Mada moto live on Channel Ten: Yaliyojiri mwisho wa wiki kuelekea uchaguzi mkuu

Allyoki

JF-Expert Member
Mar 23, 2007
251
138
Mada moto live on channel ten Monday, Mada Justice Kibuki na Humphrey Polepole kuchangia mada.

MADA: Yaliyojiri mwisho wa wiki kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba, 2015.
=========

Kibuki: Sumaye sidhani kama amefanya makosa kuhama, ni kukua kwa demokrasia katika nchi yetu. Toka kuwepo kwa dunia watu wanahama kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Polepole: CCM ilipewa dola kwa mara ya kwanza tangu vyama vingi mwaka 1995, haijawahi kutokea CCM mawaziri wake wakuu wawili kwenda kwenye vyama vya upinzani, na kama aliesema mchangiaji wa kwanza si kosa hili.

Polepole: Inatokea kwa sababu misimamo ilikuwepo kwenye chama imebadilika, pia inaweza kutokea endapo utabadili fikra (misimamo) zako.

Sumaye Amesema ameenda kule kuimarisha upinzani, mtu mmojawapo alieguswa na udhaifu wa vyama vya upinzani. Anasema kuwa na upinzani dhaifu au CCM dhaifu hakusaidii pande zote mbili kwa sababu tija ni utoaji bora huduma kwa watanzania.

Vyama vingi havipaswi kuleta uadui, mimi nikiwa mwanaCCM nimeshirikiana na watu wa UKAWA kwa karibu sana na hawakuhoji mimi ni mtu wa CCM.

Sumaye alikuwepo kwenye serikali miaka kumi, alifanya nini kuimarisha upinzani! Mkapa alitumia lugha kali kidogo.

Haya maneno hata mwalimu Nyerere alipokuwa anatofautisha mpumbavu na mjinga aliyatumia. Mpumbavu ni mtu analijua jambo na bado anaenenda. Vyama hata tungekua tumebadili vinakuja kuboresha hali za watanzania na si kuja kuwakomboa(liberation) watanzania.

Kibuki: Watanzania tuna kawaida ya kuheshimiana, sio utamaduni wetu kuongea makubwa na mazito kama yale. Kusema hawa watu ni upumbavu sio haki, mpumbavu si neno la kumwambia mwanadamu wa kawaida, kuelekea uchaguzi mkuu maneno mengi yatatumika ndio maana tunasema tuwe na kampeni za kistaarabu. Rais mstaafu alienda kwa ukali sana, watanzania tunaangali ni yupi atakuja na sera nzuri, matusi hayatusaidii, tunatakiwa tuwe na hekima.
Marais waliotangulia wamefanya kazi nzuri sana nikiri, lakini nasema tuthaminiane, hamna kitu kinachotukera kama kusema lazima tushinde, lete sera zako sisi tupige kura. Sisi hatuhitaji kusikiliza matusi, tunahitaji kusikiliza sera.

Kuna chuki inapandikizwa, baadhi wakifanya mkutano mpaka muda fulani wanaachwa na wengine wanapigwa mabomu. Na tukiangamia watakaoathirika sana ni watanzania wa kawaida.

Polepole: Kipindi cha kampeni ni kipindi cha kusikiliza hoja kwa kuvumiliana. Nisitoe hoja kisha ukatoa matusi, mimi ni mhanga.Kiwango cha matusi nilichotukanwa baada ya kufanya kipindi mwezi uliopita ni kikubwa, ustahimilivu ni kitu muhimu sana na wanaonitukana ni wale wanaosema mimi naipendelea CCM.

Alichokisema mzee, kinachotakiwa kufanywa ni kuboresha na si ukombozi.


Tutashinda mapema asubuhi siioni kwenye magazeti, naisikia ya goli la mkono tu. Kushinda asubuhi saa nne wakati wengine bado hatujapiga kura pia haifai. CCM kwa mara ya kwanza imethibitisha ni chama cha mapinduzi, mapinduzi haikuwa vita bali kubadili fikra kuvunja vyama viwili na kutengeneza kimoja. CCM imevunja majabali, yamekatiliwa mbali bila kujali uwezo wao wa fedha kisha akainuka John Magufuli. Ni mtu ambae hawakumtegemea kabisa.

