Mabati ya ALAF yako overated sana

Kwa utafiti wangu mdogo nimeona watanzania tunapigwa na wauza mabati ya ALAF kwa kuaminishwa kua yako special sana kuliko mabati mengine.

Haya mabati tunapigwa, hayana ubora wa kipekee kuliko mabati mengine, hayana utofauti wowote.

Kwa kweli sijaona chochote cha ziada kwenye hayo mabati. Usiwe draged na majority, hayana upekee wowote.
Wewe umepaua nyumba yako kwa mabati ya kampuni gani? Nyumba ina muda gani na ubora wa mabati unayotaka yawe mbadala wa ALAF Galco ni upoje?
ALAF ni kama godoro la Tanfoam wanavyojisifia (alinunua babu mpaka mjukuu analitumia/analikuta). Kampuni za kichina zimeleta mabati ya ajabu kabisa Afrika Mashariki na Kati...unanunua bati ya rangi inaanza kupauka ndani ya kipindi kifupi sana. Labda kama unakusanya maoni ya utafiti wako ujue Watanzania wengi wanaamini nini kuhusu mabati, lakini ALAF ni habari nyingine kabisa ukiachana na kampuni kubwa kama DECRA and the like of best brands...
 
Bati kuzungushwa mbali mrefu siyo issue, ni suala LA Technology mkuu.

Sijasema kuzungushwa umbali mrefu ndo ubora kiongozi! Mimi nimezungumzia ALAF kwa sababu nimeliezekea na kiwandani nilipata fursa japo ya kushangaa nini kinafanyika au wewe umeezekea bati gani kiongozi
 
Bando ilikua bei gani, na bati ngapi
Hiyo haiuzwi kwa Bandle Kiongozi namm nilichukuwa bati kulingana na uhitaji wangu so walinikatia kulingana na uhitaaji wangu kulikuwa na za mita moja moja, mbili na nusu, za mita tatu hadi mita sita kama sio sita ni saba so ilikuwa inategemea na kila upande wa paa una urefu kiasi gani na bati zikachukuliwa kulingana na huo urefu na upana wake kwa upande wa upana wa paa nifundi akae apige hesabu kwa upana huu zitakaa bati ngapi so sikuchukua bati za urefu mmoja mm kwenye urefu sikukata bati hata moja kwani ulikuja urefu niliouhitaji bati.
 
Hivi Alaf kiwanda chao kiko wapi? Ningependa niwatembelee siku moja na data zangu nione gharama zao ili nijue hichi kibanda changu kitanigharimu sh ngapi?

Na by the way nyie wengine mnaolalamika mabati yanawazingua mtudadavulie mmenunua ya geji gani?
Maana siku zote bati ni geji hizo rangi ni mbwembwe tu.
 
ALAF wapo vzr mkuu kinachowasumbua wengi nigarama zao ila nivyema ujichange uchukue kitu chakueleweka kuliko kuchukua zabei rahisi thn mwakan tu unarud kuanzisha uzi wakushauriwa rangi nzur yakupaka kwene Bati

Alafu ukiangalia hao wachina bei zao zinakaribiana na ALAF kwa mabati wanayouza kwa Mita kuna utofauti mdogo sana!
 
Hivi Alaf kiwanda chao kiko wapi? Ningependa niwatembelee siku moja na data zangu nione gharama zao ili nijue hichi kibanda changu kitanigharimu sh ngapi?

Na by the way nyie wengine mnaolalamika mabati yanawazingua mtudadavulie mmenunua ya geji gani?
Maana siku zote bati ni geji hizo rangi ni mbwembwe tu.

Ukiwa TAZARA chukua barabara ya Nyerere kuelekea Posta nadhani nikabla ya RTD/TBC siku hizi kuna barabara moja matata sana kwa kifupi ni korofi sijui siku hizi hiyo barabara inainga mkono wa kulia kama upo barabara ya Nyerere kuelekea Posta. Au ukifika TAZARA Uliza tu kiwanda cha ALAFU KIPO WAPI Ila kuwa makini kabla ya kuingia kiwandani kuna watu wa mabanda wanauza hao mabati karibia yote ambayo ni rejected japo wengine wanasema wanakuwa wanafanya deal na wafanyakazi so mabati wanayouza ni salama kabisa!
 
