mabadiliko makubwa ya mitaala ya elimu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
JUMUIYA ya Afrika Mashariki, inakusudia kufanya mabadiliko makubwa ya mitaala ya elimu kuanzia ya msingi hadi ya chuo, ili kuziwezesha nchi wanachama, kutumia mtaala mmoja tu.Akizungumza na Mwananchi jijini Mwanza, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta alisema mkakati huo, wanafunzi wa nchi hizo kusoma popote ndani ya jumuiya, tofauti na ilivyo sasa.

Kwa mujibu wa Sitta, wanafunzi wanaopata fursa ya kusoma katika nchi za jirani ni wale tu ambao wazazi wao, wana vipato. "Tunaamini mpango wa kuwa na mtaalam wa aina moja, utarudisha haki sawa kwa watoto wa jumuiya hii katika sekta ya elimu, Watoto wa nchi moja watakwenda kusoma katika nchi nyingine kwa usawa kama wanavyosoma sasa katika nchi zao," alisema waziri Sitta.

Alisema pamoja na mpango huo, jumuiya pia imeridhia uhuru kwa wahadhiri wa vyuo vikuu, kuingia na kufundisha katika vyuo vikuu vya nchi yoyote ya Afrika Mashariki.Alisema hatua hiyo imengatia mahitaji makubwa ya wahadhiri katika vyuo vikuu vya nchi wanachama.

Alisema kwa mfano, nchi ya Burundi, inahitaji zaidi ya wahadhiri 1,000 kwa ajili ya kufundisha lugha ya Kiswahili na kwamba milango iko wazi kwa wanaotaka kwenda kufundisha.

"Tunakwenda kwa awamu, baada ya wahadhiri wa vyuo vikuu, tutaenda mbele zaidi kwa walimu wa shule za sekondari na wale wa shule za msingi,"alisema Siita.

Tayari nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, zimeanza kutekeleza itifaki ya soko la pamoja kwa manufaa ya raia wa nchi hizo.


source EAC mbioni kubadilisha mfumo wa elimu
 
hasa wakenya hapo sasa mbaya zaidi wabongo hatupo makini kabisa katika kukagua na kuthibitisha vyeti!tutapata waalimu vihiyo wengi sana!wakati huohuo waalimu wetu wazuri wataenda nje!
point... Sema wawe makini na walimu/wahadhiri wanaofoji vyeti.
 
Ah? Nilikuwa najiuliza pa kuipeleka Shahada yangu ya Kiswahili. Senkyu SISIEM!(natania tu wakuu)
 
Hiyo poa mheshimimiwa,ila sasa serikari yetu inabidi iongeze kipato kwa hawa wa kwetu, otherwise wata kimbilia nje wote.
 
okay...interesting. Lakini nashindwa kuelewa ni namna gani mtaalam utarahisisha wazazi kupeleka watoto nchi jirani.
 
dah afadhali now wenye BaEd, Bed tutafaidi tutaenda hata kufundisha primary Rwanda huku Tz mchango wetu hauthaminiwi kabisa nafkiri huko salary ina package kibao
 
tatizo la hizi nchi kila moja inatumia lugha yake sijui lakini mie kwa mtazamo wangu naona kama itakua rahisi kama ikitumika lugha ya kiingereza ambayo kwa kiasi kikubwa inaweza kuwaunganisha wananchi wa nchi zote hizi kuliko kiganda,kiburundi,kinyarwanda au kiswahili maana kama waganda hawatakagi kabisa kuongea kiswahili
Yale yale....
FIKRA SAHIHI HUJA KWA LUGHA SAHIHI!
 
Back
Top Bottom