Amiliki
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,085
- 1,004
Wakati najaza fomu ya kuniwezesha kuja kupata Kitambulisho cha Uraia, niliona Watu wawili wakija pale bila ya kuwa na Viambatanisho vilivyoorodheshwa kwenye fomu, lakini wakiwa na barua za Mabalozi wao wa Nyumba kumikumi ambao ni waajiriwa wa CCM (Na si kutoka kwa Watendaji wa kata ambao wanatambulika Kiserikali).
Je hawa Mabalozi wa nyumba kumi kumi wa CCM bado wanatambulika Kisheria na kwenye shughuli nyingine za kiserikali kama Mahakamani pia? Maana nimeambiwa kuwa huwa wanatoa pia barua za kudhamini mtuhumiwa mahakamani na zinakubalika.
Hivi kama wanafanya pia kazi za kiserikali, ni nani anawalipa? Je CUF na CDM viongozi wao wa huko mitaani wana nguvu hizo hizo pia, yaani wanaweza kutoa barua za Udhamini na zikakubalika?