Nasikia mabomu yanapigwa huko getini , sina hamu. Waloandaa walikosea kuweka ukumbi mdogo may be wali undermine watu. Na la pili hao wanafunzi wakati mwingine wanatakiwa kuelewa kama ukumbi hautoshi wangeondoka wasubiri muda mwingine, mchakato ndo unaanza, wao kila kitu fujo tu, wanapenda sana vurugu.
wanapenda amani na haki mama. tatizo ni serikali imeshindwa kujipanga na kuwa na nia ya kutoa haki kwa makundi ya wananchi kushiriki. Serikali ilidhani madai ya katiba mpya ni ya viongozi wa vyama vya upinzani. Serikali ilidhani kwa kuwa wananchi hawana access na vyombo vya habari kujieleza kama serikali inavyolazimisha vipindi maalumu kwenye tv basi wananchi hawataki katiba mpya. Serikali ilidhani wananchi hawataelewa maudhui ya mswada huu wa kutunga katiba mpya na hivyo kwamba inaweza kuwaburuza kama ilivyozoea.
Serikali kama ilikuwa na nia njema ya kutoa haki kwa makundi yote ya wananchi kutoa maoni yao kuhusu huu mswada wa kutunga katiba mpya, ilitakiwa ijipange kutoa fursa hizo kwa kila kundi kwa kutumia utaratibu na kuwawezesha.
Vurugu zinazoendelea Dodoma sasa hivi ni matokeo ya Serikali kukusudia kunyima wananchi fursa ya kushiriki na kusikilizwa kikamilifu. Wanafanya mambo kwa kutegea tegea, hadi wakiona hali inabadilika wanazidiwa ndipo wanabadilisha utaratibu.
Kwanza walipanga kufanya public hearing dodoma peke yake mara moja tu. Malalamiko yalipotokea wakasema na Dar na Zanzibar. Leo watu wamekuwa wengi Dodoma sasa wanasema maoni yatakusanywa kwa vikao viwili leo na kuendelea hadi siku tatu. Hata hizi hazitoshi
Yaani ni kama kusema huko serikali hakuna hata mtu mmoja anayeweza kufikiri na mwenye nia njema na wananchi!!
Sio kweli Muhosin, Ukumbi hautoshi wangekaa wapi? na bunge ni sehemu ya kuheshimiwa wao wana mabango wanawaza vurugu tu, katika hili natetea kwasababu nashuhudia, ukumbi ni mdogo, kosa labda ni kuchagua ukumbi that all.polisi wametumia mabomu kutawanya wanaharakati dakika chache zilizopita. Kwa mara nyingine tena serikali inakandamiza haki za raia!
Sio kweli Muhosin, Ukumbi hautoshi wangekaa wapi? na bunge ni sehemu ya kuheshimiwa wao wana mabango wanawaza vurugu tu, katika hili natetea kwasababu nashuhudia, ukumbi ni mdogo, kosa labda ni kuchagua ukumbi that all.
Hizi tv za tz bomu kweli kweli. Wamejazana hapa na makamera yao muda mrefu lakini hakuna live coverage. Hata Star tv ambao wanatangaza live kutoka Dodoma hawaoneshi yanayojiri ukumbi wa bunge ambayo ni historia kubwa sana. Wananchi wameamua kufanya public hearing yao nje ya bunge barabarani baada ya kuzuiwa kuingia ndani
Sasa kama ukumbi hautoshi,mnataka watu waruhusiwe kuingia ili wakakae wapi?
Public hearing hii inafanyika kwa siku 3 mfululizo,sio lazima kila mtu aingia leo...waweke utaratibu wa wale waliojiandikisha kutoa maoni yao juu ya muswada ndio waingie ndani kwa zamu kulingana na uwezo wa ukumbi kubeba watu. Wakimaliza watoke na kuwapisha wengine wenye maoni yao. Wengi wa waliojazana pale ni mashabiki na washangiliaji-wale hawana haja ya kuwemo ndani,wanaweza kufuatilia proceedings hizo kwa kutumia PA system nje ya ukumbi na kwenye vyombo vya habari-radio ONE wanarusha live.
Kwa wale walioamua kuendesha public hearing yao nje,ni counter-productive kwasababu maoni yao hayatafika yanapotakiwa kufikishwa...sana sana wanapoteza muda wao.
By the way,mjadala wa leo ni kuhusu Muswada wa kuanzisha tume ya Katiba, na sio kujadili Katiba yenyewe...hivyo inputs/ideas/critique inatakiwa ku focus kwenye vifungu vilivyo ndani ya Muswada wenyewe.
Baada ya kusema haya mimi nina wazo moja japo kwa mchakato unaoendelea sasa linaweza kuwa limepitwa na wakati. Kwa nini zisiwepo mechanism nyinginezo za kukusanya maoni juu ya muswada husika kama vile wananchi kuruhusiwa kutoa maoni yao kwa njia ya barua, e-mail,social network platforms etc
Kwa kuruhusu hizo njia nyingine,hata watu wasioweza kufika Dar,Dodoma au Zanzibar physically wataweza kutumia haki yao ya kutoa maoni pasipo kulazimika kuwepo kwenye maeneo yanapofanyika shughuli hiyo