotokea na kinachoendelea, anasema:
“Tangu chuo kilipofunguliwa katika mhula huu mnamo Oktoba 28, 2023, kwa mujibu wa Kanuni na Taratibu za Usajili wa Wanafunzi ni kuwa pindi wanapoingia chuo (Mwanafunzi) wanatakiwa kukamilisha mchakato wa usajili kisha ndio wanapata namba na kitambulisho.
“Tangu wakati huo hadi sasa (jana Februari 23, 2024) tumesajili Wanafunzi 33,127, hao wapo vizuri wamefuata taratibu inavyotakiwa.
“Tunatambua kuwa kuna Wanafunzi wanachangamoto ya ada, mfano wapo wanaotegemea wafadhili na wengine wanajilipia wenyewe, hivyo huwa inatokea kunakuwa na uchelewaji wa hapa na pale.
“Hali hiyo imekuwa ikisababisha tuongeze muda wa usajili na kuwakumbusha kuwa wajisajili kwa kuwa hawataweza kuingia kwenye chumba cha mitihani bila kuwa na kitambulisho.
“Hivyo, baada ya kufika muda wa mitihani ndio watu wanakurupuka kufanya usajili, matokeo yake hatuwezo kuwahudumia wote kwa mara moja, wao wanataka kulipa na wapate vitambulisho hapohapo, kuna uzembe ambao wanaufanya lakini wanalaumu chuo wakati ni uzembe wao wenyewe.
“Inapofiki hatua hiyo system inazidiwa nguvu kwa kuwa kila Mwanafunzi anaingia kusajili dakika za mwisho, kisha wanaanza kutoa lawawa.
“Tumekuwa tukitoa matangazo mara nyingi kuwakumbusha wajisajili, tumetumia hadi Serikali ya Wanafunzi lakini wapo ambao hawakutimiza hilo kwa kuwa tunajua lawama zitafuata mwishoni.”
Kuhusu hoja ya Mdau, soma hapa - Chuo cha UDOM kuna utaratibu mbovu wa kutoa vitambulisho, wanatuumiza Wanafunzi