Mabadiliko Katiba ya CCM Yamelenga Kumwengua Lowassa

Mkuu Ronaldo, kumbe Lowassa alitakaswa vya kutosha. Sasa hili la ufisadi linatoka wapi? Kumbe ndio maana watu wakisema kama Lowassa ni fisadi basi aburuzwe mahakamani, wapinzani wake wanasema ni fisadi huyo. Jamani fisadi kwa lipi utasikia ni fisadi tu hata Nyerere alisema kwa kunukuliwa na Kasori! Mpelekeni basi mahakamani. Utasikia wakisema huyo ni fisadi na alijiuzulu kwa ufisadi. Kumbe masikini wa mungu hakujiuzulu kwa ufisadi.

Wao wanawaza 2015 mwenzao anawaza kuwang'oa kwenye uchaguzi wa chama 2012 . Kazi kweli kweli.

we umenena. Uchaguzi huu wanaouita wa jumuia,cjui wilaya, utaondoa maadui zake wengi na kuweka wachumia matumbo wa el. Watch out 2012!

Huo uchaguzi wa 2015 labda waamue kuiba kura juu kwa juu zaidi ya walivyofanya 2010 ndiyo mgombea wa CCM atashinda. Otherwise hii ngoma safari hii ni ya CDM. I can bet on that!!

On the other hand CCK inakuja kuimaliza CCM!!

Mkuu,
katika thread nyingine hapo awali ulizungumza kwamba CCK = CCM, unless sikukuelewa. Kama nipo sahihi, una maana gani unaposema kwamba CCK inakuja kuimaliza CCM badala ya msimamo wako wa awali ambao kamanilikua sahihi, nilikuelewa kwamba - chama cha kukimaliza CCM ni CDM?

..Chimbuko la Kuwaondoa wazee wa CCM kwenye vikao vya Kamati kuu....ni KIkwete.....

Dhumuni lake ni Kuwaondoa haraka kabla ya vikao vya michakato ya uchaguzi mkuu wa ndani wa chama .....na baadaye uchaguzi mkuuu wa Taifa 2015....
Ilijulikana wazi kuwa kutokana na uungwaji mkono wa JK kushuka....hangekuwa na nguvu ya turufu ya kupanga safu za uongozi ...chamani..na baadaye hangekuwa na nguvu ya kuweka mgombea urais anayemtaka mwaka 2015.........Mgombea yeyote ambaye angeungwa mkono na wazee ..angekuwa na nguvu kuliko mgombea ambaye angewekwa na JK.......hii ndio imepelekea JK ...anayesifika kwa siasa za "kimjini mjini" .....kuwajengea wazee zengwe...

Wazee ...Mwinyi , mkapa,salmim,malecela,na Karume....inaelezwa kuwa wamekubali ....uamuzi huu...ili kumuacha ...abaki na ubishi wake...hasa ikizingatiwa tayari Wanayo kumbukumbu ya KIkwete kuwatenga kwenye uchaguzi mkuu wa 2010(matunda Yake Aliyaona )....sababu kuu iliyowauzi wazee ilikuwa kitendo cha KIkwete kukabidhi jukumu la kampeni kwa familia Yake....kinyume na utaratibu..hii ilipelekea chama kupoteza kura nyingi....
Kitendo cha wazee kuwekwa kando kinatarajiwa kuongeza wito la Umbwe la uongozi kwenye utawala wa KIkwete...na anayo hatari ya kuondoka madarakani na chama ......

Utaratibu wa wenyeviti kubaki kwenye Kamati kuu...ni utamaduni wa ccm ..iliuiga toka china,na Russia...huu unalenga kufanya smooth transition of power....kwamba rais akistaafu ....anatakiwa aendelee kuwa mwenyekiti wa chama ...Angalau kwa miaka miwili(uchaguzi mkuu wa taifa na chama unatofautiana miaka miwili)...ndani ya kipindi hichi rais mstaafu anapata fursa ya kuendelea kumshauri rais kwa mgongo wa chama...baada ya kumkabidhi rais kofia zake mbili( katakana na utashi anaweza kuamua kuondoka mapema Kama alivyofanya Mwinyi na mkapa au kumaliza miaka miwili Kama alivyofanya Nyerere na Karume wa sasa hapo Zanzibar )....baada ya kumkabidhi hubakia kwenye halmashauri kuu...

Mtoto amelilia wembe....

Nakubaliana na Post:But kwa sababu kuu zifuatazo:-

JK na Lowassa kwa sasa hawaendi sawa.(Kuna namna fulani yakuoneshana ubabe,kutokana nafasi ya kila mmoja kwenye chama)

Sababu ya kutokwenda sawa! -JK alimsaliti Lowassa mara nyingi mno (fuatilia trend ya kutafuta uraisi wa JK toka mwanzo)

Lowassa kama binadamu hawezi akavumilia usaliti mkubwa wa kiasi hicho-Kibinadamu chukua mfano mdogo tu.,wa mme au mke kufumaniwa na mke au mme(Katika hili Lowasa kasalitiwa ambitions zake!)

Lowassa anachofanya anataka ku fullfil ambitions  zake(Jambo ambalo si dhambi!..yeyote makini katika hii dunia ndicho siku zote  anafanya).

Ukiwafuatilia baadhi ya wanaCCM(akiwemo JK) kwa nini wanataka Lowassa aachie ngazi za uongozi..wanakwambia ni kwa sababu ya picha mbaya ya UFISADI inayopoteza aiba nzuri ya chama kwa watanzania,na si kwa sababu Lowassa ni FISADI,refer  tuhuma ya Richmond,ilimhusisha Lowassa moja kwa moja na UFISADI;Lowassa aliwajibika kwa kujiudhuru Uwaziri Mkuu...ni kiongozi gani mwingine aliweza kufanya hivyo kutokana na makosa au yake mwenyewe au aliyehusishwa nayo akiwemo Kikwete,Pinda,Ngereja,Chenge, ...msururu ni mkubwa sana?

Maoni:
Kila binadamu makini katika hii dunia ana struggle kila siku ku fulfill ambitions zake :-Yafuatayo ni baadhi ya mifano

Kuwa Mjasiliamali, Mwalimu,mkufunzi,Daktari,Nesi,askari,Rubani.....n.k

Mwimbaji,muubiri,mtangazaji,mwinjilisti,askofu.....n.k

Diwani,Mbunge,Mkuu wa Wilaya,Mkuu wa Mkoa,Naibu Waziri,Waziri,Waziri Mkuu,M/Rais,Rais.....n.k

Mtendaji wa kijiji/mtaa/Kata,Mkurugenzi,DAS,RAS,Naibu Katibu Mkuu,Katibu Mkuu......n.k

RPC,RCO,MKUU WA MAJESHI, JUDGE...n.k

Sasa basi.. kimtazamo hizo nafasi zote pamoja na nyinginezo huwa zinatafutwa,na nyingine kutokana na umuhimu wake zina vikwazo vingi ,hata hivyo hazituzuii sisi binadamu kuzipigania hasa ukiona unazimudu.. kwa manufaa yako mwenyewe,jamii,taifa na Dunia kwa ujumla.Pia hizi nafasi zinahitaji Rasilimali,hasa muda..kama hivyo ndio sahihi!Kuna sababu gani kwa ZITO KABWE,EDWARD LOWASSA na wengineo kuzipigania nafasi husika..WITO WANGU NI KWAMBA SIONI DHAMBI KWA YEYOTE ANAYEHITAJI NAFASI KWA MFANO YA URAIS KAMA ATAIMUDU KATIKA NCHI HII AKIWEMO ,LIPUMBA,CHEYO,LOWASSA,KABWE,DR.SLAA,DR.MIGIRO,MAKAMBA,MNYIKA...TINDU LISSU,SUGU...MSULULU NI MREFU SANA........
hitimisho:
Lowassa kaza buti,kama wengine nchini na kokote duniani ambavyo wamekuwa wakikaza buti.,ZUMA RAIS WA SASA WA AFRIKA KUSINI.,PAMOJA NA KASHFA YA UBAKAJI KABLA YA URAIS,STILL NDIYE ALIYECHAGULIWA KUWA RAIS WA  NCHI ILE..I MEAN,WANANCHI WALIMPENDA NA NDIE RAIS WAO.KAZA BUTI  LOWASSA!

Lowasa kashika robo tatu ya wajumbe wote nec hivyo basi piga ua bado atawasumbua; haitakuwa rahisi kivile wanavyopanga kumwengua. Hiyo ni hatua lakini bado kazi ipo kwani yule fisadi kadhamilia na kajipanga

Uchaguzi ni mwaka huu.

Jibu rahisiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Ni mwizi, fisadi.:yawn::eyebrows:

Why is he fighting hard for Presidential post? Do you think he loves this country alot? Or he get so sick to see the widening gap between the poor and rich? Does he realy want to c the national cake is shared equaly among Tanzanians? Do you trust him? is he real for the weak and poor of this country?

kushnei bwana EL,subiri mteule wa ccm atakeyetolewa na wanaccm lazima akubalike na makundi yote

naona title imechakachuliwa au imelenga kupotosha jamii, ilitakiwa iwe 'mabadiliko yamelenga kumbeba EL', na naomba nitabiri kifo cha ccm muda sio mrefu...

naona nguvu kubwa sana inatumika kumdhibiti huyu mheshimiwa ingawa dalili zinaonyesha hakamatiki ... let's wait and see the outcome, but i guess the 'cyclone' is going to leave a trail of so many victims by the wayside come 2015

WANAOSEMA LOWASSA NI FISADI KWA SABABU YA RICHMOND SAGA, HAMKUONA HII TAARIFA NILIYOIONA MAHALI?
EDWARD LOWASSA ALISAFISHWA NA MWAKYEMBE
Sasa ni wazi kwamba baada ya waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa kujitetea mbele ya kikao kilichopita cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) mjini Dodoma, wajumbe wengi wa kikao hicho, na wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini wanakubaliana kwamba mbunge huyu wa Monduli amekuwa akisakamwa na baadhi ya viongozi ndani ya chama chake na watu wengine, si kwa sababu yeye ni fisadi au kuna tuhuma za ukweli za ufisadi dhidi yake, bali ni kwa sababu ya mbio za urais za mwaka 2015.Ingawa yeye mwenyewe hajakubali wala kukanusha nia yake ya kugombea urais mwaka 2015 kupitia chama chake, lakini zimejengeka hisia kwamba ana nia hiyo, lakini kinachoumiza wengi si hiyo nia tu, maana na wengine wengi tu ndani ya chama hicho wanaelezwa kuwa na nia hiyo. Kinachowasumbua watu wasiompenda ni kwamba kati ya hao wanaodhaniwa kuwa na nia Inawezekana kumbukumbu za watu wengi zimechakachuliwa kiasi cha kutokumbuka kwamba Kamati Teule ya Dr. Harrison Mwakyembe iliyokuwa inachunguza sakata la mkataba wa kufua umeme baina ya TANESCO na kampuni ya Richmond ilimsafisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kwamba hakuwajibika na kujiuzulu kutokana na ufisadi wake katika sakata hilo, bali aliwajibika kisiasa kwa makosa ya watu waliokuwa chini yake.Inashangaza pia kwamba hata wajumbe wa Kamati hiyo, akiwemo mwenyekiti wao, Dr. Mwakyembe, wanashindwa kumtetea Bw. Lowassa anapoendelea sasa hivi kusakamwa na baadhi ya wanasiasa na wanajamii kwamba ni fisadi kutokana na kashfa ya Richmond, na hawajitokezi kumtetea na kurejea hitimisho la ripoti yao ndani ya Bunge. Lakini mbaya zaidi hata baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu kabisa wa chama chake hawakumbuki hitimisho la ripoti hiyo na wameng’ang’ania kwamba kujiuzulu kwa Lowassa uwaziri mkuu hakutoshi na inabidi chama kimtose zaidi kutokana na kashfa ya Richmond.Kwa kweli suala la tuhuma dhidi ya Edward Lowassa kwamba ni fisadi kutokana na tuhuma za Richmond, mtu unaweza kusema huu ni unafiki na chuki za kisiasa zilizopita kipimo. Suala la Richmond ni moja kati ya kashfa hapa nchini ambazo zilichunguzwa kwa makini sana na Bunge kupitia Kamati Teule na matokeo na hitimisho la uchunguzi huo yakamsafisha Lowassa kwamba alijiuzulu siyo kwa sababu alihusika moja kwa moja na kashfa hiyo bali aliwajibika kwa makosa yaliyotendwa na watu wa chini yake. Tarehe 15 Februari 2008, kwa mujibu wa taarifa rasmi za majadiliano Bungeni (Hansard), Dr. Harrison Mwakyembe, wakati akihitimisha hoja ya Kamati Teule iliyochunguza suala la Richmond, alisema:“Mheshimiwa Spika, ninaomba nianze na utangulizi mfupi na rahisi; uwajibikaji kwa viongozi waandamizi katika nchi zinazolinda na kuenzi demokrasia kama vile Tanzania, una sura mbili; sura ya kwanza, kiongozi anawajibika kwa makosa yake mwenyewe ya kiutendaji. Kiongozi anafanya maamuzi mabaya, pengine kwa kishawishi cha pesa, maamuzi yake yakaleta hasara au kiongozi ameshindwa kutoa ushauri mzuri kama kiongozi, kwa kukiuka kanuni, kukiuka taratibu na kadhalika, matatizo yakatokea, anawajibika. Sasa sura hii ya uwajibikaji, inahusisha uvunjwaji wa maadili, kanuni, sheria, miiko ya uongozi na kadhalika. Chini ya uwajibikaji wa aina hii, kiongozi anaweza akashitakiwa, akaadhibiwa mbali na kuachia ngazi. Nitarejea kwenye sura hii hivi punde. Suala la msingi hapa ni kuwa, kuna element ya adhabu katika sura hii ya kwanza.“Sura ya pili; kiongozi anawajibika kwa makosa ambayo si yake moja kwa moja ila yaliyofanywa na watendaji chini yake. Kitendo cha kuwajibika kwa aina hii, kunaijengea Serikali au taasisi heshima na imani ya pekee katika jamii, kunatoa picha ya kwamba, uongozi unajali, unalielewa tatizo kwa kubeba lawama wao wenyewe. (Makofi)“Mheshimiwa Spika, katika suala hili la Richmond, viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na Waziri Mkuu, walikuwa wanakabiliwa na uwajibikaji wa aina hizo mbili. Kwanza, uwajibikaji unaotokana na makosa ya viongozi wenyewe katika maamuzi yao, maelekezo yao, maagizo yao na kadhalika. Mawaziri wote wawili wa Nishati na Madini; aliyetangulia na aliyefuatia baadaye, Katibu Mkuu na Kamishina wa Nishati, wote tukawaona wana makosa ya moja kwa moja, waliyoyafanya wao kwa njia moja au nyingine. Kwa kuwa uwajibikaji wa aina hii, unatokana na ukuikwaji wa kanuni, taratibu, maadili, sheria na kadhalika, Kamati Teule ikahakikisha inawahoji wote ili kusikia their side of the story kabla ya kutoa pendekezo la kuwawajibisha kwa makosa waliyofanya. Ndiyo maana baada ya kuwahoji, tumependekeza hatua za kuchukuliwa dhidi yao.“Hali haikuwa hivyo kwa Waziri Mkuu; Kamati teule ilikuwa na ushahidi wa mawasiliano ya karibu kati ya Waziri Mkuu na Uongozi wa Wizara. Ushahidi huo haukutosha kwa uwajibikaji wa sura ile ya kwanza wa kiongozi kukutwa na makosa ya moja kwa moja, aliyoyafanya yeye mwenyewe kwa njia moja au nyingine, lakini ushahidi huo ulitosha kwa uwajibikaji wa sura ya pili, ambao hauhitaji mahojiano, kusikilizwa wala utetezi. Unawajibika kwa makosa ya watendaji walio chini yako. Hiyo ndiyo demokrasia. Wabunge wengi wametoa mifano mingi hapa, ukiwemo wa Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, alipokuwa waziri wa Mambo ya Ndani; aliwajibika kwa makosa ya askari huko Shinyanga wakati yeye alikuwa Dar es Salaam; hatukumsikia akidai apewe nafasi ya kusikilizwa na hata kama angepewa, bado angewajibika yeye mwenyewe. (Makofi)“Mheshimiwa Spika, Kamati Teule inatamka ukurasa wa 37 wa taarifa yake kuwa, ninanukuu ‘Ushiriki huu wa karibu wa Waziri Mkuu katika kila hatua ya zabuni ya umeme wa dharura si lazima uwe ushahidi wa kwamba, kiongozi huyo wa Kitaifa alihusika katika kuibeba Richmond. Unaweza pia ukawa ushahidi wa style yake ya kawaida kabisa ya Waziri Mkuu katika kufuatilia masuala yote ya Kitaifa kwa karibu sana, tukizingatia kwamba, nchi wakati huo ilikuwa katika kipindi kigumu sana cha ukosefu wa umeme…..”Nina wasiwasi kwamba baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa na wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM ama wamesahau kauli hii ya Dr. Harrison Mwakyembe, ama kwa makusudi wanataka kupotosha watanzania. Akina Nape Nauye na John Chiligati wanamjumuisha Edward Lowassa kwenye kundi la mafisadi kutokana na suala la Richmond. Lakini Chiligati alikuwa Bungeni wakati Mwakyembe akihitimisha hoja ya Kamati yake Teule, na alimsikia Mwakyembe akimsafisha Lowassa kwamba makosa yake hayakuangukia kwenye sura ya kwanza ya uwajibika, ya kiongozi kuwajibika kwa makosa yake mwenyewe. Sura hii ndiyo unayoweza hata kumwita mtu fisadi. Lakini Lowassa aliwajibika kwa makosa ya watendaji walio chini yake, hata kwa mujibu wa Dr. Mwakyembe. Anayewajibika kwa aina hii ya pili huwezi kumwita fisadi. Akisifu aina hii ya Edward Lowassa kuwajibika, Dr. Mwakyembe anasema, “…Kitendo cha kuwajibika kwa aina hii, kunaijengea Serikali au taasisi heshima na imani ya pekee katika jamii, kunatoa picha ya kwamba, uongozi unajali, unalielewa tatizo kwa kubeba lawama wao wenyewe”. (Makofi). Mwakyembe anakwenda mbali na kuhusisha uwajibikaji huu wa Lowassa na ule wa Mzee Ali Hassan Mwinyi.Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiwasilisha utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu suala hilo tarehe 28 Agosti 2008 alisema yafuatayo kuhusu azimio na. 16 la Waziri Mkuu kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huo, “Mheshimiwa Naibu Spika, hatua zilizochukuliwa ni kwamba, Azimio hili lilitekelezwa mwezi Februari, 2008 kwa kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu aliamua kujiuzulu kwa kuwajibika kisiasa kwa maslahi ya Taifa.” Hivyo ni wazi hata Serikali inakubaliana na Kamati Teule kwamba Mhe. Lowassa aliwajibika, siyo kama fisadi bali aliwajibika kisiasa kwa maslahi ya Taifa. Ndiyo maana Azimio na. 16 linalomhusu Waziri Mkuu halikuendelea kujadiliwa Bungeni. Hata wanaodai kwamba baadaye Spika aliondoa hoja hii Bungeni kabla halijakamilika, wajue kwamba suala la Waziri Mkuu kuwajibika (Azimio na. 16) halikuwemo tena, na kwa hiyo hata hoja ingeendelea kuwa Bungeni Lowassa asingeguswa tena.
Hapo umecheza kama Christiano Ronaldo.Hongera