Magufuli kujinadi alizungumza kama kiongozi mtumishi, mimi ni mwana CCM na nasema katiba inayopendekezwa ni mbaya. Magufuli ana fikra huru na amesema mambo mengi na unajua kabisa tumepata kiongozi na mtumishi.

Katika miaka kumi ameenda ulaya si zaidi ya mara nne, CCM ni chama sikivu, wamejua katiba inayopendekezwa imetugawa watanzania ndio maana wameacha mchakato kwanzo kwa sababu katiba sio ya chama, katiba inaletwa na raia.

Kibuki: Hawa wanasema goli la mkono, hawa wanasema tutashinda asubuhi. Wanaosema goli la mkono kwa akili ya kawaida wanalazimisha tofauti na wnaosema tutashinda asubuhi. Mungu akiamua kuweka kiongozi awe Magufuli au Lowassa atakuwa, yule aliekuwa mchafu anaweza kuwa msafi. Kuna vitu vingine tukivichunguza, uchaguzi huu una mkono wa Mungu.

Kuna utajiri ambao Mungu ameufunua kama utajiri wa gesi, kila mtoto atakaezaliwa lazima afike form six. Atakae kuwa mpagani ni kwa sababu ya ugumu wa maisha, watanzania wengi wanaamini Mungu. Ulimi ni kiungo ambacho hakifugiki, pembezoni mwa Tanzania wanajua siasa iko vipi kuliko watu wa Dar es Salaam.

Wasomi wetu wangetuwekea tunataka taifa letu liongozwe kwa mustakabali huu, mgombea atakaekuja aseme yes mimi nitayafanya.

Polepole: Anachosema ndugu yangu niseme, Mungu ametupa mamlaka ili tuziendeshe na ametupa maarifa. Vyama vinapaswa viseme ilani, sisi si kumwachia Mungu tu bali tusome ilani na ni mkataba wa ahadi kwa miaka mitano.

Magufuli jana alisema Inawezekaje Tanzanite inachimbwa Tanzania lakini inaonekana ni Kenya na India

Kibuki: Mtu anahukumiwa kwa matendo na si dhamira, miaka yote ni hayohayo.

MASWALI
  1. Venus(Mwanza): Nashauri kila mgombea anaeweka ahadi tufungiane mkataba. Tunahitaji mbadala kutoka sehemu mmoja kwenda nyingine, kwanini mtu atuahidiRajabu: Tunaangalia serikali ilichofanya na matatizo tuliyonayo
  2. Alex(Ubungo): Tukizungumza ukombozi hatuna maana ya ukombozi wa ndugu, hata CCM ina uwezi wa kuwakomboa watanzania kifikra, naona Polepole amejikita huko, huko tumeshaondoka zamani. Inakuwaje nyumba 2400 zinauzwa na kujengwa nyumba 700
  3. Omari(Zanzibar): Siku zote tunaahidiwa, vitu kama maji tunaahidiwa miaka 50 sasa, inakera bwana.
  4. Nicholas: Niungane na wale ambao hawana uhakika na ahadi za wagombea, Polepole unifafanulie swala la katiba.
  5. Nshangani(Lindi): Nawaasa vijana tusikilize sera za vyama vyetu, tupige kura kwa Lowassa.
  6. Mbuzi(Tandika): Tumemwona Magufuli kajinadi sana mpaka mimi nimemkubali, Viwanda havijajengwa rasilimali zinapopatikana(anatoa mfano wa tumbaku kulimwa Moro na kuletwa Dar etc)

Polepole: Kubwa ni kuendelea kuwa washiriki kwenye kuleta maendeleo yetu, mimi kama raia nina wajibu wa kushiriki moja kwa moja, serikali ni watu na watu wenyewe ndio sisi. Kingine maendeleo ni hatua, taaluma yangu ni maendeleo. Mwalimu alipokea nchi hii mainjinia hawakuzidi kumi, madaktari hawakuzidi kumi, nchi hii watendandaji walikuwa wazungu. Gesi ilijulikana zamani lakini mwalimu alisema msichimbe. Leo hii limejengwa bomba, umejengwa mtambo Kinyerezi, maendeleo ni hatua.

Tulipata ukombozi, kazi tuliyonayo sasa ni kuendelea kuboresha maisha ya watu wote, na hili ni jukumu la watu wote, ni jukumu la watu wenye wazo mbadala.

Kibuki: Kiu ya watu ni kusonga mbele, chuo kikuu wanahitimu watu kila mwaka lakini hata kutengeneza baiskeli hawawezi, madera yanatoka China.

Baada ya kampeni kufunguliwa watu wasiwe washabiki, wasiweke siasa moyoni, inawezekana mtu wao wanaesema hajakwatwa ndio ametoa rushwa.

Polepole: Msewe tuna EPZ wanatengeneza jeans na suti, hivi vitu vipo. Tangu mwaka 60 tuna standard gauge ya TAZARA, watu wanadhani wa kwanza ni kutoka Kenya.
 
Chanel mbona kila siku mnaalika kada Wa ccm Polepole mnatakiwa mnaweka balance,yeye mada yake ni Lowassa tumemchoka !!
 
Hivi leo ataacha kusema mimi kijana Mdogo kabisa,nyie ni wakubwa kwangu,kama wewe ni Mdogo mambo ya Lowassa umejuaje na ya Magufuli unafunikaje ??
 
Angekuwa si mjenga hoja ningempuuza, nasubiri siku apate anaewezana nae kwa hoja zenye mashhko na ushawishi.
 
Julius Mtatiro naye aende hata kama hajaalikwa.Polepole you cant Julius Ntatiro katika nyanja zote...
 
Madamotto live on channel ten monday mada justice kibuki na humphrey polepole mada yaliyojiri mwisho wa wiki kuelekea uchaguzi mkuu october 2015

Mimi vyombo vya habari vyenye kupendelea ccm nimeacha kuangal4 wala kusikia. kwa mfano radio free nimeifuta. star tv nasubili muda wa bbc kiswahili na focus on africa tu. nimeona bora habari za mitandaoni. CH10 nimeifuta kabisa toka walivyoanza kumtumia polepole vibaya. tbc nimefuta. ITV na radio one ndiyo nafuatilia kidogo afadhali.
 
It is expected ...kinajulikana anachoenda kuongea...kumshambulia lowasa

hatutaki tena kusikia personal attacks

Tunataka kuongelea issues
 
Kwa nini hivi vipindi vinamualika Polepole kila mara na kuongelea mada karibu ileile? Hakuna watanzania wengine wenye uwezo wa uchafumbuzi wa mambo ya kijamii na kisiasa?

Ukitazama kipindi cha jana cha Star TV unona Polepole anarudia mambo yaleyale kila siku ba unajiuliza hiki ndicho vyombo vya habari vinataka kusikia? Nadhani wangekua wanajitahidi kuweka fikra tofauti ingefanya vipindi kuwa na faida zaidi. Kumrudia mtu yuleyule kwa mada zilezile hata kama ana mawazo mazuri kiasi gani kutawafanya wasikilizaji wamchoke na wamwone hana jipya. Ningekua mimi ni Polepole nisingekubali.

Jana asubuhi mwendesha kipindi ilikuwa akimuuliza swali anamwachia Polepole atiririke pasipo kumkatisha mpaka ache mwenyewe kuongea, hakukuwa na maswali ya kuunganika (rejoinder questions) wala kumkatisha na kumwelekeza kuichambua mada kwa masuala, Polepole alikuwa anaongea kama anatoa muhadhara.
 
Hivi hiki kipindi pole pole ni mtangazaji au mchambuzi kwa hiyo mchambuzi wa kudumu ni pole pole tu au maana naona wanabadilishwa watu waupinzani yeye habadilishwi
 
Julius Mtatiro naye aende hata kama hajaalikwa.Polepole you cant Julius Ntatiro katika nyanja zote...

Dah,,,wakuu tangu nimejitambua sijawahi kuona kiingereza kibovu kama hichi,,,""Polepole you cant Julius mtatiro katika..."",,,u made my day kamanda wa ukawa
 
Back
Top Bottom