Maarifa ni dawa

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
10,341
16,722
Kuna wakati unataka kufanya jambo fulani, unashindwa. Kuna wakati unatamani kuwa mtu wa aina fulani, unashindwa. Unashindwa kutokana na vifungo. Vifungo vya kifikra na imani vilivyo na misingi toka kwenye mazingira yako. Mazingira yako hayaruhusu ukue. Mazingira hayaruhusu mabadiriko. Mwisho wa siku unadumaa kifikra na imani. Hugundui mambo mapya. Maisha yako yanatabirika. Ukitoka hapa, utaenda pale na kuishia kule. Mwisho. Unayachukia maisha kwakua hayakufanyi ufikiri raha ya kuishi bali hofu ya kifo kila mda. Mtumwa. Ndio, utumwani. Hakuna tumaini, limepotea.

Kuna yule rafiki ambaye unampenda na kumuamini. Ambaye kila unapotaka kufanya kitu hukosoa na si kukutia moyo. Hushusha thamani na si kuongeza. Kuna yule ndugu yako. Ambaye yeye kila siku hujitafutia mabalaa bila kujali madhara yake. Hukuletea habari za hudhuni kila siku. Unaumia moyo. Unarudi nyuma. Unakua dhaifu. Kuna yule mpenzi wako. Ndio, mpenzi wako. Ambaye mnatofautiana sana kimtazamo. Haendani na ndoto zako. Unapopita huku, yeye anaona njia ni ile. Unafadhaika. Unavunjika moyo. Kuna jamii. Hakika jamii ya watu unapoishi. Imekosa imani na sura zao zimekosa nuru. Jamii ambayo haiamini katika ushindi. Jamii ambayo haiamini katika ushujaa. Kila kitu kwao hakiwezekani isipokua umaskini, uchungu na kifo tu. Inakutia giza usoni, unashindwa kwenda. Unakata tamaa, unarudi shimoni. Ndoto zinakufa, nawe unakufa na kubaki ukidumu tu. Tafsiri ya maisha yako inabaki katika pumzi, kula na kunywa. Unafurahia, wala hujawahi kufurahi.

Giza. Giza nene. Hakuna pakutokea. Hapa ndipo unapohitaji sana mapinduzi. Ni kweli kwenye maisha yetu tunahitaji watu kuwa na furaha. Tunahitaji watu kwakua sisi ni watu. Lakini hitaji letu halimaanishi tunamuhitaji kila mtu. Achilia mbali ukaribu wa damu, urafiki au hisia. Ili kukua tunahitaji kukaa mbali na watu au jamii ambazo ni kiwanda cha habari mbaya. Watu ambao ni chachu ya maumivu na kukata tamaa ndio njia ya kudumaa na kufa ilihali tunapumua. Ili kukua tunahitaji watu wenye roho ngumu kando yetu. Tunahitaji watu wenye jicho la Tai. Watu wanaoweza kuona mbali achilia hali iliyopo kwa muda husika. Tunahitaji watu wanaoweza kuona mema hata kwa mtu aliyekosa. Tunahitaji watu wanaoweza kuona fursa katika janga.

Watu wengi hushindwa kukua kwakua muda mwingi hutumia katika kusema watu, kuchunguza maisha ya watu na umbea, kutafuta habari mbaya, kubishana, kupinga, kudharau, kujidharau na kuona kwamba vitu wanavyovifikiri haviwezekani. Hushindwa kukua kwasababu ya kukosa mawazo endelevu na kuishi na watu ambao wamekosa mawazo mbadala. Watu wanaodhani kukua ni umri, kuishi ni pumzi na kuendelea ni kuwa na mali.

Ni wakati wa kufanya mapinduzi. Chagua watu sahihi wanaokuzunguka. Watu watakaokusaidia kukua na si watakaokusaidia kufa. Unawafahamu kulingana na ndoto zako.

Maarifa ni Dawa.

Joshua Mwantimwa
 
Asante muungwana!
Dunia hii watu wote sahihi na wasio sahihi utakutana nao tu, huwezi kuwakwepa.

Tuishi kwa kuwaelewa watu huku waliojaliwa hekima wawe nguzo kwa wasio na hekima.
 
Kabisa
 
Those who can't change their minds can't change anything.-George Bernard Shaw.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom