HORSE POWER
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 2,102
- 1,415
Kama kuna kauli iliyonifurahisha na kujisikia fahari kama Mtanzania kutoka kwa Mkuu wa Nchi,basi ni kauli hiyo hapo juu ya Rais John Magufuli.Hiyo ni kauli ya kiuongozi.Amekana unafiki kwa kujikweza na kujipendekeza kwa 'wajomba' kwa kuhofia kuusema ukweli.Alichozungumza ndio ukweli na utabaki kuwa ukweli.Mabeberu hawawapendi Watanzania,bali wanaipenda Tanzania kwa rasilimali zake.Ametuma ujumbe mahsusi kwamba ana msimamo wa namna gani.
Ujumbe wake ufike kule Brettonwoods,yalipo makao makuu ya taasisi tatu mumiani duniani za WB,IMF na WTO.Sera za taasisi hizi ndizo zinazoumiza uchumi wa Afrika.
Ujumbe wake ufike kwa mawakala wote wa mabeberu hapa nchini;wanaoshabikia,kupigia debe na kunufaika na 'sera fukarishi' za mumiani hawa Magharibi.
Tumuunge mkono Rais wetu.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu mlinde Rais wetu.