Mabadiliko Katiba ya CCM Yamelenga Kumwengua Lowassa

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Nilikuwa nazungumza na mtu mwenye cheo cha juu sana ccm akaniambia mabadiliko ya katiba ya CCM ni moja ya mikakati ya kumwondoa Lowassa katika kinyanganyiro hivyo akina Nape wameshinda round ya awali.

Kwamba Lowassa ana nguvu sana na ukimpeleka Halmashauri kuu na Mkutano mkuu atashinda. Mkakati ni kumwondoa katika ngazi ya kamati kuu lakini kisiki alikuwa Mkapa na viongozi wengine wastaafu akiwamo Karume. hivyo kuwaondoa hawa Wazee kamati kuu ni kuondoa nguzo ambazo zingemtetea Lowassa wakati wakijadili jina lake likatwe. Na pia anasema mkapa ndie kiongozi mwenye nguvu na msimamo zaidi ndani ya chama hivyo ilikuwa muhimu kumwondoa katika nafasi za maamuzi. Akabainisha jinsi Nyerere alivyoingila mchakato wa kumpata Mkapa ni kwa kuwa alikuwa mjumbe wa vikao vya maamuzi otherwise asingefanya hivyo.

Kwa wale wanaokurupuka watasema ni hadithi ya kutungwa, sawa tu ila anayeweza kuwaza vizuri ataona mantiki ya taarifa hiyo
 
Lowasa kashika robo tatu ya wajumbe wote nec hivyo basi piga ua bado atawasumbua; haitakuwa rahisi kivile wanavyopanga kumwengua. Hiyo ni hatua lakini bado kazi ipo kwani yule fisadi kadhamilia na kajipanga
 
mimi toka muda nilitegemea hayo kufanyika . . .
Hii ni kutokana na ukwel kuwa jk sasa ni hasimu mkubwa wa Lowassa
 
Hapa bila kuhusisha tetesi, ni dhahiri kwamba haya mabadiliko ni ya kumbeba Lowasa wala siyo kumuengua. Hawa wazee waliondolewa ni wale wenye msimamo na maamuzi thabiti juu ya kile wanachokiamini. Kuwemokwao ndani ya vikao vya maamuzi kulikuwa kunatia shaka juu ya nini utakuwa msimamo wao juu ya Lowasa. Na sasa wajumbe waliobaki wote Lowasa anawamdu!!!
 
mimi toka muda nilitegemea hayo kufanyika . . .
Hii ni kutokana na ukwel kuwa jk sasa ni hasimu mkubwa wa Lowassa
Halafu msisahau kuwa JK pia ana ajenda yake. Anajaribu kurahisisha njia kwa yule anayemtaka amrithise madaraka.
Lakini naona watakatana mapanga huko
 
Halafu msisahau kuwa JK pia ana ajenda yake. Anajaribu kurahisisha njia kwa yule anayemtaka amrithise madaraka.
Lakini naona watakatana mapanga huko

If they segregate him he will separate them
 
Kwa nini hawataki Lowassa awe Rais?
Kwani wewe unamtaka?
A%20S%20embarassed.gif
 
Halafu msisahau kuwa JK pia ana ajenda yake. Anajaribu kurahisisha njia kwa yule anayemtaka amrithise madaraka.
Lakini naona watakatana mapanga huko

Huo uchaguzi wa 2015 labda waamue kuiba kura juu kwa juu zaidi ya walivyofanya 2010 ndiyo mgombea wa CCM atashinda. Otherwise hii ngoma safari hii ni ya CDM. I can bet on that!!

On the other hand CCK inakuja kuimaliza CCM!!
 
Kwa wale wanaokurupuka watasema ni hadithi ya kutungwa, sawa tu ila anayeweza kuwaza vizuri ataona mantiki ya taarifa hiyo

Usihofu hata hadithi zinamafunzo! Cha msingi ni kuwapongeza wanao panga mkakati huo,pamoja na mikakati ya kifedha inayofanywa na EL Kuteka wajumbe na taasisi fulani muhimu naamiini maombi ya JK-N YATAMFUNGIA MLANGO TARATIIIIIIBU Mpaka kieleweke at the end,hao wanaomkaribisha katika issues zao wengi wao ni wanafika wa nyuso zao.

Siku CCM wakimtoa huyu mtu watarudisha great thinkers wengi japo naye ataondoka ma uchafu mwingi wenye magamba ndani yake.TAFAKARI CHUKUA HATUA.

NIMEIPENDA HII THREAD.
 
lengo ni kumpa mwenyekiti umungu mtu, wakishatoka wazee wastaafu serikalini ambao ndio nguzo ya busara ya chama basi tena ccm itakuwa kama nccr ya mrema. hehehe yaani jk, pindo ndio watakuwa alfa-omega. kweli tumedhamiria kuipa cdm ushindi wa kishindo 2015
 
Napingana na wewe kifikra,lengo ni kuendesha kisayansi badala ya mfumo mazoea uliopo.Angalia mambo yanavyokwenda pale CDM NAMNA Magwiji ya mambo yanavyo kishauri chama at practical thoughts,ndiyo CCM wanaiga mfumo huo!TRUE OR FALSE?
 
Akiondoka tunabadilisha katiba tena ilinayeye awemo na wenzake wastaafu,maana lengo lake litakuwa limetimia.
 
EL anatumia mbinu zilizile ambazo JMK alizitumia! Sasa wanashangaa nini? Kwanini WANAMWOOGOPA? Kwa nini kuweka sheria kwa ajili ya kumwengua mtu mmoja?
 
EL anatumia mbinu zilizile ambazo JMK alizitumia! Sasa wanashangaa nini? Kwanini WANAMWOOGOPA? Kwa nini kuweka sheria kwa ajili ya kumwengua mtu mmoja?

Kwani hujui usemi huu? UWANJA TOFAUTI TIMU NI ILEILE? Ndiyo tunayo isubiri yaani CCM ASILI NA CCM MOVEMENT! Kwa lugha nyepesi CCM CLEAN NA MAGAMBA.JE KIPI kitakuwa na nguvu dhidi ya CDM?
 
Napingana na wewe kifikra,lengo ni kuendesha kisayansi badala ya mfumo mazoea uliopo.Angalia mambo yanavyokwenda pale CDM NAMNA Magwiji ya mambo yanavyo kishauri chama at practical thoughts,ndiyo CCM wanaiga mfumo huo!TRUE OR FALSE?

mkuu kwenye hili chezo usiingie kichwa kichwa kama vigogo wa ibange walivyoingia na ibange mwenyewe wakaja kumuingiza chaka. Hii ndio yasansi yenyewe! na bado wengi wamepanga foleni kuingia porini
 
Back
Top Bottom