Mabosi mnaokula bar acheni kuwaweka madereva kwenye gari kama wafungwa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Nimesikitika sana leo jamani embu tuwe na utu hata kama una kangast mwekesawa asiharibu kwa mamaa

Gari zaidi ya tatu zilikuwa pale city hotel nje stj/stk xxx/yyy

Nje madereva wamesimama kama wanaota jua masikini mmoja namjua nkamuuliza vipi kaka kwema karibu
tuonje oohhh ahsante mpwa kibosile yuko ndani humo anakula na mzigo yake na jamaa zake

Jamani nani kawaambia mkila madereva mnaawaacha wangamue kwenye magari kwani hawana matumbo kama nyie embu badilikeni bana mi bosi wa jf lakini kila nikienda sehemu dereva wangu anakula shav ila asile ninachokula hiyo haifai kama wali nyama ale ugali nyama, usihofu nimasharti ili tuendelee kuongoza jf

kwi kwiii ila inaumaa sana unamkuta mjomba wako yuko nje ya gari jua linapiga kangamua mbaya una uwezo wakumnunulia akale masikini anaogopa bosi yuko ndani anakula aisee

Shidaaa
 
Bora ya hao wanaokula chakula mbaya zaidi wapo wanaokwenda diversion na kuwasubirisha madereva wao nje
 
Hapo yuko kazini yeroo - kazi yake ni dereva na hiyo ndiyo ofisi yake - halafu haimaanishi kuwa yeye huwa hapati muda wake wa kula kwa hivyo hizi huruma hazina stahili yoyote..
 
Kazi yao ndo hiyo kusubiria mhusika aje ili ampeleke atakapo
 
mabosi wa hivyo ni wanoko mpaka nyumbani.binadamu kuwa simple uki faint kwenye gari nani wa kwanza kutoa taarifa ?
 
Gari yake ndiyo ofisi yake, wewe unataka watoke ofisini waende wapi? Muda wake wa kula ukifika bosi anajua.
 
Mabosi wachoyo sana.....

Kwani lazima amkaribishe dereva?!! Huo ni mwanzo wa kuzoweana na kukosa ufanisi, sanasana ni kumpa off tu, bwana nitakuwa humu ndani kwa muda wa dakika 40, kama unataka kuingia sehem ingia ila observe muda! Tatizo mmbongo akiambiwa hivyo atachomoka halafu bosi anamaliza mishe zake haoni gari anaanza kupiga simu tena. Wacha kila mtu afanye kazi yake.
 
nizaidi ya wabahili mtumishii..nahisi kuna baadhi ya pesa wanapata zina masharti....
Hapo umenena vyema paroko......maana wengine vyeo vyao huwa wanavipata katika mazingira magumu na kwa ndumba sana...wengine kwa kuwafanya ndugu zao machizi mandondocha au hata kuutoa uhai wa binadamu wenzao......sasa usitegemee mtu kama huyo atakuwa na utu kiasi cha kumthamini dereva wake...ikiwa ndugu zake kawaweka misukule hadi kufikia levo hizo.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom