Mabasi yaendayo kasi....!

jcb

JF-Expert Member
Jul 6, 2010
280
66
Serikali inaanzisha mradi wa mabasi yaendayo kasi kuja katikati ya jiji ili kupunguza msongamano na foleni katikati ya jiji.
Barabara ndo hivyo Mh. John P. Magufuli anaendelea nayo ili kufanikisha hili.

Hivi kweli hili ndilo suluhisho la foleni? Na mabasi haya yataleta tija kwa Taifa hili?
Je fedha inayo wekezwa katika mradi huu itakuwa na faida?
Je kuna shughuli za uzalishaji kiasi gani katikati ya jiji au ndo tuna kwenda kariakoo kununua bidhaa? Maana shopping zetu nyingi tunafanyia kariakoo hata mtu akihitaji chupi anakuja katikati ya jiji kununua.

Wana JF naomba mnisaidie katika hili kwani nimetafakari nimekosa jibu au majibu juu ya hili.
 
suluhisho ni watu kuacha kutumia private cat na watumie buplic cars kama daladala na tax
 
Huu mradi sitaki hata kuusikia maana umechosha masikio yangu. Tangu 2003 huu mradi unapigiwa kilele za siasa leo ni zaidi ya miaka 8 hata mradi wenyewe haujaanza, hivi kweli huu mradi utakuwa na ufanisi uliotarajiwa? nadhani inaweza chukua miaka mingine 5 kabla ya mradi ku-kamilika, je mikakati mingine ni ipi ilikukabilaina na tatizo la foleni? hizi siasa za CCM ni hatari sana, ni mambingwa wa kugawana posho lakini kuteleza miradi ni shida kweli.
 
naungana na aliyesema tukitaka kupunguza msongamano dar, basi tuhakikishe tunatumia treni, ambapo kutakuwa na route kama tatu ama nne hivi kwa kuanzia: toka stesheni hadi ubungo kwenda kimara, stesheni hadi vingunguti-gongo la mabomu-pugu na nyingine stesheni -tabata reli-kimanga, na ile ya mbagala. pia kwa watu wa masaki na kawe boti ziendazo kasi zaweza kutumika.

Lakini pia, watu wa mipango miji na mamlaka zinazoruhusu ujenzi dar, usiruhusu ubomoaji na ujenzi wa maghorofa city centre. kama mtu ana hela yake anataka kujenga ghorofa, apelekwe kibamba, kinyerezi, chanika, mbagala rangi tatu- n.k ili kuepusha watu wote kujazana katikati ya miji.

na tatu suala la wizara kuhamia Dod ni sawa, na hata kama ofisi ndogo zitabaki zipelekwe mbali na city centre. vilevile serikali ijipange kuhakikisha kuwa huduma zile muhimu mfano ufuatiliaji wa malipo baada ya kustaafu(pensheni),mashule, mahospitali mazuri vipatikane paia katika mikoa mingine huko, ikishindikana basi kwa kuanzia kila kanda ipewe mamlaka ya kumaliza mambo huko bila kwenda dar.

kingine ni barabara zilizopo zipanuliwe kiasi cha kupitisha magari mengi kwa wakati. kwani hayo yaendayo kasi yenyewe yatakuwa yanaruka hewani? serikali pia ifanye kwa matendo pia kuwa na barabara za juu kwenye junctions zote kubwa.
 
mimi nahisi haya mabasi yaendayo kasi ni mazuri ila yatatugharimu miundo mbinu yake.
kuokoa gharama wangetuletea treni za kisasa kila wilaya,still machuma ya reli bado yako mengi kule stoo ya reli. na kwa mradi huu serikali itajiingizia kipato sana.
 
naungana na aliyesema tukitaka kupunguza msongamano dar, basi tuhakikishe tunatumia treni, ambapo kutakuwa na route kama tatu ama nne hivi kwa kuanzia: toka stesheni hadi ubungo kwenda kimara, stesheni hadi vingunguti-gongo la mabomu-pugu na nyingine stesheni -tabata reli-kimanga, na ile ya mbagala. pia kwa watu wa masaki na kawe boti ziendazo kasi zaweza kutumika.

Lakini pia, watu wa mipango miji na mamlaka zinazoruhusu ujenzi dar, usiruhusu ubomoaji na ujenzi wa maghorofa city centre. kama mtu ana hela yake anataka kujenga ghorofa, apelekwe kibamba, kinyerezi, chanika, mbagala rangi tatu- n.k ili kuepusha watu wote kujazana katikati ya miji.

na tatu suala la wizara kuhamia Dod ni sawa, na hata kama ofisi ndogo zitabaki zipelekwe mbali na city centre. vilevile serikali ijipange kuhakikisha kuwa huduma zile muhimu mfano ufuatiliaji wa malipo baada ya kustaafu(pensheni),mashule, mahospitali mazuri vipatikane paia katika mikoa mingine huko, ikishindikana basi kwa kuanzia kila kanda ipewe mamlaka ya kumaliza mambo huko bila kwenda dar.

kingine ni barabara zilizopo zipanuliwe kiasi cha kupitisha magari mengi kwa wakati. kwani hayo yaendayo kasi yenyewe yatakuwa yanaruka hewani? serikali pia ifanye kwa matendo pia kuwa na barabara za juu kwenye junctions zote kubwa.

Mwenye maeneo mengi mjini ni NHC, na huyu Mkurugenzi mpya wa NHC mipango yake ya kufikia 2020 ni kubomoa majeno yote ya zamani yaliyopo town center na Upanga na kujenga mengine mapya yatakayozidi 10 floor. wahusika kwenye traffic planning and managment naombeni mwelimisheni huyu jamaa maana hajui anachokifanya.
 
Back
Top Bottom