Kapteni Lowasa ana mikakati sana, hivyo hata hao atawalobby 2, but its gud ngoja watafunane kwa sana, ili dhana za zidumu fikra za m/kiti ziwaondoke, itakuwa kama vita ya panzi.................
• :rant:

Napingana na wewe kifikra,lengo ni kuendesha kisayansi badala ya mfumo mazoea uliopo.Angalia mambo yanavyokwenda pale CDM NAMNA Magwiji ya mambo yanavyo kishauri chama at practical thoughts,ndiyo CCM wanaiga mfumo huo!TRUE OR FALSE?

It is TRUE!

Binafsi nimefurahishwa na mabadiliko hayo, siyo tu kwa kuenguliwa Kwa Lowasa na wazee wastaafu, bali pia lile Ombwe la uongozi litaondoka na m/kiti sasa atafahamika kwa vitendo na nchi itatulia(bilieve me or not).

Kwanza hawa wazee wastaafu 90% hawakupenda JK awe Rais mwaka 2005. Kutokana na sababu hiyo ya chuki (japo ni ya msingi sana kutokana na mwenendo wa uongozi wa JK), wazee hao wamekuwa wakikwamisha mambo mengi ndani ya ccm kutokana na ushawishi wao walionao kwa wajumbe wa NEC.

Pili, ni hofu aliyonayo JK dhidi ya wazee hao. Kumbuka alifanya kazi nyingi tofauti chini yao. Hivyo kila jambo alilokuwa akilifanya anahofia misimamo ya mabosi zake hao wa zamani (nidhamu ya woga). Kwa kuondolewa kwao naamini JK sasa atakuwa huru kufanya anachoamini kuwa ni sahihi.

Kwa ujumla, kuondolewa kwao kutamfanya mwenyekiti awe na nguvu za kimaamuzi na lile Ombwe la uongozi litapungua kama siyo kuondoka kabisa.

Kwa hili, tumpongeze hata kama hatumpendi.

Pamoja na hekima na busara walizonazo wazee wetu, lakini zisitumike sana hasa ktk kipindi hiki kigumu watz wanakipitia.

Kimatendo na sio kinadharia kwa sasa, Rais wa Nchi hajulikani ni nani, M/kiti wa ccm hajulikani ni nani, kila mtu ni msemaji, kila mtu ni mshawishi, kila mtu ni mfanya maamuzi (mepesi na ya hatari), kila mtu ni mlalamikaji e.t.c. Lets him be free bana..

Kumekuwa na tetesi kuwa marekebisho ya Katiba ya CCM kwamba viongozi wanaotumikia chama full time na nafasi zingine watapaswa wachague moja ama nafasi hizo zingine ama nafasi za unec ya CCM. Kama itakuwa imefanyika hivyo kwa ajili ya EL sidhani kama ni busara sana. Kama ni marekebisho ya kawaida tu na hayakuangalia EL basi hata mimi nayaafiki ni mazuri. Ila tu, ningependa kumpatia hekima bwana EL, kama ikiamuliwa hivyo ili yeye aweze kufanikiwa kufikia azma yake ya Uraisi (kama anayo kweli hiyo azma) basi achague kukitumikia chama na hivyo aachie nafasi yake ya Ubunge. Hapo naamini ataweza kuleta ushindani mzuri zaidi kwani kupitia chama mambo yote mswano!

Ni mambo yale yale ya Urais 2015 ambayo mimi naona muda wa kuyazungumzia hapa bado! ngoja nipite mie

Back
Top Bottom