Mabalozi wa jumuia za ulaya wajiandaa kutoa tamko kuhusu kufungiwa mwanahalisi

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Mwana-Nadha.jpg

BALOZI wa Uholanzi nchini, alipotmbelea gazeti la MwanaHALISI na kukutana na uongozi wa gazeti hilo, Saed Kubenea Mhariri Mtendaji na Jabir Idrissa, Mhariri mkuu wa gazeti hilo.

Wakati huo huo, taarifa zilizolifikia MTANZANIA zilisema kuwa Jumuiya ya Mabalozi nchini jana zilikutana na kufanya kikao cha pamoja kujadili suala la Serikali kulifungia gazeti la Mwanahalisi, kwa kile kilichodaiwa kuandika habari za uchochezi.
 
Sasa naona kama kuna mtu ambaye amemuaribia JK ni huyu aliyetoa pendekezo la Kufungiwa Gazeti!! Najua sasa wataanza Hata kufuatilia Gazeti lenyewe na maudhui ya Habari yenyewe!! Then itakuwa ndio Kujiumbua Tosha!! Ilitakiwa wakae Kimya ila kwa sasa wameshalikoroga!! Hawa wachumia Tumbo hawamsaidii rais ila wanamuaribia!! Lol!!
 
It is about time JK kuumbuka we are tired hakika watu walisema kufungiwa na mahakamani kila kukicha.Si walikuwa wanamcheka Mtikila jamani?
 
nimepitia habari ya Mwanahalisi kuhusu Ulimboka na ukisikiliza maneno ya DR.ULIMBOKA kwenye YOU TUBE utagundua mwanahalisi walinukuu kila kitu. Kama ni uchochezi itakuwa DR.ULIMBOKA ndo alijichochea mwenyewe na wala sio mwanahalisi kitu kisichowezekana.
 
Ndio taabu ya kuwa omba omba, hawa development partners wanajua timing sana kwani sasa wanajua mnapitisha budget yenu tegemezi na hapo hapo ndio watakapokaza screws juu ya misaada yao/ good governance!! Uchumia tumbo utaifanya serikali ifyate mkia na kulifungulia MwanaHalisi ama sivyo hakuna budgetary support na hivyo miradi mliyowaahidi wadanganyika itabaki hivyo hivyo kwenye karatasi!!
 
mkuu umeongea ukweli mtupu
 
Duh jamaa wanatafuta kila sababui ya kumnyima fungu la bajeti huyu Baba Mwanaasha
 
na bado kitaeleweka tu Mwanahalisi la wiki iliyopita lilikuwa linakuja na yale majina ya wenye billion 300 uswiss ndio maana jamaa akaenda kugawa ng'ombe teh teh teh
 
Upepo tu utapita

nikimaliza ziara arusha naenda zangu ulaya,,,,,,,
 
Upepo tu utapita

nikimaliza ziara arusha naenda zangu ulaya,,,,,,,

Hapana huu upepo naona unasumbua, huenda babu kule Bagamoyo amejisahau kuchoma ule ubani niliomnunulia juzi.

hivyo nitaanzia Bagamoyo kwanza nikapime huu upepo naona migomo inafuatana sana na watu wanachonga sana kuhusu uongozi wangu. Nikitoka bagamoyo then Ulaya nawafuata huko huko hao mabalozi.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Back
Top Bottom