Mabasi yatakiwa kufungwa mikanda kabla ya Oktoba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
2939238.jpg

Friday, August 28, 2009 10:16 AM
KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, James Kombe, amewaagiza wamiliki wa mabasi yote ya abiria kuhakikisha mabasi yao yanafungwa mikanda ya kwenye siti kwa usalama wa abiria kabla ya Oktoba, mwaka huu Akizungumza jijini Dar es salaam jana, Kombe alisema suala la kufunga mikanda katika mabasi sio jambo la hiari na halina mjadala ni wajibu wa kila mmiliki wa basi kuhakikisha anatekeleza agizo hilo kwani ni moja ya sheria za usalama barabarani nchini.

Alisema ifikapo Oktoba mosi basi ambalo litakuwa halijatekeleza agizo hilo litakamatwa na askari na kupelekwa mahakamani pamoja na kulizuia kuendelea kufanya kazi hiyo ya kusafirisha abiria.

Amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na mabasi ambayo hayatatekeleza agizo hilo na watapewa adhabu kali kwa kudharau agizo hilo.

Amesema lengo la agizo hilo ni kukabiliana na ajali za barabarani zimalizike ama zitoweke kabisa na kila basi linatakiwa liwe na cheses nzuri, na mikanda ya kuvaa abiria wanapokaa kwenye siti kwa kuwa abiria wamekuwa wakijeruhiwa na kufa kwa kukosekana kwa mikanda hiyo. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2939238&&Cat=1
 
Back
Top Bottom