Madai ya Janeth Shayo, Mkazi wa Uru, Moshi, kutosikilizwa

Dkt. Gwajima D

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
543
3,575
Imetolewa taarifa hapa Jf hoja mchanganyiko na anayejitambulisha kama Anonymous kuwa: mtajwa hapo juu sikumsikiliza alipokuja mara ya pili kwamba amekwama kwenye mfumo wa huduma dawati la jinsia.

Kwanza napongeza watoa taarifa za kijamii pale penye changamoto za kijamii ambazo, zimekwama hatua moja au nyingine na jamii inahitaji msaada.

HATA HIVYO, naomba kuweka taarifa ya ufafanuzi kuwa, sijawahi kuongea na mlalamikaji kwa simu na wala huwa situmii huduma ya kuongea kwa simu kwa yeyote yule bali huduma ya kuandika ujumbe Ili nibaki na kumbukumbu na ndiyo nilitangaza hivyo.

Nimemuomba mlalamikaji hizo namba ambazo alizipigia baada ya yeye kukanusha pia kuwa hakuongea na mimi, tangu asubuhi hadi sasa jioni nasubiri. Uzuri Nina Imani mifumo ya simu za kuongea inatunza kumbukumbu, hivyo sitarajii nikanushe halafu kumbukumbu ziseme niliongea naye.

Huenda aliongea na namba za call center au namba za madawati ya Jinsia eneo husika, ambapo, tangu asubuhi nimeomba anitumie kumbukumbu husika, bado hajanipatia.

Aidha, kwa taarifa zaidi kuhusu shauri hili ni namba
MOS/IR/1950/2024 KIFO CHA MASHAKA ambapo, Watuhumiwa 5 wamekamatwa na Polisi kwa mahojiano (taarifa ya Polisi imeambatishwa hapa chini kwa rejea sn 3).

WITO WANGU; Watoa taarifa za jamii pamoja na pongezi kwa kazi kubwa mnayofanya, vema muwe mnachukua taarifa pande zote siyo moja (strike a balance). Vinginevyo tutayumbisha mshikamano wa pamoja katika kupambana na matukio haya.

Ahsanteni sana, mbarikiwe wote, Kila mmoja kwa kadri alivyochangia.
IMG_20240315_140850_094.jpg
IMG_20240315_140850_164.jpg
 
Aah Mama atakuwa nayo ya kimya kimya sema yupo vizuri mama very energetic
Mimi jambo likisingiziwa kwenye kazi ambayo Naamini nimefanya, nitajitetea mwenyewe kwa data. Sitaki hata kujipa stress. Yaani kazi ifanyike mwingine aje apindue apoteze wengine. Haikubaliki. Au ww unaonaje ndugu yangu

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Sijasoma mada ila nimesikitika sana
Jitahidi usome, itakusaidia kwenye kushirikiana. Siku hizi hakuna kukubali kusingiziwa jambo la uongo, simama, sema. Kama ni kweli na ni kwa bahati mbaya, hekima ni kuomba radhi. Lakini kama uongo simama kwa hekima, kanusha.

Ni hekima mchango wa kila mmoja kwenye ujenzi wa taifa utambuliwe.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom