Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Thursday, May 10, 2012 9:34 AM WAKAZI WA MBAGALA jijini Dar es Salaam walioathirika na mlipuko wa mabomu mwaka juzi, wameandaa maandamano ya amani kumuona Rais kwa lengo la kushinikiza kulipwa malipo yao ya uharibifu wa nyumba zao. |
Wakazi hao juzi walitinga Ofisi za mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kufikisha lengo lao hilo wakiongozwa na Mwenyekiti wao Steven Gimonge. Gimonge alisema wamejipanga vilivyo kuandamana kumuona Rais Kikwete ili kuijua hatma yao na kutambua kama hawajapata stahiki zao. Gimonge alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na kushindikana na kudharauliwa kwa maombi yao na juhudi za kumuona Waziri Mkuu tangu Februari 2010 kugonga mwamba Zaidi wakazi 2000 wanadai fidia kutokana na kuharibiwa kwa nyumba zao zilizoharibiwa kwa mabomu yaliyotokea April 2009 huko Mbgala na kusababisha vifo kadhaa. Waathirika wa Mabomu Mbagala waandaa maandamano |