Machangu Wala Bakora Mwezi Mtukufu

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
1.jpg

549128_336809559739892_671110977_n.jpg

http://api.ning.com/files/xvg03MJhTS*9froBh32XGgVUU18iPC OczjRjubBUoGF-Rju-*RMfq0Nr4X-miLTXJPvMkGkKzqO0wxfOrhdPh8F8C AmKvLhS/1.jpg?width=600

http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/machangu
 
Wanawachapa wao wakiwa kama nani...? wana mamlaka gani kisheria ya kufanya hivyo?
wangewapeleka polisi hii nchi inasheria zake sio kila mtu kujiamulia.
 
Mijitu mingine bana! Wadada wa watu wako kazini yenyewe inajichukulia tu majukumu mikononi. Mijinga kabisa hiyo mijitu.

Leave those girls alone you stupid disrespectful bastards.
 
Unyanyasaji wa kijinsia huu,wanatake advantage ya udhaifu wao wa kimaumbile,mbona vibaka,wavuta bangi wanaendelea kama kawaida au mwezi mtukufu dhambi ni moja tu.
Ningependa nione wakiwaendea mateja na hizo bakora zao,halafu tuone kati yao na mateja nani uamsho.
 
Mijitu mingine bana! Wadada wa watu wako kazini yenyewe inajichukulia tu majukumu mikononi. Mijinga kabisa hiyo mijitu.

Leave those girls alone you stupid disrespectful bastards.

Wewe utawekewa fatwah shauri zako. Usijione kuwa uko mbali ndiyo unatukana watu.
 
Unyanyasaji wa kijinsia huu,wanatake advantage ya udhaifu wao wa kimaumbile,mbona vibaka,wavuta bangi wanaendelea kama kawaida au mwezi mtukufu dhambi ni moja tu.
Ningependa nione wakiwaendea mateja na hizo bakora zao,halafu tuone kati yao na mateja nani uamsho.
Mkuu nakuunga mkono, huo ni unyanyasaji wa kijinsia kwanini wasichape bakora na wateja wao au ndio kuogopana? kwani hao wanauzia wanawake wenzao?

Tumewazoea, wameshindwa nguvu ya hoja wameibukia kwenye hoja ya nguvu.
 
Wewe utawekewa fatwah shauri zako. Usijione kuwa uko mbali ndiyo unatukana watu.

Waweke hiyo fatwah tuwaone akina Khomein wa bongo!, wapuuzi hawana maana yoyote,wao wenyewe ndo wateja wakubwa wa hao akina dada poa!
 
Ni uonevu wa mwisho kabisa. Hakuna anaeruhusika kuchukua sheria mkononi hata kama kuna sheria za nchi zimekiukwa.

Serikali inapaswa kulinda raia wake
 
Wanawachapa wao wakiwa kama nani...? wana mamlaka gani kisheria ya kufanya hivyo?
wangewapeleka polisi hii nchi inasheria zake sio kila mtu kujiamulia.

Wawapeleke POLISI ipi tena?!
Hawa nao ni Polisi wa Mahakama ya KADHI wanatimiza majukumu yao kisharia...:spy:
 
Mkuu Grafani11, nafikiri Kiziza alikuwa na maana ya MATEJA na si WAteja.

Mateja ni wale jamaa wanaotumia madawa ya kulevya na wameshakuwa Wagonjwa wa hizo dawa maana bila kutumia basi hali yake inakuwa mbaya sana na anakuwa mtu hatari sana kuwa karibu yake.

Mwenyewe nalaani sana watu kujichukulia sheria mkononi. Ila hii habari kidogo inachanganya maana habari yenyewe kwa urefu ipo kwenye Mjengwa Blog.

KISA KUHARIBIWA SWAUMU

Kwa mujibu wa vijana hao, walifikia hatua ya kufanya zoezi hilo baada ya muumini mmoja wa kiume kukatiza maeneo ya Corner Bar, Afrika Sana na kuvutwa kisha kuchezewa nyeti na makahaba na kusabisha kuharibika kwa swaumu yake.
Ilielezwa kuwa baada ya kukutwa na kimbembe hicho, ilibidi muumini huyo kukatiza safari yake ya kwenda kuswali msikikini mishale ya saa 2:00 usiku. (hii mishale kweli kwa Dar kunakuwa bado kuna Swaumu? Mwanaume mzima uvutwe na Changu doa na wakuchezee NYETI, tena BURE? Khaaa!!!)

Mkuu nakuunga mkono, huo ni unyanyasaji wa kijinsia kwanini wasichape bakora na wateja wao au ndio kuogopana? kwani hao wanauzia wanawake wenzao?

Tumewazoea, wameshindwa nguvu ya hoja wameibukia kwenye hoja ya nguvu.
 
[h=2]Sunday, July 29, 2012[/h]
[h=3]MWEZI MTUKUFU: Machangu wala Kichapo na Viboko Vya Nguvu huko Kinondoni Ni Kutoka Kwa Kikundi Cha Jumuia Ya Uamsho Tanzania Bara![/h]

Stori: Issa Mnally na Richard Bukos
Machangu wamekiona cha mtemakuni! Wakati Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ukiwa katika chungu cha nane, akina dada wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili maarufu kama Machangudoa au Chipsi Funga au Wauza Sukari Tamu, wamekula viboko laivu baada ya kutuhumiwa kuwatega Waislamu.
Tukio hilo lilijiri katikati ya wiki hii ambapo vijana wa Kiislamu waliodai ni wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Tanzania Bara walizunguka mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuwashushia fimbo machangu ambao kwa sasa wametapakaa kila kona jijin

WATUMIA BAJAJ

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, waumini hao, wakiwa wamevaa kanzu huku wakitembea na bakora mkononi walichukua jukumu la kukodi Bajaj na kuzunguka maeneo mbalimbali jijini inapofanyika biashara hiyo haramu ya ukahaba.

BARABARA YA SHEKILANGO

Vijana hao waliolenga kukomesha biashara hiyo hasa kipindi hiki cha mfungo walianzia kwenye Barabara ya Shekilango inayokatiza kwenye viunga vya Sinza, Dar ambapo kila kituo cha daladala kuanzia Afrika Sana hadi kwenye mataa ya Shekilango waliwakuta machangu na kuwatandika viboko kabla ya kutua mitaa ya Mwenge.

KINONDONI

Baada ya kufagiafagia Sinza kwa kuwaadabisha wanawake hao ndipo zoezi likahamia mitaa ya Kinondoni ambapo nao walipokea bakora za kutosha huku wengine wakitoka nduki.

KISA KUHARIBIWA SWAUMU

Kwa mujibu wa vijana hao, walifikia hatua ya kufanya zoezi hilo baada ya muumini mmoja wa kiume kukatiza maeneo ya Corner Bar, Afrika Sana na kuvutwa kisha kuchezewa nyeti na makahaba na kusabisha kuharibika kwa swaumu yake.
Ilielezwa kuwa baada ya kukutwa na kimbembe hicho, ilibidi muumini huyo kukatiza safari yake ya kwenda kuswali msikikini mishale ya saa 2:00 usiku.

Ilisemekana kuwa aliporudi nyumbani alitawadha na kufunga safari nyingine ya msikitini na alipofika kwenye nyumba hiyo ya ibada ndipo akawasimulia waumini wenzake ambao nao walikasirishwa na kitendo hicho hivyo wakapanga kuvamia maeneo yote ya biashara hiyo ili kuwashikisha adabu.
Waandishi wetu, wakiwa kwenye mishemishe zao za kutafuta habari mishale ya saa 5 usiku waliwashuhudia waumini hao wapatao saba wakishuka kwenye Bajaj nyeusi maeneo ya Sinza wakiwa na bakora mikononi kisha kuwavaa machangu hao na kuwatandika.

Wakati wakitekeleza zoezi hilo, jamaa hao walisikia wakiwaambia: "Sisi tupo kwenye swaumu nyiye mnatutega, ala!"

HAWAHESHIMU MWEZI MTUKUFU?

Waumini hao waliongeza kuwa makahaba hao wamekuwa hawaheshimu mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan ndiyo maana wanaendeleza biashara yao hiyo ya aibu.
www.globalpublishers.info

From: Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo: MWEZI MTUKUFU: Machangu wala Kichapo na Viboko Vya Nguvu huko Kinondoni Ni Kutoka Kwa Kikundi Cha Jumuia Ya Uamsho Tanzania Bara!

Similar Discussions

Back
Top Bottom