Asante kwa kunijuza.
 
Binafsi mm nalikubali bati la ALAF na ndilo nililoezekea nyumba na nilienda kuchukuwa kiwandani kwa vipimo nilivyokuwa navihitaji, asikwambie mtu bati lina miaka minne kasoro lakini utaliona chafu kipindi cha kiangazi kama lina vumbi hivi sasa ngoja mvua inyeshe utadhani ngozi ya nyoka mweusi:):):) Nimeezekea versetile rangi Chacoal grey! Nilipata na wasaa wa kuingia kiwandani asikwambie mtu material yanavyobadilishwa kuwa bati ni hatari na sheet inazungushwa umbali mrefu kabla ya kuanza kukatwa na mbaya zaidi nikaambiwa hicho kiwanda kilikuwa cha serikali enzi za Nyerere!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Nikahuzunika.
Mkuu hiyo rangi ya charcoal grey ni nzuri hadi kero, binafsi nilitoa 6M huku nachekelea kuchukua hilo bati na kamwe sijawahi kujuta.
 
Embu leteni variaties ya bati na garama zake. Binafsi natafakari ains gani za bati nikayotumia kuezekea lakin unafuu wa bei kuzingatiwa
Mkuu inshu ya bati inahitaji umakini mkubwa sana ukikosea hapa hutatamani kuitazama nyumba yako. Ni bora ujipange uchukue kitu kilicho bora, ukitaka unafuu kwa sasa inaweza kukugharimu hapo baadae.
 
Jaman vp kuhusu SUNSHARE nayo je yanalingana na ALAF????
Yanalingana ubora hata mafundi huwa wanashauri ALAF na SUNSHARE.

Hata bei zao hazijapishana sana.

Kuna mtu juzi kanunua migongo mipana alienda kiwandani ALAF hawakua na rangi ya GREY ikabidi aende SUNSHARE cha kushangaza bei ya ALAF ilikua pungufu kidogo...so nadhani zina ubora sawa
 
USIHARIBU BIASHARA ZA WATU... TANGAZA MABATI YAKO WATU AUTOMATICALLY WATATAMBUKA KUNUNUA HAYO ALAF.. MPUMBAVU MKUBWA WEWE...
 
Inategemea na kampuni,kuna jamaa yangu alipaua na bati za kampuni 1 ya wachina inaitwa eagle,unaenda mwaka wa 3 bati ziko vile vile,jirani yake alipua na alaf,ngoja niishie hapa kwa leo
Atakuwa alikudanganya huyo jirani yake
 
Kwa utafiti wangu mdogo nimeona watanzania tunapigwa na wauza mabati ya ALAF kwa kuaminishwa kua yako special sana kuliko mabati mengine.

Haya mabati tunapigwa, hayana ubora wa kipekee kuliko mabati mengine, hayana utofauti wowote.

Kwa kweli sijaona chochote cha ziada kwenye hayo mabati. Usiwe draged na majority, hayana upekee wowote.
Sijaona fact ktk maandishi yako, as ulinunua na hukutosheka na ubora? Umefanya tafiti yoyote labda kwa vigezo/vipimo vinavyotumika ukabaini udanganyifu ama una refference ya kipi juu ya bidhaa husika? Nadhani yakupasa uje na fact pasipo hiyo hiki ulichokiandika ni rahisi kuata tafasiri ya chuki ama umbea.
 
Kwa utafiti wangu mdogo nimeona watanzania tunapigwa na wauza mabati ya ALAF kwa kuaminishwa kua yako special sana kuliko mabati mengine.

Haya mabati tunapigwa, hayana ubora wa kipekee kuliko mabati mengine, hayana utofauti wowote.

Kwa kweli sijaona chochote cha ziada kwenye hayo mabati. Usiwe draged na majority, hayana upekee wowote.
Unajua maana ya biashara ni matangazo?
 
Back
Top Bottom